Namshukuru Mungu Kwa Maana HAKUNA HATA MTU MMOJA ALIYEMUUMBA AKIWA TAYARI AMEMPANGIA MPAKA WA MAISHA YAKE…. Hapana, Mungu Amemuumba Kila Mtu Akiwa Na Sura Na Mfano Wake (Mwanzo 1:26). Halafu Kila Mmoja Wetu, Mwanamme Kwa Mwanamke, Mungu Ametuwekea Ndani Yetu BARAKA YAKE Ya Kuzaa Na Kuongezeka [ To Be Fruitful And Multiply] (Mwanzo 1:27-28). Kiwango Cha Maisha Yako Na Ubora Wako Utategemea Na Kumjua Kwako Mungu (Ayubu 22:21, Danieli 11:32b). Jinsi Unavyoyatunza Mahusiano Yako Na Mungu Kiasi Kwamba Anakuwa Msaada Kwako Ili Utende Mambo Makuu (Zaburi 60:12)… Lakini Inategemea Na Kiasi Gani Cha Neno La Mungu Umelisikia, Kuliamini, Kulitenda Na Kuliishi, Ili Likusaidie Mvua, Upepo Na Mafuriko Ya Maisha Yanapokuja Yasikuondoe, Yasiondoe Amani Yako Na Furaha Yako Ya Maisha (Mathayo 7:24-27)... Na Pia Mtazamo Sahihi Wa Maisha Alionao Mtu Unaamua Kiwango Cha Maisha Atakayokuwa Nayo Na Kuyafurahia; Maana Ajionavyo Mtu Nafsini Mwake Ndivyo Alivyo, Hauwezi Kuwa Bora Zaidi Ya Mtazamo Wako (Mithali 23:7)!