MOJA WAPO YA SABABU ZILIZOFANYA NIKAZANIE KUWA BORA-01

“SIKUONA HESHIMA WANAYOPEWA WATU WA “JUMLA” NILIONA WANAOPEWA HESHIMA NI WALIOFANIKIWA KUFANYA VITU VYA PEKEE AU VITU VILEVILE KWA UPEKEE”

YAANI NILIGUNDUA, DUNIA HAISHANGILII KILA MTU, INASHANGILIA ALIYEFANYA AMBACHO HAKIJAWAHI KUFANYWA AU KILICHOWAHI KUFANYWA LAKINI KWA NAMNA TOFAUTI!

YAANI NILIONA “UKIWA MTU WA KAWAIDA” KAMA WENGINE, UTAPATA WANACHOPATA WENGINE NA HUATAKAA UWE “MTU KATI YA WATU” MILELE!

KWA MAAMUZI YANGU YA DHATI, NIKASEMA SITAKI KUWA KAMA WENGINE WOTE, NATAKA KUWA MTU WA TOFAUTI, MTU WA PEKEE, MTU AMBAYE ULIMWENGU HAUJAWAHI KUWA NAYE NA AMBAYE AKIONDOKA HATAKUWEPO WA KUZIBA NAFASI YANGU AU ITAHITAJI MUDA MREFU KUPATA ANAYEONEKANA KUFANYA KAMA MIMI!

HII ILIBADILISHA VIPAUMBELE VYANGU, NDOTO NILIZOKUWA NAZO, NA HATA PICHA YA MAISHA AMBAYO NILIKUWA NAYO… I JUST WANTED MORE OUT OF LIFE! INGAWA SIJAWA NINAVYOTAKA KUWA, LAKINI NAMSHUKURU MUNGU MTU YEYOTE MWENYE AKILI NJEMA ANAWEZA KUONA MIMI SI MTU WA KAWAIDA, NINA LADHA YANGU YA KIPEKEE!

Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila

21/05/2019