“Wenzako wote uliokua nao au kusoma nao wanaoa. Ndoa si ALISEREMA ARIJA AU MWENGE TUNAUKIMBIZA. Ndoa ni taasisi ambayo Mungu amemuwekea kila mmoja wetu ALARM ya kujua lini aingie huko na inahitaji HEKIMA ITOKAYO JUU kujua ni yupi ambaye atasababisha useme, BINTI ZA WATU WAMEFANYA MEMA LAKINI WEWE UMEWAZIDI WOTE. Sasa wewe oa kwa sababu una wanaoweza kukupa michango ya TUKIO LA SIKU MOJA (harusi), usahau kuwa KUANZIA HAPO MPAKA KIFO KINAWATENGA UTAKUWA PEKE YAKO… Ndoa si upele kila mtu ajikune. KABLA YA KUANZA UJENZI WA MNARA KAA CHINI HESABU GHARAMA KAMA UTAUMALIZA ILI USIJEKWAMA NA KUWAFANYA WATU WAKUDHIHAKI… Kurupuka uone utakavyokukuruka…”
HEKIMA ZA NDOA 5
“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza