UDHALIMU

Ni tabia mbaya ambayo inawatesa watu wengi.

Kama Mtu alikufanyia jambo jema, na unakumbuka alikutoa hatua moja kwenda hatua nyingine na Ukasahau au ukajisahaulisha, na Leo unamsema vibaya; hiyo ni tabia ya UDHALIMU

Kama mtu alikufanyia jambo jema na haukumbuki na kuchukulia kwa uzito kile ulichofanyiwa hiyo ni tabia ya UDHALIMU

Kama Kuna Mtu alisababisha uwe hivyo ulivyo SASA halafu leo unasema nilipambana mwenyewe hiyo ni tabia ya UDHALIMU.

Kama Kuna mtu aliwahi kukugharamikia maisha yako ya kiroho kiuchumi, alitembea na wewe kwenye hali zote, lakini leo unashindana naye hiyo ni tabia ya UDHALIMU

Hakuna Mtu aliyekua mwenyewe
Kila mtu alikuzwa !

Jifunze Kutambua Watu Waliowahi kuwa mchango wa maisha yako na waliokusaidia uwe hivi ulivyo Leo

Nenda waambie kwa kinywa chako kuwa wao ni wa thamani kwako
Andika hata kwa maandishi kuwaonyesha jinsi walivyochangia kuwa hivi ulivyo.

Utakuwa mtu wa thamani daima, siku zote za maisha yako.

Pastor Ibrahim Amasi
ABC-KAHAMA

LivingWord
@2019

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »