YATAKAYOKUWAKO YAMEKWISHA KUWAKO…

Ni muhimu ujue jambo hili wewe ambaye Yesu ni Bwana na Mwokozi wako, na wewe ambaye Mungu ni Baba yako kupitia kwa Kristo Yesu!
Kila utakalo kwa ajili ya Maisha yako ya kila siku na kwa ajili ya utauwa, vyote umeshatengenezewa hata kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa…Ndio maana Biblia haisemi tutabarikiwa, bali inasema, \”ATUKUZWE BABA MUNGU, BABA WA BWANA W

ETU YESU KRISTO ALIYETUBARIKI KWA BARAKA ZOTE ZA ROHONI\”
Unaweza kuniambia \”Lakini Mwalimu, si ni za rohoni na hajasema za mwilini?\” Jibu langu kwako ni hapana, anaposema za ROHONI anazungumza kwa lugha ya kiungu (divine language) akitaka kuweka msisitizo kuwa kila kinachoonekana hapa duniani kina msingi wake kwenye ULIMWENGU WA ROHO…Kwa sababu VITU VILIVYO DHAHIRI[Vinavyoonekana] vimetokana na VITU VISIVYO DHAHIRI[visivyoonekana]…
Mungu amekupa NAFASI YA KUAMUA KIASI CHA KIWANGO GANI CHA MAISHA UNATAKA UISHI UKIWA HAPA DUNIANI…KIWANGO CHAKO CHA MAISHA HAKIWEZI KUWA ZAIDI YA VILE UNAVYOJIONA NAFSINI MWAKO NA KUKIRI MBELE ZA WATU KILA SIKU BILA KUJALI UNA NINI MKONONI, UNAMILKI NINI AU UNA KIWANGO GANI KINACHOONEKANA KWA MACHO NA KUSHIKIKA KWA MIKONO…Kwa kuwa, \”AJIONAVYO MTU NAFSINI MWAKE; NDIVYO ALIVYO\”
Usije kufanya kosa la kuyatafsiri, au kuyaamua maisha yako kwa kile ulichonacho au hali yako ya maisha ya sasa…Thamani ya mtu haiko kwenye kile alichonacho bali katika KILE AWEZACHO KUFANYA…Kwangu ni bora kuwa na rafiki MASIKINI MWENYE HEKIMA NA MAWAZO YASIYODHIBITIWA AU KUTATIZWA NA KILE ANACHOKIONA, AU KUKIPITIA KWENYE MAISHA kuliko kuwa rafiki wa TAJIRI MKUBWA ASIYEWEZA KUONA TENA MBALI, NA ANAYELIA KILA APATAPO CHANGAMOTO AU SHIDA!
Kila kitu ambacho unakitaka kwenye maisha yako, kipo tayari, kiko hatua chache kutoka hapo ulipo, usipojua hilo utakula kila makombo, na mataputapu yanayokuja mbele zako!
Mungu aliye hai, Baba yako, ametangaza mwisho wako tangu mwanzo wako (Isaya 46:9-10)
Alikujua hata kabla ya mimba yako haijatungwa tumboni kwa mama yako (Yeremia 1:4-5)
Mimba yako ilitungwa kwanza kwenye mawazo ya Mungu kabla ya kutungwa kwenye tumbo la mama yako, wala kabla haujawekwa kwenye viuno vya baba yako…Mwamini Mungu, Anakuwazia mawazo mema na ya amani, kukupa tumaini kwenye siku zako zijazo (Yeremia 29:11)
MWAMINI MUNGU, MWACHE ATENGENEZE KESHO YAKO!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *