Aina za watoa sadaka na mitazamo iliyo mioyoni mwao; 1.Wanaotoa kwa sababu wanajua Mungu atawarudishia maradufu…hawa wanatoa wakiwa na wazo la kutumia sadaka kama chambo cha kupata pesa au uchumi mzuri toka kwa Mungu (hawatoi kwa vile wanampenda Mungu wao na wana mioyo ya shukurani, bali wanajaribu kuitumia sadaka kama kitega uchumi kupitia nini watapata kama matokeo ya utoaji wao) 2.Wanaotoa sadaka kama utaratibu wa dini au dhehebu lao…hawa wanakwenda kanisani na wanatoa ilimradi tu…kwahiyo hawaangalii
UBORA wala KIASI cha matoleo…hawa wanatoa hata CHENJI zilizobaki kwenye nauli au manunuzi ya dukani…hawa ni wapoteza muda tu 3.Wanaotoa ili wajioneshe au wapate sifa kwa Mchungaji au Washirika…hawa hawatoi sadaka, wanafanya matangazo tu 4.Wanaotoa sawasawa na msukumo/sauti ya Mungu ndani yao…Hawa ndo watoaji hasa, hawatoi kwa sababu ni muda wa kutoa au kwa vile wamehubiriwa somo la utoaji…bali wanatoa kutii sauti/ msukumo alioweka Mungu ndani yao…hawa ndo wale wanaomtolea Mungu kwa moyo wa kupenda…hawa wana tabia ya kumuuliza Mungu juu ya kila shilingi ipitayo mikononi mwao (asomaye na afahamu) 5.Wanaotoa sadaka kutegemeana na huduma au mtumishi…hawa wanatoa si kwa lengo la kumgusa Mungu bali wanatoa kwa sababu ya jina la huduma au mtumishi… JE WEWE UKO NAMBA NGAPI? Wewe, Mungu na shetani mnajua uko wapi..!