KUTANA NA ROHO MTAKATIFU…
Imeandikwa katika 2Kor 2:12, \” Hatukupokea roho ya dunia bali Roho atokaye kwa Mungu MAKUSUDI tupate kuyajua yale tuliyokirimiwa[tuliyopewa bure] na Mungu\”
Kusudi mojawapo la Mungu kumpa Mwamini kipawa cha Roho Mtakatifu pale anapoamua kumpokea na kumwamini Yesu ni ili Roho Mtakatifu afumbue macho ya Mwamini huyo ili apate kuyajua yale ambayo Mungu tayari ametupatia sisi Waamini bure, kwa ukarimu kama zawadi iambatanayo na wokovu!
Hautaweza kujua haki zako ndani ya Kristo Yesu endapo Roho Mtakatifu hatafanya kazi yake ya kuyafungua macho ya roho yako ili ugundue na kujua yale ambayo Mungu amekupa…na kama hautajua haki zako kama Mkristo mbele za Mungu, hautaweza kuwa na maisha ya ustawi na mafanikio…maana kama haujui kuwa una kitu fulani, hautaweza kukitumia na kukifurahia maishani!
Yesu anasema yafuatayo kuhusu Roho Mtakatifu, \”Atakapokuja huyo Msaidizi, Roho wa Kweli atokaye kwa Baba, hatanena kwa shauri lake mwenyewe, atachukua katika YALIYO YANGU na kuwapasheni…YOTE ALIYONAYO BABA YANGU NI YANGU\” (Yohana 16:13,15).
Yote aliyonayo Mungu amempatia BWANA YESU, \”Nimekabidhiwa yote na Baba yangu\” (Mathayo 11:27)…atakayekujulisha yale yote aliyonayo Yesu ni Roho Mtakatifu…KAANAYE VIZURI…LINDA USHIRIKA WAKO NA YEYE…NA KAMA HAUJAWA NA UHUSIANO THABITI ANZA LEO..!