kuwekeza kwenye Maombi

\"\"

Biblia Inatufundisha Juu Ya \”KUWEKEZA KWENYE MAOMBI\” Au \”MAOMBI YA AKIBA\” Kama Ayaitavyo Baba Na Rafiki Yangu Mwl Mwakasege… Haya Ni Maombi Ambayo MWAMINI Anayaomba Kabla Ya Kufikia Jambo Fulani, Au Maombi Ya Ulinzi; Dhidi Ya Majaribu, Changamoto Za Maisha Nk… Mfalme Daudi Aliwahi Kulizungumzia Hili Pale Aliposema, \” Kwa Hiyo Kila Mtu Mtauwa [Msafi Wa Moyo, Alijitenga Na Uovu] Akuombe Wakati Unapopatikana. Hakika Maji Makuu Yafurikapo, Hayatamfikia Yeye\” (Zaburi 32:6).
Jenga Mazoea Ya Kuomba \”KILA WAKATI UNAPOPATIKANA\” Maana Tumehakikishiwa Kuwa, \”MAJI MAKUU [Majaribu, Changamoto Za Maisha, Magumu] YATAKAPOFURIKA HAYATATUFIKIA SISI\”
Shetani Na Kuzimu Hawashindani Na Kila Anayejiita Mkristo, Bali Wanajitahidi Sana Kushindana Na Kila Mkristo ANAYEDUMU KWENYE MAOMBI, Maana Huyo Ni Mtu Hatari Sana, Hakuna Mtego Wa Siri Utakaomnasa Wala Wavu Utakaomtega, Maana Anakuwa Na Taarifa Za Ziada Kabla Ya Wakati Wenyewe!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *