NAIPENDA SANA DUNIA YANGU IITWAYO IMANI…
Hii ni dunia halisi isiyoendeshwa kwa kile ambacho macho yanaona au masikio yasikia…Wenyeji wa dunia hii tunaishi kwa kile kinachotoka kwenye kinywa cha Mungu [NENO LA MUNGU].
Tunatembea hata kama dunia inasema simama, ilimradi kinywa cha Mungu kimesema tembea…Tunastawi sana na kuchanua hata kama dunia inasema, \”Haiwezekani, uchumi umeporomoka, hali ni mbaya\” …Tunakuwa na afya na uzima muda wote hata kama dunia inalia kwa kila namna ya ugonjwa na maradhi, kwa sababu Mungu mwenyewe ni \”MUNGU ATUPONYAYE\”…Tunafanya yale ambayo dunia inasema hayawezekani kwa vile Mungu amesema, \”KWA MSAADA WANGU MTATENDA MAKUU\”…Tunapita kwenye changamoto na ugumu kama wengine walio hapa duniani lakini hatuko katika msiba wao kwa sababu Mungu ametuhakikishia, \”UJAPOPITA KATIKA MAJI MENGI HAYATAKUGHARIKISHA WALA KATIKA MOTO HAUTAKUUNGUZA\” …Wakati dunia inasema ili ufanikiwe sera yetu ni WHOM YOU KNOW, Mungu anatwambia sisi, \”MSIWE NA SHAKA, MNANIJUA MIMI, INATOSHA, MTAKUWA NA AMANI, NA MEMA YATAWAJIA\”…Dunia inaposema unajua Mnajinyima raha na mnapitwa na wakati, Mungu anatunong’oneza, \”MSIWE NA SHAKA, YOTE YATAPITA LAKINI NENO LANGU HALITAPITA KAMWE…NINALIANGALIA NENO LANGU ILI NIPATE KULITIMIZA…MIMI SI MTU NISEME UONGO WALA SI MWANADAMU NIJUTE…LIAMINI NENO LANGU HALITAWAANGUSHA\”…Dunia inaposema Ni ngumu kuwa mtakatifu, mmevaa mwili, Mungu anatusemesha mioyoni mwetu kwa Furaha, \”MSIWE NA SHAKA, SIHITAJI JUHUDI YENU ILI NIWAKUBALI KUWA NINYI NI WATAKATIFU WANGU MPENDWAO…NILISHAMFANYA YESU ASIYEIJUA DHAMBI KUWA DHAMBI ILI NINYI MFANYIKE HAKI YANGU…HAKUNA WA KUWAHUKUMU, MIMI MWENYEWE NDIYE NINAYEWAHESABIA HAKI…\”
Hii ni Dunia yangu bora ninayokaa ndani yake, huwezi kunitoa hapo, huwezi kunibadilisha, huwezi kwa neno lako lolote au kwa tendo lako lolote…HUU NI MFUMO WANGU WA MAISHA, UKO KWENYE ROHO YANGU NAFSI NA MWILI WANGU…NI SEHEMU YA DAMU YANGU…NI UZIMA WA MUNGU [ZOE] NDANI YANGU