Usinyooshe kidole chako dhidi ya ndugu zetu Waislamu kwa ajili ya kile kilichotokea

\"mbagala\"

\"mbagala\"

Usinyooshe kidole chako dhidi ya ndugu zetu Waislamu kwa ajili ya kile kilichotokea kule Mbagala, kama umeandika ujumbe au chochote kwenye wall yako kwa sababu ya hasira na hisia na jazba, baada ya kupokea taarifa za tukio hilo, nenda kafute hicho, Mkristo ni Mpatanishi na si wa machafuko kama Mungu asivyo wa machafuko…haitakuja kuingia akilini kwamba watu wazima wenye akili timamu, na ufah

amu mwema wa kujua jema na baya na kujua sheria na taratibu na mkono wa dola kama wanaweza kwenda kituo cha Polisi kufanya vurugu kwa sababu ya kosa la mtoto. Lazima kuna NGUVU ya kiroho nyuma yao iliyowafanya wasifikiri vema na kuchukua maamuzi ya UHARIBIFU badala ya taratibu za kawaida za kisheria na za amani. Hii si vita ya Waislamu na Wakristo. Waislamu ni kaka zetu na dada zetu. Wao ni ndugu zetu kabisa. Hatuna ugomvi nao hata kidogo, wao ni watu wetu wa karibu na wa muhimu kwa maendeleo yetu na ustawi wa taifa letu. Hii ni vita ya rohoni, ambayo athari zake tunaziona kwenye macho yetu ya nyama. Shetani na Jeshi lake wako nyuma ya hili na wanajaribu kuficha UKWELI WA MAMBO kwa kuiita VITA YA DINI.
Kanisa lazima liamke, lichukue nafasi yake, limkanyage nyoka na ng’e wake wote na nguvu zote za adui

(Luka 10:19).

Hii ni vita ya ROHO MTAKATIFU dhidi ya roho za uharibifu toka kuzimu!
Wale jamaa wa UAMSHO waliliamsha KANISA [mimi na wewe] LAKINI badala ya kuwa macho na kulinda, tumelala na kuacha ADUI APANDE MAGUGU katikati ya ngano!
Kamwe usishughulike na MATAWI YA TATIZO [Waislamu] BALI SHUGHULIKA na MIZIZI [Malango ya Kuzimu yasiyoweza kulishinda kanisa kamwe, japo yanajaribu kupigana]…Ni vema tukue katika kuyajua mambo ya rohoni na namna ya kuyashughulikia kwa njia za rohoni na si maneno, jazba na hisia na hasira!

Salaam zangu kwa kanisa, toka juu sana nilikoketi na Kristo Yesu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *