Wakati naingia kwenye UWANJA WA UTUMISHI WA MADHABAHUNI,kiu yangu kubwa ilikuwa ni kuona Miujiza ikifanyika,Wagonjwa wakiponywa nk.Nilikuwa tayari Kufunga na kuomba kwa siku kadhaa lakini sikuwa nikiliruhusu NENO LA MUNGU NA ROHO MTAKATIFU Wanishughulikie!
Siku ukiamua Kuyafisha MAPENZI NA MATAKWA YAKO YA KIBINADAMU, na kujitoa Roho, Nafsi na Mwili chini ya UTAWALA wa Roho Mtakatifu na Neno la Mungu. Maisha yako yataanza kufanya MIUJIZA YOTE aliyofanya Yesu na kudhihirisha SURA na MFANO HALISI wa MUNGU.
