Yesu Aliwahi Kusema, \”MAKAHABA NA WATOZA USHURU WATAWATANGULIA KATIKA UFALME WA MUNGU\”
Kinachowafanya Hawa Makahaba Na Watoza Ushuru Wawe Na Uwezekano Wa Kuingia Na Kuwatangulia Wale WALIOKO KANISANI, Ni Kwa Sababu HAWA DHAMBI YAO IKO WAZI, HAWANA UFICHO, NA WAKISIKIA INJILI YA KRISTO YA NEEMA NA MSAMAHA, WANASOGEA BILA MAZOEA NA KUPOKEA UZIMA WA MUNGU KWA URAHISI!
Lakini Watu Walioko Makanisani (Watu Wa Dini) Wako Humo Na WANAENDELEA KUTAFUNWA NA DHAMBI KWA SIRI, Wanaogopa Kutafuta Suluhu, Wanaogopa Macho Ya Watu Huku WAKIENDELEA KUELEKEA JEHANAMU KIMYAKIMYA, Wanaogopa Kuwa Wawazi Ili Wasaidiwe Na Kuelekezwa Namna Ya KUTOKA KWENYE UTUMWA WA DHAMBI WALIOMO; Wako Kwenye Kwaya, Lakini Ni Wazinzi, Wasengenyaji, Wenye Kiburi, Wenye Mashindano Na Manung’uniko; Wanafundisha Kilichoandikwa Kwenye Biblia Lakini Hakijaweza Kuwabadilisha Wao, Wanamtaja Roho Mtakatifu Lakini Hata Kukutana Na Walau Mguso Wake HAKUNA!
Wakati Wa Kuigiza Na Kuishi Kwenye DINI Badala Ya YESU Umepitwa Na Wakati, Heshima Yako Mbele Za Wanadamu Haitakusaidia Kama Hautakuwa UMEANDIKWA KWENYE KITABU CHA UZIMA NA MWISHO WA MAISHA YAKO KUINGIA MBINGUNI.
Umilele Wako Unasubiri Maamuzi Yako Ya Dhati Leo, Toka Kwenye Ukristo Wa Jina Umaanishe Kumjua Na Kumuishia Yesu Aliye Hai Sasa!