Tai

\"\"

Jambo La Kwanza Wanalofanana TAI Na Ndege Wengine Ni Kwamba Wote Ni Ndege… Kama Ambavyo Mkristo Aliyeokoka Alivyo Binadamu Kama Binadamu Wengine Kwa Sababu Ya Mwili Aliovaa… Jambo La Pili Ambalo Tai Na Ndege Wa Kawaida Wanalofanana Ni Kwamba Wakati Wanaporuka Kuelekea Juu, Wote Wanapigapiga Mabawa Yao… Sawa Na Jinsi Ambavyo Mtu Aliyeokoka Anavyolipa Gharama Kuelekea Mahali Pa Ukuu Kama Wafanyavyo Pia Wanadamu Wengine Wa Kawaida… Ila Tofauti Ya TAI Na Ndege Wengine Inakuja Wakati Wanapofika MAHALI PA JUU; Tai Hapigipigi Mabawa Yake Ili Kutunza Nafasi Yake Na Asivutwe Kurudi Chini, Bali Wale Ndege Wa Kawaida Wanalazimika Kupigapiga Mabawa Yao, Wakichoka Wanaporomoka Na Kurudi Chini, Bali TAI Ananyoosha Tu Mbawa Zake Halafu Anaanza Kuelea Akiwa Anapelekwa Huku Na Huku Na Msukumo Wa Upepo, Bila Kuchoka Wala Kurudi Chini… Ndivyo Ilivyo Kwa Mtu Aliyeokoka, Yeye Akishapandishwa Mahali Pa Juu, Hatoki Hapo Ng’o Maana Ameandikiwa Kuwa Juu Tu Na Wala Sio Chini; Binadamu Wa Kawaida Asiye Na Yesu, Akifika Juu, Inabidi Atumie Namna Zote Na Mbinu Zote Kuweza Kubaki Juu, Atatoa Rushwa, Ataua, Atadhurumu, nk Ili Kulinda Nafasi Yake, Lakini Siku Nguvu Zake Zikiisha, Anaporomoka Na Kurudi Chini Tena… \”Bali Wamngojao BWANA Watapata Nguvu Mpya; Watapanda Juu Kwa Mbawa Kama TAI; Watapiga Mbio Wala Hawatachoka; Watakwenda Kwa Miguu, Wala Hawatazimia\” (Isaya 40:31)!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *