NDOO YENYE MATUNDU HAIJAZI MAJI!!

NDOO YENYE MATUNDU HAIJAZI MAJI!!

(USHUHUDA WANGU UTAKAO KUJENGA)

  Wakati fulani nikiwa mchanga kiroho nilikuwa nina juhudi kubwa sana ya KUSOMA NENO LA MUNGU na KUOMBA na kusoma vitabu vya kiroho vya watumishi wa kweli wa Mungu na kusikiliza MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU na kutazama VIDEO ZA MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU na Mahubiri mbalimbali hii ilinijenga sana kiroho na kunifanya kutumia muda mwingi sana na Mungu Lakini sikuwa najua kufanya hivyo nakusanya nguvu za Mungu Ndani yangu!

Nakumbuka nilivutwa kwenda kushuhudia nyumba moja wapo iliyokuwa jirani na nyumbani,kulikuwa na mgonjwa hatembei ni wa kubeba wa kumtoa nje na kumuingiza ndani!

Siku niliyoenda walikuwa wamemtoa nje yule mgonjwa nilimshuhudia habari za Yesu na nilimwambia ikitokea amekufa nje ya Yesu (kufa akiwa hajaokoka anaelekea pabaya sana kwenye mateso ya milele)!
Alinisikiliza na Baadae wakamuingiza ndani (maana nilikaa mpaka giza lilipo ingia)

Nilipoingia sebuleni nikawa naendelea kumshuhudia yule baba (Kwa sasa ni MAREHEMU) hakutaka kukubali moja kwa moja, baadae nilihamisha injili kwa dada wa kazi wa ile nyumba,nilimueleza habari za wokovu na kwanini anatakiwa kuokoka, Yule dada alikubali kuokoka na akawa tayari tuombe pamoja!
Tuliomba pamoja na akampokea YESU huku yule baba akitazama,sasa baada ya kumuongoza maombi nikamwambia naomba nikuombee,nikamshika mkono ile naanza kuomba na kumuita Yesu juu ya maisha ya huyu binti akaanguka chini, moyoni niliogopa nikajiuliza hii nini, kumbe ni mapepo,sikutumia hata dakika tano Bwana YESU alimfungua yule binti!
Baadae yule baba akaomba nimuombee,nikamuombea nikamwambia asimame akawa anashangaa, nikamshika mkono akasimama Mungu akamtia nguMung
(Lakini huyu baba licha ya Bwana kumtendea muujiza aligoma kuokoka,sina uhakika mpaka anakufa aliokoka maana niliondoka huko)

Baada ya muda nikajikuta nikienda kufanya huduma au kumuombea mtu kama anapepo hata moja linanitoa jasho,nakemea weee,naweza kutumia masaa kutoa pepo moja ndani ya mtu au wakati mwingine halitoki kabisa! Nilikosa amani sana, nikajikuta naanza kuota ndoto ambazo kabla sijaokoka nilikuwa naziota,yaani naota nakimbizwa,mara napigana na watu harafu nashindwa ndani ya ndoto,naota nafanya mapenzi na mwanamke nisiyemjua,nikiamka nakemea ile ndoto,nimatafuta Masomo ya kushughulikia ndoto mbaya Lakini inakata kwa muda zinarudia tena,nakumbuka niliota nachomwa sindano kwenye paja na nilipoamka nikajikuta Nina maumivu lile eneo!
Baadae niliamua kumuomba Mungu kwani nilijua nikiwa nimeokoka na nguvu za Mungu ziko Ndani yangu sitakiwi kuteswa na chochote kwenye ndoto au kawaida na WACHAWI WALA MAPEPO au waganga!
Baadae Ndio nilipopewa jibu na Roho Mtakatifu kuwa”MWANANGU WEWE NI NDOO ILIYOTOBOKA HAIWEZI KUKAA NA MAJI”
Japo ilikuwa lugha ya fumbo ila Roho Mtakatifu alinisaidia kuelewa alinionyesha maeneo yafuatayo ambayo inaweza kuwa na wewe ni unayapitia haya naamini Bwana atakuponya!

MOVIES!

Nilipokuwa sijaokoka nilikuwa napenda sana movies za SEASONS za kikorea na kimarekani, movies za kibongo, Hivyo baada ya kuokoka tabia hii niliiacha kwa muda ya kuangalia movies ila baadae nikarudi tena (Nikijisemea kuwa kuangalia movies sio dhambi mbona)!
Kumbe shetani ni mjanja sana, ndani ya zile movie kuna wakati wahusika wanashikana shikana,wanabusiana,mara wapo vitandani KUMBE NDIO NANYONYWA NGUVU ZA MUNGU NILIZOZIKESHEA KWA KUFUNGA NA KUOMBA!

MPIRA
Kabla sijaokoka nilipenda sana mpira,nilikuwa naenda kwenye mabanda kuangalia mpira hasa Arsenal ikicheza na Tanzania Simba ikicheza,hata iwe usiku naenda!
Nilipookoka nilijitahidi kujizuia ila baadae nilianza Tena kufuatilia, kumbe nikienda kule kutazama MPIRA unakuta watu wanabishana,wanatukanana nayasikia yote YANANITIA UNAJISI!
Nilikuwa niko radhi kutafuta hela ya kuangalia mpira hata itakuwa juu ila kanisani sina sadaka au natoa sadaka kidogo ukilinganisha na pesa nikiyoitumia kuangalia mechi za mpira!

MITANDAO YA KIJAMII
Nayo ilitumika kunirudisha nyuma na kuninyonya nguvu za Mungu nilizozihangaikia kwa kusoma vitabu na maombi na kufunga!
Nilianza kuangalia MEMES napoteza muda huko,vichekesho,naweza kutumia hata masaa mawili huko Lakini kuangalia video za mafundisho ya Neno la Mungu natumia nusu saa Hapa shetani aliniweza pia!
Status yangu ya whatsapp, Instagram na wakati mwingine Facebook yangu (Nilikuwa na akaunti mbili) nikuweka vichekesho utani ili watu wacheke tu basi,wala sikupenda kuitumia kufundisha Neno la Mungu na kuwajenga watu!

MARAFIKI WABAYA
Bado baadhi ya marafiki tuliendelea kuwasiliana na kuongea kwenye simu utani wa kijinga,maswala ya mpira tunataniana, wakati huyo rafiki hajaokoka simwambii habari za Yesu ila namwambia habari za Simba na Yanga na MANCHESTER!

Biblia inasema”MSIDANGANYIKE; MAZUNGUMZO MABAYA HUARIBU TABIA NJEMA”(1Wakoritho 15:33)

Kupitia mazungumzo ya marafiki, Memes, movies viliharibu tabia zangu njema za maombi, kufunga, kusoma Neno, kusamehe n.k

NDIO NIKIPOGUNDUA HAYO YOTE NI MATUNDU YALIYOTUMIKA KUNINYONYA NGUVU ZA MUNGU NDANI YANGU!

Ndio Maana hata Pepo haliniogopi tena kama Mwanzo!
Usiku nakabwa kama kawaida,nakaliwa kama kawaida kumbe wameondoa nguvu za Mungu Ndani yangu!
Nikajikuta nilikuwa na Hasira zikarudi tena,nikajikuta nakuwa mgumu kusamehe (Moyo wa jiwe umerudi)!

Namshukuru Mungu maana nilifanya marekebisho na kuzijua fikra za shetani, Hivyo nimeziba hiyo mianya (hayo matundu!

SHETANI AKISHINDWA KUKUZUIA USIMTAFUTE MUNGU NA NGUVU ZAKE BASI ATATAFUTA NJIA YA KUZIONDOA HIZO NGUVU NA USIPOKUWA MAKINI ATAZIONDOA TU!

Utaonekana unaendelea kuimba kwaya kwa sauti ya kuvutia,unahubiri madhabahu, unafanya kazi ya Mungu Lakini huna nguvu za Mungu Ndani yako (Powerless)

Si unaumkubuka Samson jinsi shetani alivyo tumia mbinu ya kuziondoa nguvu zake?(Soma WAAMUZI 6:4-21)
alitumia mapenzi tu na Delilah alimnyoa nywele!

ANGALIA NA WEWE USIJE KUWA NDOO YENYE MATOBO!
LEO MAKANISANI VIJANA WENGI NI NDOO ZENYE MATUNDU,WANAFUNDISHWA NENO KANISANI WAKITOKA KANISANI AKIWASHA SIMU TAYARI KATOBOLEWA ANACHOTAZAMA KWENYE MAGROUP AU INSTAGRAM NDIO KWISHA YAKE!

KAMA UNASOMA NENO, KUFUNGA, KUOMBA,KUUTAFUTA USO WA MUNGU,NI NJIA YA KUKUSANYA NGUVU ZA MUNGU NDANI YAKO LAKINI USIPOJUA KUZITUNZA HIZO NGUVU,KWA KUJINIDHAMISHA MBALI NA MARAFIKI WABAYA, KUPOTEA MUDA KWENYE GAMES,MIPIRA, SOCIAL MEDIA UTAKUWA NI SAWA NA NDOO INAYOKINGWA MAJI NA MAJI YANACHURUZIKIA NJE KUPITIA MATUNDU MENGI YALIYOTOBOLEWA NA SHETANI!

Kuna watu walijazwa Roho Mtakatifu walifunga na kuomba kwa gharama kubwa, wengine waliombewa wakajazwa,wakawa wanaomba kwa lugha mpya BAADA ya kujiingiza kwenye mambo HAYO,sasa hivi imebaki historia kuwa na yeye aliwahigi kujazwa ROHO MTAKATIFU ila haelewi imekuaje!
Kumbuka anaitwa ROHO MTAKATIFU maana yake ni MTAKATIFU,ukianza kuingiza mambo hayo yatakayokutia unajisi,basi anaondoka na nguvu zake! Unajikuta umebaki ikabodi!

HEBU ANGALIA MTUME PAULO ANAVYO ZUNGUMZIA NGUVU ZA MUNGU KATIKA HUDUMA YAKE NA NDIO MAANA ALIFANIKIWA SANA!

LAKINI LEO TUNAWATUMISHI HAWANA NGUVU WANAMANENO YA KUSHAWISHI,UNAKUTA MCHUNGAJI AU MTUMISHI WA MUNGU YUKO KIJIWENI KUTWA NZIMA ANABISHANIA MPIRA WA SIMBA NA YANGA!

LEO TUNAWATUMISHI WENYE HASIRA,UKICHEZA ANAWEZA KUKUPIGA KIBAO MADHABAHU BILA SABABU YA MSINGI UKIMFUATILIA NI MTAZAMAJI MZURI WA MOVIES ZA NGUMI,MIELEKA,HIVYO KUMPIGA MSHIRIKA NGUMI NI KAWAIDA KWAKE!

HANA NGUVU ROHO INABIDI ATUMIE ZA MWILI, HARAFU ANAKUPA ANDIKO LA KUHARARISHA ALICHOKIFANYA KWA KUSEMA,HATA YESU NAE ALICHAPA WATU VIBOKO ALIPOWAKUTA WAKIUZA HEKALUNI!

Inaweza kuwa tayari mtumishi huyu ameshatobulewa matundu, hakuna nguvu ndani yake Wala hekima ya Mungu!

Angalia Paulo anachosema:-

“Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu,bali kwa dalili za Roho na NGUVU, ili Imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu,bali katika NGUVU ZA MUNGU”(1Wakoritho 2:4-5)!

YESU ANARUDI UPESI, ANGALIA NI WAPI ULIKO ANGUKA (Unakovuja) utubu na kuanza upya(Ufunuo 2:4-5)
hakika utashinda, huduma yako itarudi tena, ushindi wako utarudi tena,utamseta shetani chini ya miguu yako.(WARUMI 16:20)

Pastor Emanuel Baltazary Moria
ARUSHA TANZANIA
04/02/2022

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »