MUNGU aliwahi kuwaambia..

MUNGU aliwahi kuwaambia WAISRAEL
[WAEBRANIA]…\”MASIKINI HAWATAKOMA JUU
YA NCHI\”
Ila hakuwahusisha wao WAEBRANIA na huo
UMASIKINI…Aliwapa tu wao taarifa juu ya
uwepo wa MASIKINI kati yao na pia
akawahimiza kuwasaidia!
Mungu hakuwahi kumuona MWEBRANIA [Mzao
wa Ibrahimu rafiki yake] akiwa MASIKINI…Ndio
maana aliwapa angalizo hata kabla ya kuingia
KANAANI kuwa WATAKAPOKUWA WAMEINGIA
NCHI HIYO NA KUSTAWI, NA KUFANIKIWA
KATIKA MAENEO YAO YOTE, WASIJE
WAKAMSAHAU YEYE MUNGU WA BABA YAO
IBRAHIMU ALIYEWAPA NGUVU/UPAKO WA
KUWA MATAJIRI
(Kumbukumbu 8:12-18)!
Ashukuriwe Mungu kwani hiyo haikuishia kwa
WAEBRANIA WA KUZALIWA TU…HAPANA…KILA
ALIYE WA KRISTO NI MZAO WA IBRAHIMU NA
MRITHI WA AHADI YA IBRAHIMU (Wagalatia 3)!
Nitashangaa sana kukuta Mkristo unawaza juu
ya hali ya uchumi wako na kesho yako
itakuwaje…Wewe ni MWEBRANIA, MRITHI WA
BARAKA ZOTE AMBAZO MUNGU ALIMPATIA
IBRAHIMU (Mwanzo 12, Mwanzo 15)…Mpo
matajiri wenzangu? Usijisumbue ULE NINI,
UVAE NINI, UNYWE NINI haya mambo hata
Mataifa/Masikini huyatafuta…Kila siku waza
namna gani utawasaidia Masikini na
Kumkopesha Mungu ambaye mwisho wa siku
atakulipa kwa tendo lako hilo jema (Mithali
19:17)!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *