Yesu aliwahi kuwaambia WANAFUNZI WAKE,
\”MASIKINI mnao siku zote…\”
Hakuwahi hata mara moja kusema WANAFUNZI
WAKE ni MASIKINI wala YEYE MWENYEWE…Alis
ema MASIKINI MNAO SIKU ZOTE…Kama wewe
ni mwanafunzi wa Yesu Kristo, mwana wa
Mungu na mrithi wa ahadi za Mungu pamoja na
Kristo Yesu hauruhusiwi kufikiri hata mara
moja kwamba unaweza kuja kuwa masikini…ila
unaruhusiwa kufikiri juu ya MASIKINI
TULIONAO SIKU ZOTE, waliotuzunguka, ambao
ni wajibu wetu KUWAKUNJULIA MIKONO
YETU…
Uamuzi wa kwenda mbinguni ukiwa MASIKINI
AU TAJIRI NI WAKO…Ibrahimu na Lazaro wote
walikuwa watakatifu na marafiki wa Mungu
lakini Ibrahimu alikuwa tajiri hapa duniani na
Lazaro alikuwa masikini…Mungu alikuwa
Mungu wao wote, rafiki wao wote, mwezeshaji
wao wote, lakini Ibrahimu alimwelewa Mungu
kwa hatua ya ziada na kumfaidi ili hali Lazaro
akiishi kama ombaomba wakati Mungu wake ni
mmiliki wa FEDHA NA DHAHABU NA VYOTE
VIIJAZAVYO NCHI (Zaburi 24:1)!