MFUNGO WA WA SIKU 10WA MWISHO WA MWEZI, [SIKU YA KUMI]

 

MAMBO YANAYOWEZA KUKUFANYA USITEMBEE KATIKA NEEMA

(THINGS THAT CAN HINDER YOUR GRACE WALK).

Lengo la somo hili ni kukuwezesha na kukufunulia baadhi ya mambo unayopaswa kuyaepuka kama kweli una nia ya dhati ya kutembea katika neema na kupata matokeo makubwa ya neema ya Mungu maishani mwako!

Yafuatayo ni mambo yanayozuia neema isiweze kukufanyia kazi na kutoa matokeo yanayostahili;

1. Kuidharau kazi ya msalaba (To take the finished work for granted).

Watu wengi wakisikia kuidharau kazi ya msalaba wanadhani ni kuitukana au kuiona haifai, HAPANA!

Kuidharau kazi ya msalaba ni pamoja na kudhani kwamba, “kuna unachoweza kuongeza” na kumfanya Mungu akupende zaidi… Hili ni kosa kubwa mno!

Msalaba ni kiwango cha juu cha Mungu kudhihirisha upendo wake katika mwili (Yohana 3:16).

Ni aidha unaikubali na kuipokea kazi ya msalaba “iliyofanywa na Yesu kwa ajili yako” au unaikosa na kupoteza nguvu yake kwa kujaribu kumpendeza Mungu kwa matendo yako ya kibinadamu (Waefeso 2:8)!

Yesu ni mwanzilishi wa kazi ya msalaba, na ndiye anayetukamilisha, jeuri na kiburi chetu kama wana wa Mungu ni KILE ALICHOFANYA YESU na si kile tunachojaribu kufanya kwa ajili yake!

Alitupenda mwanzo (Yohana 15:16), alituchagua tukingali wenye dhambi na wasiofaa (Waefeso 2:1-8), akatufanya uzao mteule na ukuhani wa kifalme, taifa takatifu na watu wa milki ya Mungu (1Petro 2:9).

•Yeye ndiye aliyetuokoa kutoka katika Ufalme wa giza na kutuhamisha na kutuingiza kwenye Ufalme wa Mwana wa Pendo lake (Wakolosai 1:13).

•Yeye alikubali kuwa fidia yangu na yako… Alifanyika dhambi ili mimi na wewe tupate kuwa haki ya Mungu (2Wakorintho 5:21).

Kuomba, kufunga, kusoma Neno, kutoa sadaka, kukesha, HAVIWEZI KUTUFANYA WEMA ZAIDI… WEMA WETU UMEFUNGWA KWENYE KAZI TIMILIFU YA YESU MSALABANI!

“Tunaomba, tunafunga, tunakesha, tunatoa sadaka, tunakaa ndani ya Neno nakadhalika KAMA MATOKEO YA KAZI YA MSALABA NA SI KAMA NJIA YA KUMSHAWISHI MUNGU!”

Ukielewa haya mambo vizuri (Roho Mtakatifu akusaidie) itakusaidia USIWE MKRISTO WA DINI/ MLOKOLE WA DINI bali Mwana wa Mungu anayeufurahia msalaba na neema ya Mungu!

“Na katika utimilifu wake (kazi yake iliyokamilika) SISI SOTE TUMEPOKEA NEEMA JUU YA NEEMA….”
(Yohana 1:17).

Kukubali kuwa ALICHOFANYA YESU NDICHO KILICHOTUSTAHILISHA NA KUKUBALI KUWA YOTE MENGINE NI KWA SABABU YA HICHO, huko ndiko kunaitwa KULIKUBALI NA KULIHESHIMU NENO LA MSALABA!

“Kwa maana NENO LA MSALABA kwao wanaopotea ni upuuzi, BALI KWETU TUNAOOKOLEWA NI NGUVU YA MUNGU…”
(1Wakorintho 1:18).

Zingatia haya;

i) Bila kazi ya msalaba hakuna nafasi na haki yetu mbele za Mungu (2Wakorintho 5:21).

ii) Kukesha, kuomba, kufunga, utoaji, ibada, kusifu, na mengine mengi tunayofanya, YAMEPATA MAANA BAADA YA KAZI YA MSALABA, bila msalaba yanakuwa utaratibu wa kidini wa mwanadamu kumtafuta Mungu kama walivyokuwa wakiyafanya Mafarisayo (Washika dini), lakini HAYAWABADILISHI!

iii) Yesu ni mwanzilishi wa imani yetu (msalabani) na mtimizaji wa imani yetu (kupitia Roho wake mtakatifu tuliyepewa), lazima UIKUBALI NA KUIHESHIMU NGUVU ILIYOKUINGIZA KWENYE UFALME ili nguvu ya kukustawisha kwenye Ufalme itende kazi (Waebrania 12:2)!

Nukuu;

“Msalaba wa Yesu ndio chanzo cha Nguvu ya Mkristo, ukiuondoa umeondoa sadaka yake iliyotufanya kuwa wana wa Mungu- Pasipo msalaba (neema na pendo la Mungu) hatuna ushirika na Mungu”
(Pst. D.C.Kabigumila)

2. Maisha ya dhambi (Sinful living).

•Dhambi inakula utukufu wa Mungu (Warumi 3:23).

•Dhambi inaleta mauti (Warumi 6:23).

•Dhambi inatufarakanisha na Mungu (Isaya 59:1-2).

•Dhambi inazuia neema ya Mungu kufanya kazi (Warumi 6:1-11).

•Ni wajibu wako na wangu kuwa watakatifu kama Baba yetu alivyo mtakatifu (1Petro 1:15-16).

Nukuu;

“Kama unapenda kutembea katika neema ya Mungu usicheze na dhambi!”

3. Kutolipa nafasi Neno la neema (Giving no room to His Word of grace).

•Huwezi kutenganisha neema ya Mungu na Kweli ya Mungu (Neno la Mungu)!

•Neema na Kweli vyote viwili vimekuja toka kwenye Neno lililochipuka mwili (Yohana 1:1-5,14,16).

•Neno la Mungu ni Neno la neema yake (Matendo 20:32).

•Huwezi kuwa mtu wa Neema endapo hautadumu katika Neno la Mungu!

•Watu wote wenye neema kubwa ya Mungu ni watu wenye Ufunuo katika Kweli za Neno na wamekubali kuwa WATENDAJI WA NENO NA SI WASIKIAJI WASAHAULIFU (Yakobo 1:22-25)!

•Ukiwa mvivu wa kukaa katika Neno, unajimaliza, unaiua Neema ya Mungu maishani mwako maana inajengwa kwenye msingi wa Neno la Mungu ulilonalo (Yohana 15:4, 7, Wakolosai 3:16)!

Litafute Neno la neema kwenye:
– Biblia yako,
-Vitabu vya watumishi wa kweli wa Mungu,
-DVD, CD za watumishi wa Mungu
-Mikutano,
-Semina na makongamano
-Video za mafundisho You Tube

Nukuu:

“Ukiwa mchovu katika Neno la Mungu hakuna ubishi utakuwa mchovu kwenye neema ya Mungu!”
(Pst. D.C.Kabigumila)

4. Kiburi na dharau (Pride and arrogance).

Hivi vitu ni silaha ya uangamivu kutoka katika malango ya kuzimu.

•Shetani anajua Wakristo wengi hawataiba, kuzini, wala kutoa mimba… Ila anajua wana kiburi na dharau, na tayari kupitia mlango huo anawazuia kutembea kwenye neema!

“Kwa maana Mungu HUWAPINGA WENYE KIBURI NA HUWAPA NEEMA WANYENYEKEVU…”
(Yakobo 4:5-6, 1Petro 5:5).

•Unyenyekevu utakufanya upande juu sana, bali kiburi kitakuchimbia kaburi (Wafilipi 2:5-11).

Mara nyingi kiburi ni matokeo ya;
-Maarifa uliyonayo,
-Hadhi uliyonayo,
-Kibali ulichonacho,
-Uwezo wa kiuchumi,
-Uwezo wa kiakili au kielimu,
-Nafasi ya uongozi (cheo),
-Au kipawa kikubwa kinachokupa umaarufu!

Kumbuka, “…kufanikiwa kwa mpumbavu kutamwangamiza” (Mithali 1:32).

Nukuu:

“Epuka kiburi, jivike vazi la unyenyekevu, na neema ya Mungu itakufikisha ambako hujawahi kuota kufika”
(Pst. D.C.Kabigumila)

5. Maisha yasiyo na maombi (prayerlessness).

•Kila mtu mwenye neema kubwa ni mtu wa maombi.

•Musa alikuwa mtu wa neema kubwa kiasi cha USO WA MUNGU kuwa naye (Kutoka 33:12-18), lakini alikuwa Mwombaji asiyekuwa wa kawaida!

•Yesu ni Bwana wa neema (Yohana 1:16-17), lakini pia alikuwa mwombaji mno (Waebrania 5:7).

•Paulo alikuwa mtu mwenye neema iliyopitiliza (1Wakorintho 15:10), lakini siri yake kubwa ni maombi (Waefeso 6:10-18).

•Madhabahu ya maombi huzaa neema na rehema za Mungu (Waebrania 4:16).

Nukuu:

“Usipokuwa mwombaji hakuna unayemkomoa, unajimaliza mwenyewe, unajikosesha neema na rehema za kukusaidia kwenye kila eneo la maisha yako”
(Pst. D.C.Kabigumila)

6. Kukosa Maarifa na Ujuzi wa kutosha kuhusu Mungu na Kristo Yesu.

•Kadri unavyoongezeka katika Kumjua Mungu na Kristo Yesu, unaongezeka na kukua katika neema na amani (2Petro 1:2)!

•Uzima wa milele uliobeba ndani yako hauwezi kufanya maajabu, miujiza na mambo makubwa zaidi ya maarifa yako katika Mungu na Kristo Yesu aliyemtuma (Yohana 17:3).

Nukuu:

“Huwezi kuwa na neema zaidi ya kiwango cha maarifa ya Mungu ulichonacho.”
(Pst. D.C.Kabigumila)

MAOMBI

-Muombe Mungu akusaidie kuvuka kila kizuizi cha neema kilichokufunga na kukuzuia!

-Muombe Mungu akumwagie Roho ya maombi na neema (Zekaria 12:10).

-Muombe Mungu akusaidie usiipungukie neema yake (Waebrania 12:15).

-Muombe Roho Mtakatifu ajifunue kwako kama Roho wa neema, ili ukue katika neema yake (Waebrania 10:29).

-Muombe Mungu akupe kuithamini na kuiheshimu kazi ya msalaba (1Wakorintho 1:18).

Hongera sana kwa kufunga siku zote 10 za mwisho wa mwezi wa tatu, Maisha yako hayatabaki yalivyokuwa!

NB: TUMA SADAKA YAKO YA KUMSHUKURU MUNGU, INAYOAMBATANA NA MAOMBI ULIYOOMBA KWA SIKU ZOTE KUMI! MAOMBI NA SADAKA HUENDA PAMOJA

(Matendo 10:1-3)!

Tuma sadaka yako kuja:
M-PESA: 0753 466 675
TIGOPESA: 0655 466 675
UKITUMA SADAKA NIJULISHE INBOX TAFADHALI.

Pst. Dickson Cornel Kabigumila,
Mchungaji kiongozi,
Assembly Of Believers Church (ABC),
31/03/2019.

USIOE KWA SABABU :2

  “Wenzako wote uliokua nao au kusoma nao wanaoa. Ndoa si ALISEREMA ARIJA AU MWENGE TUNAUKIMBIZA. Ndoa ni taasisi ambayo Mungu amemuwekea kila mmoja wetu

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »