Siku ukigundua ulichoumbwa kufanya

\"image\"

SIKU UKIGUNDUA ULICHOUMBWA KUFANYA DUNIANI, UTAKUWA MTU HATARI KWA WATU NA HATA KWA SHETANI…
Yesu alipokuwa hapa duniani, alikaa kama mtu wa kawaida kwa muda wa miaka 29…Alipofikisha umri wa miaka 30, majira na muda sahihi ambao Mungu alimkusudia kuanza rasmi kazi ya kulitumikia kusudi la maisha yake, na Yeye Yesu alipodaka ndoto (Vision) ya Mungu maishani mwake na kisha akatangaza rasmi kule Kapernaumu, \”ROHO WA BWANA YU JUU YANGU, MAANA AMENITIA MAFUTA KUWAHUBIRIA MASIKINI HABARI NJEMA, KUWATANGAZIA UHURU WALIOFUNGWA, KUWAFUNGUA WALIOSETWA, NA KUTANGAZA MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIKA…\” (Luka 4:18-19).
Siku zote ukigundua KUSUDI LA UWEPO WAKO DUNIANI, UKAIONA PICHA YA NDANI YA WEWE HALISI, NA ROHO WA MUNGU AKAKUPA AMANI NA UHAKIKA…UNASHINDWA KUKAA KIMYA, UNAJIKUTA UNAAMINI HICHO HATA KAMA WOTE WALIOKUZUNGUKA HAWAELEWI USEMACHO AU WANAONA KAMA UMECHANGANYIKIWA…Yesu alipodaka ndoto ya Mungu juu ya maisha yake na kuidhibitisha, alishindwa kukaa nalo moyoni…aliamua kwenda hekaluni na kulitangaza mbele za wale watu kwa Ujasiri…Wengiwalimwona kama amechanganyikiwa…wengine walimkasirikia na kumkamata na kutaka kumuua…Unapodaka ndoto (Vision) ya Mungu…Marafiki hawatakuelewa, Ndugu zako hawatakuelewa, Wazazi wako hawatakuelewa…Kama ilivyokuwa kwa YUSUFU au kwa DAUDI…Ndoto ya Mungu (Vision) ni kubwa mno, haiwezi kuingia ndani ya mawazo ya mtu, haieleweki kwa Yeyote isipokuwa wewe uliyeibeba…Baadhi ya watu wataanza kupata picha pale unapoweka SKELETON/BLUE PRINT mezani NA HAO NI WACHACHE SANA…Lakini wengi wataelewa pale yatakapokuwa halisi…Ndio wanazinduka usingizini kwa mshangao, watasema, \”KUMBE HUYU FULANI ALIKUWA AMEBEBA HAYA YOTE NDANI YAKE? KUMBE HAKUWA MTU WA KAWAIDA? DAH JAMANI…\”
Bill Gates alikuwa kijana wa kawaida tu…ila alipogundua njozi ya Mungu maishani mwake…
Henry Ford alikuwa mtu wa kawaida sana, tena hakuwa na elimu kubwa kama baadhi yetu tulizonazo, lakini alipogundua Njozi ya Mungu maishani mwake…
Benny Carson alikuwa kijana wa familia masikini ya Wamarekani weusi, alipogundua Njozi ya Mungu kwake…
Steve Jobs, Abraham Lincoln, Smith Wigglesworth, Kathreen Kuhluman, Benny Hinn, Bill Graham, na wengine wengi hata wale ambao ni ROLE MODELS wako, Waligundua Njozi ya Mungu kwao ndio maana Dunia na Mazingira hayawezi kuwaficha!
UKIGUNDUA NDOTO YA MUNGU KWAKO, UNAKUWA MTU HATARI SANA…HAIJALISHI UMRI WAKO…ELIMU YAKO…HISTORIAYAKO nk

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *