Kama Hauwezi Kumtii Mungu Kwenye SADAKA, Hasa AHADI/ NADHIRI Na Fungu La Kumi, Sioni Ni Kwa Namna Gani Utaweza Kumtii Mme Wako Kama Kumtii Kristo!
Kama Hauwezi Kumpenda Mungu Kwa Mali Yako, Muda Wako, Moyo Wako Na Nguvu Zako Zote Sioni Ni Kwa Namna Gani Utaweza Kumpenda MKEO Kama Kristo Alivyolipenda Kanisa!
Mwanamke, utii Wako Kwa Mungu, Utaamua Utiifu Wako Kwa Mmeo!
Mwanaume, Upendo Wako Kwa Mungu Utaamua Upendo Wako Kwa Mkeo!
Maana Hauwezi Kusema Unampenda Mungu Usiyemwona Wakati Kuna Wanadamu Hapo Jirani Hauongei Nao, Kisa Madhehebu Yao, Dini Zao, Makabila Yao Au Kwa Vile Hutarajii Msaada Wao!
BIBLIA NI MAISHA YA KILA SIKU KATIKA WEPESI KAMA HUU; SI MAANDIKO KWENYE KURASA ZA KITABU!