SIFA ZA MME BORA

 

Mwl. Dickson C Kabigumila
Mwl. Dickson C Kabigumila

1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18).

-Atambue thamani ya wokovu na kuutunza kwa dhati (Waebrania 2:3)
-Aheshimu uhusiano wake binafsi na Mungu kwanza (Yohana 17:3)
-Alitunze vazi lake la UTAKATIFU kwa kumaanisha (Zaburi 16:3, 1Petro 1:15-16),
-Aiteteee na kuishindania imani yake aliyokabidhiwa mara moja tu (Yuda 1:3)!

2. Awe AMETAMBUA ALICHOUMBWA KUFANYA DUNIANI (KUSUDI) na AMEJITOA KUKIFANYA HICHO HADI DAKIKA YAKE YA MWISHO bila kuchoka wala KUKUBALI KUSHINDWA (Yeremia 1:4-5).
-Ajitahidi atafute jambo ambalo litamtambulisha,
-Awe na kitu productive kwake, kwa Mungu, familia na taifa ambacho jina lake linatambuliwa kwacho!

3. Awe AMEFANYA UAMUZI WA KUWA MME WA MKE MMOJA TU, BILA KUJALI VITA KUBWA YA WANAWAKE WENGI WANAOPITA NA KUJIPITISHA MBELE ZAKE! Namaanisha AWE AMEAMUA KUPEVUKA KURIDHIKA NA MWILI WA MWANAMKE MMOJA TU DUNIANI anayeitwa MKEWE na si KUWA MZINZI NA MWASHERATI! Akubali KUHESABU GHARAMA NA KUJIKANA NAFSI YAKE kuwa na kuishi na MWANAMKE MMOJA TU AITWAYE- MKE WAKE!
-Ndiyo kuna pressure ya mwili,
-Ndiyo kuna pressure ya kutegwa,
-Ndiyo kuna hila za Shetani,
-Ndiyo kuna marafiki wanaokushawishi utoke nje,
-Ndiyo mitandao ya kijamii, simu vina vitu na content ambazo ZINAWEZA KUKUFANYA KAMA MWANAUME usikie kusisimka, kutamani na kutaka hata KUZINI lakini YAKUPASA USHINDE!
FANYA HIVI:
i) Mwambie Mungu kuwa unahitaji misaada wake na neema yake kukusaidia kuwa MWAMINIFU KWA MKEO PEKEE SIKU ZOTE

ii) Usiwe na mawasiliano yaliyovuka mipaka na watu wa jinsia ya kike tofauti na mkeo : Chats, Jokes, calls nakadhalika ambazo unajua ZITAAMSHA HASHIKI NA TAMAA ZA MWILI NA UKIJA KUSHTUKA TAYARI UMEHARIBU NA UKO NJIA PANDA YA KUHATARISHA NDOA YAKO

iii) Najua siku hizi wako mabinti, wanawake WANAOJILENGESHA na wamekaa kimitego mitego ilimradi tu WAMNASE MTU NA KUHARIBU MAHUSIANO YAKE NA MUNGU NA NDOA YAKE, lakini nakushauri USIJARIBU KUKABILIANA NAO PEKE YAKO, MUONESHE MKEO YA KUWA FULANI NA FULANI WANALETA UPUUZI, ILI AWE ANAJUA LAKINI ATAKUSAIDIA HATA KUWAJIBU MARA MOJA MOJA AU ATAWAPIGIA AU KUKUTANA NAO… Usiseme, MIMI NI MWANAUME, NI KIDUME NITAYAMALIZA MWENYEWE, utakuja kushtuka UNAFUNGA ZIPU YA SURUALI YAKO, muamini mkeo na JIAMINISHE KWAKE, HUYO NI MLINZI MUNGU KAKUPATIA!

iv) MPENDE MKEO

-Usione haya kumuita MKE WANGU (Maana hakika ni wako), usimuite MAMA ANNA AU MAMA MICHAEL, maana hao akina Anna na Michael NI NYONGEZA, wa kwako hasa ni MKE WAKO, Muite MKE WANGU MZURI, MREMBO WANGU, KIBOKO YANGU, KIPENZI CHANGU NAKADHALIKA (Build confidence inside her)!
-Dedicate hata siku moja kila baada ya mwezi au kila baada ya miezi miwili au mitatu MTOE OUT, HATA HOTEL FULANI, mkae tu huko, muache watoto na familia huko mbali, MKAE PEKE YENU HATA SIKU MBILI AU TATU, MKITANIANA, KUCHEZA PAMOJA, KUPATA JOTO PAMOJA MBALI NA KITANDA MLICHOKIZOEA, NA KUONGELEA MAISHA YENU YA SASA NA FUTURE YENU PAMOJA!
-Simu yako iwe na picha yake JUU KABISA YA SCREEN, ukiweza hata ACCOUNT ZAKO za mitandao PICHA YAKE IWEPO PALE kila mtu ajue WEWE SIO SINGLE!
-Kaa na tembea na PETE YAKO YA HARUSI KILA MAHALI, usipende kuvua pete hata kama UNAOGA, ichukulie kwa uzito na kuheshimu AGANO ULILOFANYA MBELE ZA MUNGU NA MBELE YA MASHAHIDI WENGI, na IAPIZE NA KUIFUNDISHA AKILI YAKO YA KUWA ILE PETE NI UWAKILISHI WA AGANO LILILO MBELE ZA MUNGU NA KATI YAKO NA MKE hivyo HUTAKIWI KUFANYA UPUUZI WOWOTE!
-Mheshimu mkeo (Mpe mkeo heshima), hili ni agizo halali la NENO LA MUNGU katika kitabu cha 1PETRO 3:7, ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU!
Usitake heshima bila wewe kutoa heshima kwanza kwa mkeo! Mkeo anastahili heshima, AMEFANYA UAMUZI MGUMU WA KUJA KUISHI NA WEWE MBALI YA MAPUNGUFU MENGI ULIYONAYO!

v) Wajibika kujali, kuhudumia na kutunza FAMILIA YAKO!
Maandiko yanasema, “ASIYEWATUNZA WALIO WAKE, HASA WALE WA NYUMBANI MWAKE, NI MBAYA KULIKO ASIYEAMINI (MPAGANI) NA AMEIACHA IMANI” (1Timotheo 5:8)!

-Toa mahitaji ya kila siku kwa kadri ya kipato na uwezo ulionao
-Hakikisha watu wa nyumba yako wanauona uso wako na uwepo wako kuliko pesa yako (Wewe ni wa muhimu kwao kuliko pesa yoyote)!
-Usile nyama choma na kitimoto peke yako barabarani halafu nyumbani wanakula dagaa, ukija unadai hujisikii kula au unazuga zuga, huo si ubaba bali inaonesha wewe ni mvulana aliyekimbilia kuwa na majukumu ya ubaba na familia bila kupita shule ya Neno na maisha!

Tuishia hapa kwa leo,
Ni mimi mwanaume mwenzenu,
Mme wa mke na baba wa familia,
Mchungaji kiongozi,
Assembly Of Believers Church (ABC) GLOBAL.
17/06/2019

Nifuate WhatsApp: 0655 466 675

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »