UKITAKA KUJUA ULIPO/ UNAPOABUDU KUNA KWELI YA MUNGU AU NI NJIA PANA IELEKEAYO UPOTEVUNI, ANGALIA YAFUATAYO;

 

1. Je msisitizo mkubwa mahali hapo ni INJILI YA KUGEUZA ROHO ZA WATU TOKA DHAMBINI AU NI KITUO CHA MIRADI, MIPANGO NA HARAMBEE ZA VITU VINAVYOISHIA DUNIANI TU?

2. Je KUNA WATENDA DHAMBI WALIOBADILISHWA JUMLA TOKA MAISHA YAO MACHAFU YA KWANZA hadi KUWA USHAHIDI WA WAZI KUWA YESU ANABADILISHA AU ni mahali ambapo WATU WANAJAZANA TU, BILA KUBADILISHWA TOKA DHAMBINI, UOVU NA MAISHA YASIYOMPA MUNGU UTUKUFU?

3. Je Msisitizo wa mahali hapo ni WATU WAOKOLEWE TOKA MIKONONI MWA SHETANI, DHAMBI NA KUIPENDA DUNIA ili WAWE MASHAHIDI WA YESU KWA DUNIA YAO kwa MANENO NA MATENDO AU NI MAHALI PA KUJIVUNIA IDADI YA WATU BILA KUJALI WANAKWENDA MBINGUNI AU LA?

4. Je MTUMISHI WA MUNGU (MUASISI) WA HILO DHEHEBU/ KUSANYIKO ANATAJWA MNO, KUHESHIMIWA MNO, KUONWA KAMA MTU WA KIPEKEE, ALIYEJALIWA MNO KULIKO WENGINE au NI MNYENYEKEVU ANAYEKATAZA WATU WASIMSIFU, KUMTUNGIA NYIMBO ZA KUMUINUA, AU KUMFANYA MAALUM kuliko WATUMISHI WENGINE?

5. Je mahali hapo unapoabudu, MTUMISHI WA MUNGU ULIYENAYE ANA MAJINA MAKUBWA MAKUBWA YA KUJISIFU, KUJIINUA, KUJIWEKA JUU NA KUJIONYESHA MAALUM, halafu JINA LA YESU HALITAJWI MNO KAMA A.K.A ZAKE?
MTU YEYOTE AKITAJWA MNO KULIKO YESU, HATA KAMA KWELI ANA YESU, HALAFU AKAACHA MAJINA HAYO YAENDELEE, TAYARI AMETOKA KWENYE MSTARI AWE ANAJUA AU HAJUI!!

TUISHIE HAPA,
TUTAFAKARI HAYA LEO.
Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila

Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »