MTU HAWI WA NAMNA FULANI SIKU AKIKALIA KITI CHA UTAWALA AU AKIKAA KWENYE NAFASI FULANI

MTU HAWI WA NAMNA FULANI SIKU AKIKALIA KITI CHA UTAWALA AU AKIKAA KWENYE NAFASI FULANI, HAPANA! ANAKUWA MTU WA AINA FULANI SIKU AKIFANIKIWA KUWA HIVYO NDANI YAKE…

  1. Akijiona tu ndani yake NDIVYO ALIVYO tayari, japo itachukua muda kumtoa yule wa ndani kuwa kitu halisi nje!
  2. Akijiona tu ndani yake sio atakuwa, tayari amekuwa na asipopoteza hiyo picha nje, LAZIMA ITAKUWA HIVYO NJE!

CHA KUFANYA SASA…

I. Jaza ndani yako taarifa nyingi na sahihi za UNAVYOTAKA KUWA

II. Hizi taarifa zikiwa halisi mno ndani yako, ZITAANZA KUKUPA NIDHAMU NA MFUMO WA MAISHA wa kukuandaa na kukulinda uwe unavyotakiwa kuwa!

III. Jenga UVUMILIVU wakati unapopitia mchakato wa kutoka wewe unayejiona ndani kuja wewe utakayeonwa na kila mtu! Wengi hukwama hapo, wengi hushindwa kwenye hatua hii… ili kuirithi ahadi yoyote, lazima kuwe na uvumilivu na imani (Waebrania 6:12)!

ANDIKO

Mithali 23:7
[7]Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo…
For as he thinketh in his heart, so is he…

Askofu Dickson Cornel Kabigumila
ABC GLOBAL DUNIANI

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »