- USIIGIZE WALA USIWADANGANYE WATU KWAMBA UNA UWEZO MKUBWA WA KIFEDHA/ UMEBARIKIWA MALI NA VITU ILHALI UNAWAPIGA MIZINGA NA VIBOMU KUPITIA MBEGU NA SADAKA ZA AJABU AJABU AU KUCHUMA PESA ZA WATU WA MUNGU KWA UJANJA UJANJA!
Maandiko yanatuambia;
“LAKINI WALE WATAKAOKUWA NA MALI HUANGUKA KATIKA TANZI NA MAJARIBU, NA TAMAA NYINGI ZISIZO NA MAANA, ZENYE KUDHURU, ZIWATOSAZO WANADAMU KATIKA UHARIBIFU NA UPOTEVU”
(1TIMOTHEO 6:9). - Ukilisoma andiko hili utajifunza yafuatayo;
i) Kuna wahudumu wa INJILI ambao sababu hasa iliyowaingiza kwenye kinachoitwa HUDUMA NA UTUMISHI ni ili wapate pesa na mali
ii) Kuna walioingia kwenye HUDUMA NA UTUMISHI wakikusudia kabisa KUVUNA ROHO ZA WATU na kumzalia Mungu matunda lakini NJIANI WAKAVAMIWA NA HII KIU YA KUTAKA MALI NA VITU na wakaingia kwenye ukengeufu na upotevu na uharibifu!
iii) Kuna watumishi wa Mungu ambao walikuwa halisi kabisa na hawakuwa na mzaha na kazi ya Mungu, lakini WALIPOWATAZAMA WAHUBIRI MAARUFU WA AFRIKA MAGHARIBI NA MAREKANI wenye pesa na mali na vitu, wakaingia kwenye mtego wa wao pia kufanya kila wawezalo ili wapate mali na vitu, NA WAKAISHIA KUPOTEZA KITU KIKUBWA CHA MUNGU WALICHOKUWA NACHO! - Maandiko hayo juu yanatueleza siri kadhaa;
- i) Hakuna uwezekano mtumishi avamiwe na hii kiu ya kupata Mali na vitu kupitia injili ambaye HATAANGUKIA KWENYE MAJARIBU NA TANZI (MITEGO) YA SHETANI NA MAWAKALA WAKE!
Huduma nyingi zilizokuwa Moto mno wakati mlengo (focus) ilipokuwa KULETA ROHO NYINGI KWA YESU, walipobadilika na KUINGIZA SUALA LA MALI NA PESA KUPITIA MGONGO WA INJILI, kila kitu cha MUNGU kilinyamaza na ukabaki UJANJA UJANJA na kutengeneza SHUHUDA ZA UONGO na UTAPELI! - ii) Hata kama mhudumu wa INJILI alikuwa vizuri kiasi gani, akinaswa na mkumbo huu wa KUTAMANI MALI NA VITU, lazima ataishia pabaya, kwenye ULEVI, UZINZI, UTAPELI, KUFELI KWA NDOA YAKE NA HATA KUHARIBIKA KWA HUDUMA AU KUANZA UJANJA UJANJA MADHABAHUNI!
NAMNA AMBAVYO WATUMISHI WENGI WA MUNGU WANAVYOINGIA KWENYE MTEGO WA KUPENDA MALI NA VITU NA KUPOTEZA HUDUMA; - i) Kwa kudanganyika na mafanikio ya WAHUBIRI MAARUFU wa magharibi au ulaya, wanaojinadi ya kwamba wanao utajiri, mali na vitu kama magari, majumba, ndege, mabenki nakadhalika! Na hii inafanya huyu mtumishi “mdogo” abadilishe mtazamo toka kwenye UVUNAJI ROHO ZA WATU TOKA DHAMBINI kuja kwenye KUFANIKIWA AU KUTAJIRIKA KUPITIA KIPAWA AU HUDUMA YAKE!
- ii) Waimbaji wa INJILI wengi wamenaswa na mkumbo huu! Wengi walianza kufanya kazi ya huduma kama njia ya kumfanyia Mungu IBADA, na KUFIKISHA walichobeba kwa watu wa Mungu ili kuleta majibu na masuluhisho, lakini badala yake, WALIPOKUTANA NA WALE WAIMBAJI MAARUFU WATOZAO PESA, WENYE MAMENEJA, WENYE MLOLONGO MREFU WA MASHARTI YA KUHUDUMIA WATU WA MUNGU, wakawaonesha ya kwamba WATAKUFA MASIKINI WAKIENDELEA KUTOA BURE KILE WALICHOBEBA, matokeo yake na wao wakawa na MANAGENENT, WASIMAMIZI WA MIALIKO NA KAZI, ambao wanalenga kunufaika kupitia KIPAWA CHA MUIMBAJI, ambao WENGI HATA KUOKOKA HAWAJAOKOKA ni wachumia tumbo na WAZEE WA FURSA!
KWENYE MADHABAHU (WACHUNGAJI, MITUME NA MANABII); - i) Wameasisi vitu vinaitwa VIFAA VYA KIROHO (spiritual materials) kama VITAMBAA, CHUMVI, MAJI, SABUNI, MAFUTA, MIFAGIO, KALENDA, PICHA ZA WATUMISHI, BANGILI NA MATAKATAKA MENGINE ambayo wao WANAYAITA YA UPAKO! Ambayo HUUZWA KWA BEI ZA JUU, NA WAKIDAI LENGO NI ILI ZISUKUME HUDUMA lakini ukweli ni kwamba HAZIFANYI HAYO, bali WANAKULA WAO, NI VITEGA UCHUMI VYAO WENYEWE!
- ii) Kumuona mtumishi kwa KUTOA SADAKA MAALUM, AU KIASI FULANI KILICHOPANGWA ILI KUMUONA MTUMISHI HUSIKA!
Wengine wanatoza 50,000 Wengine 70,000, wengine 200,000, wengine hadi 500,000/=
iii) Kuandaa chakula maalum cha kinabii au safari na nabii/ mtumishi!
Hapa hawa watumishi njaa wanaandaa vyakula (prophetic dinner) ambapo watu wanaingia kwa malipo maalum na kwa ngazi tofauti tofauti mfano dollar 50, dollar 100, VIP dollar 200, kuwa meza moja na nabii dollar 500!
Au anaandaa hata safari labda ya kwenda mbugani au mlima wa maombi au hata Israeli, ambapo wanaokwenda naye ni walio na SADAKA MAALUM au waliotoa pesa fulani iliyowekwa kama kigezo! Ambapo asilimia kubwa wengi HUZIDISHA KIASI KWA AJILI YAO, NI BIASHARA!- iv) KUPANDA MBEGU kwa mtumishi!
Wako watumishi wa Mungu ambao huwezi kumuona kama huna PESA MKONONI inayoitwa MBEGU! Hawa watu wanasema wako busy, ili wakusikilize, wakupe muda wao lazima UWAFURAHISHE MIOYO YAO kwa kuwapa MBEGU MAALUM, yaani pesa walau DAU FULANI LA KUELEWEKA!
v) Kuanzisha machangizo kwa ajili ya ujenzi wa kanisa, au ununuzi wa kiwanja, au ununuzi wa magari ya huduma, au chochote kwa mgango wa huduma, lakini HILO JAMBO LINAKUFA KIMYAKIMYA miaka inapita na halitafanyiwa kazi kabisa! Na vile WASHIRIKA ni watiifu (mazombie) hawawezi kuuliza au kufikiria nini kinaendelea, tayari mhusika ameshawapiga!
Wengine waliahidi wanaanzisha miradi ya kununua mashamba na kulima, lakini hadi leo imeishia hewani! Mwingine aliwaambia watu wake waweke hela benki ya kanisa lao, hadi leo hiyo pesa hawajawahi kuipata zaidi ya miaka 7 sasa!
MTUMISHI WA MADHABAHU AKIINGIWA NA ROHO YA KUPENDA PESA, ANAWAZA KUJINUFAISHA NA KUJITAJIRISHA, ANAPOTEZA UADILIFU, UAMINIFU NA UWAJIBIKAJI! ANABAKI NA UZOEFU NA MANENO MANENO, LAKINI MUNGU ALISHAMUACHA MUDA MREFU!
vi) Makusanyo ya zaka yasiyoeleweka!
Kuna mahali ambapo WATU HATA WAKIPOTEZA KAZI AU VYANZO VYAO VYA MAPATO WANAAMBIWA LAZIMA WAENDELEE KUTOA ZAKA, NA KAMA HAWANA CHA KUTOA LINAKUWA DENI…. HUU NI UHUNI, SI NENO LA MUNGU!
Kwa msingi wa namna hii, WAKRISTO WENGI WAMEACHA WOKOVU, WAMERUDI KWENYE DINI AU KUKAA TU NYUMBANI KISA TU ANA DENI LA ZAKA KANISANI, NA WAKIENDA WANAAMBIWA WAMEACHA IMANI, AU NI WEZI ILHALI MHUSIKA HANA TENA MAPATO TENA, UCHUMI UMEKWAMA!
HII SI INJILI, HUU SI UPENDO WA MUNGU, HII SI KWELI ALIYOLETA YESU, HUU NI UHUNI!
MCHEZO ULIOANZA KUOTA MIZIZI KANISANI;
i) WAHUBIRI kusema ni matajiri, wanamiliki mahoteli, ndege, migodi, biashara kubwa kubwa lakini cha ajabu wanaminya na kupiga hela za masikini kwa UTAPELI!
ii) WAHUBIRI kusema ni matajiri na huku wanakaba washirika wawalipie kodi, ada za watoto, wengine hadi suti za kuvaa ibadani na upuuzi mwingine kama huo!
Kama umebarikiwa, Una pesa na uchumi mzuri, ACHA KUWA MZIGO NA TANZI KWA WATOTO WA MUNGU!
Tumalize kwa andiko hili;
“MAANA SHINA MOJA LA MABAYA YA KILA NAMNA (YOTE) NI KUPENDA FEDHA, AMBAYO WENGINE HALI WAKIITAMANI HIYO WAMEFARAKANA NA IMANI (WAMEIACHA IMANI), NA KUJICHOMA KWA MAUMIVU MENGI”
(1TIMOTHEO 6:10).
WAHUBIRI WENZANGU,
WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI,
TUSIJARIBU KUPUUZA UJUMBE HUU,
GHARAMA YA KURUDI KWENYE MSTARI NI KUBWA MNO KULIKO RAHA NA MAPATO YA UDHALIMU!
JE UNAO USHUHUDA KUHUSU HAYA NILIYOANDIKA?
JE UMEWAHI KUWA CHINI YA MTUMISHI MJANJA MJANJA KAMA ULIVYOONA KWENYE SOMO HILI?
TUANDIKIE UZOEFU WAKO BILA KUTAJA MAJINA YAKE….
Pastor Dickson Cornel Kabigumila,
Assembly Of Believers Church (ABC GLOBAL),
28/10/2021
Kujifunza kupitia WhatsApp Status: 0655 466 675
MAWASILIANO YANGU KUJIFUNZA ZAIDI KWANGU, BONYEZA LINK HAPA CHINI;
https://linktr.ee/pastorkabigumila
HEKIMA ZA NDOA 3
“Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko