Mwezi wa Tano

MWANAUME ULIYEOA
“UKIAMUA KUTENGA DAKIKA 30 TU KILA SIKU NA MKE WAKO ZA KUONGEA, KUCHEKA, KUTANIANA, KUMSIKILIZA, KUMKUMBATIA KWA UPENDO (HATA KAMA ILISHAKATA AU UMEMZOEA), KUMSIFIA KWA UREMBO NA UZURI WAKE (MAANA NDIYE ULIYENAYE, NDIYE MREMBO WAKO WA DUNIA HUYO, USHAMUWEKA NDANI)… KISHA MNAOMBA PAMOJA, MKIWA MMESHIKANA MIKONO, UNAMRUHUSU ATAMKE MANENO MBELE ZA MUNGU KWA AJILI YAKO, NA KISHA NAWE UNAMTAMKIA MANENO YA BARAKA MBELE ZA MUNGU HUKU UNAMTAZAMA… UKIFANYA HILI ZOEZI KWA MWEZI HUU WA TANO TU, NAKUHAKIKISHIA UTAPATA BONGE MOJA LA MKE, BONGE MOJA LA RAFIKI, BONGE MOJA LA MAPENZI YA KWELI, TOKA KWA MWANAMKE ULIYEKUWA UNAONEKANA KUMZOEA NA KUMCHOKA… USISAHAU KILA NG’OMBE ANAYEPEWA MAJANI MAZURI LAZIMA ATOE MAZIWA TU… KAZI KWAKO ULIYEOA”

UNAWEZA KUM-TAG MMEO, SHEMEJI YAKO, KAKA YAKO ALIYEOA NA MWANAUME YEYOTE MWENYE MJI!


 

“UKIAMUA KUWA NA DAKIKA 30 ZA UTULIVU, ILI UWAZE, UFIKIRI NA KUPANGILIA MAISHA YAKO, WALAU MARA 3 AU 4 KILA WIKI, NA MAAMUZI UTAKAYOFIKIA UYATEKELEZE BILA KUJIHURUMIA, HAKIKA MWEZI HUU MMOJA TU UNATOSHA KUGEUZA UELEKEO MBAYA NA WA KUSUASUA WA MAISHA YAKO! KILICHOBADILI MAISHA YA MWANA MPOTEVU TOKA KUWA MCHUNGA NGURUWE, ANAYETAMANI KULA MAGANDA WANAYOKULA HADI KURUDI KWENYE NAFASI YAKE YA UKUU NI KUPATA MUDA WA KUYATAFAKARI MAISHA YAKE, KUJIFANYIA TATHMINI, KUKUBALI MAKOSA YAKE, KUFIKIRIA MASULUHISHO, NA KUKUBALI KUYAISHI (Luka 15:11-32)… SIDHANI KAMA UNASHINDWA KUFANYA HILI AU HUNA MUDA… NI WEWE TU NA UPUUZI MWINGINE ULIOUPA MUDA WAKO… BADILI MFUMO WA MAISHA YAKO, ILI TUKUONE WEWE HALISI MWENYE THAMANI… ISHI KWA MAKUSUDI, ACHA KUISHI KWA BAHATI BAHATI”


“UKITENGA DAKIKA 30 AU SAA 1 KILA SIKU YA KUTAZAMA VIDEO 1 TU YA MAFUNDISHO YA WATUMISHI MBALIMBALI WA MUNGU KULE YOUTUBE, NA KUANDIKA ULIYOELEWA ILI UYAWEKE KWENYE MATENDO, NDANI YA MWEZI UKIWA SERIOUS NA UKAJITOA, UTAKUWA UMEMALIZA VIDEO 30 AMBAZO NINAJUA ZITABADILI AKILI NA UFAHAMU WAKO, ZITAKUFANYA SMART, ZITAGEUZA MTAZAMO WAKO KUHUSU VITU NA MAISHA, NA ZITABORESHA HALI YAKO YA KIROHO MNO! ILA BAHATI MBAYA SIWEZI KUKULAZIMISHA…”


“UKITENGA DAKIKA 30 AU SAA 1 KILA SIKU YA KUTAZAMA VIDEO 1 TU YA MAFUNDISHO YA WATUMISHI MBALIMBALI WA MUNGU KULE YOUTUBE, NA KUANDIKA ULIYOELEWA ILI UYAWEKE KWENYE MATENDO, NDANI YA MWEZI UKIWA SERIOUS NA UKAJITOA, UTAKUWA UMEMALIZA VIDEO 30 AMBAZO NINAJUA ZITABADILI AKILI NA UFAHAMU WAKO, ZITAKUFANYA SMART, ZITAGEUZA MTAZAMO WAKO KUHUSU VITU NA MAISHA, NA ZITABORESHA HALI YAKO YA KIROHO MNO! ILA BAHATI MBAYA SIWEZI KUKULAZIMISHA…”


“UKIAMUA KUTUBU DHAMBI YOYOTE ULIYOIZOELEA, NA KUOMBA NEEMA YA KUIACHA JUMLA, UTAKUWA MWEZI WAKO WA MABADILIKO YA ROHO YAKO NA KUFUFUA MAHUSIANO YALIYOKUFA AU YANAYOZOROTA KATI YAKO NA MUNGU”


 

NDOA

Haikuanzishwa Na WANADAMU Bali MUNGU Ndiye Aliyeanzisha TAASISI HII… Imeanzishwa Na MUNGU Ambaye Ni Roho, Uwe Na Uhakika Haiwezi Kuendeshwa Kwa Kutegemea AKILI, HEKIMA NA

Read More »

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »