Hakuna Roho Mtakatifu Robo Au Nusu Ndani Ya Mwamini… Roho Yuleyule Aliyekuwa Ndani Na Juu Ya Kristo Yesu Ndiye Anayekaa Ndani Yako Wewe Uliyeokoka… Roho Yuleyule Aliyemfufua Yesu Kwa Wafu Ndiye Anayekaa Ndani Yako… Ila Utendaji Wake Na Udhihirisho Wa NGUVU ZAKE, HEKIMA YAKE, UFAHAMU WAKE, UWEZO WAKE, MAARIFA YAKE, UPENDO WAKE Nk Vitaonekana Kwenye Maisha Yako Kwa Kiwango Tofauti Na Kwangu Kutegemeana Na Namna Ambavyo Tunamwelewa, Tunajua Kumtumia Na Kumtumikia, Namna Tunavyotunza Ushirika Naye Nk… Anayekwenda Ndani Zaidi Anakuja Na Uzoefu Zaidi… Ni Swala La Kulipa Gharama Tu, Mtaji Tayari Unao!