Una Uamuzi Wa Kufanya Chochote Kwenye Maisha; Na Hakuna Atakayeingilia Maana Ni Maisha Yako… Lakini Athari Utakazopata Zitakuwa Dhahiri Kwenye Maisha Yako!
Uamuzi Ni Wako, Upige Kelele, Utukane Au Umlaumu Kila Utakaye, Useme Kila Neno Hasi, Uzungumze Na Kukashifu Kwa Maneno Yako Kwa Kadri Uwezavyo, Lakini Hali Yako Haitabadilika, Wala Hautapata Hata Nafuu Ama Ahueni… Ila Unaweza Kufanya Uamuzi Wa Maana, Uamuzi Wa Hekima, Uamuzi Wa Busara, Wa Kuzungumza Maneno Ya Uzima Kwenye Kila Eneo La Maisha Yako Lililokufa, Uzungumze Maneno Chanya Kwenye Kila Eneo Hasi La Maisha Yako, Uzungumze Habari Njema Kwenye Kila Eneo La Maisha Yako Linaloonekana Lina Habari Mbaya… Mungu Amekuumba Ukiwa Na Sura Na Mfano Wake; Yeye Alikuumba Ukiwa Na Uwezo Kwenye Ulimi Wako… Utakachosema Kwa Kumaanisha, Kwa Imani Na Kwa Dhati, Kitatokea Kwenye Maisha Yako… Kitakuwa Dhahiri, Ipo Siku Utakikamata Mkononi, Utakiona Kwa Macho Na Kumtukuza Mungu!
Kumbuka Baba Yako, Mungu Aliye Hai, Huwa Anayaumba Matunda Ya Kinywa Chako (Isaya 57:19).
Hakika Ukisemacho Kitayaamua Maisha Yako, Ukisemacho Kitaweka Mpaka Wa Maisha Yako, Utayapata Uyasemayo!