MFUNGO WA WA SIKU 10 WA MWISHO WA MWEZI [SIKU YA TISA]

NEEMA YA KUISHINDA DHAMBI NA KUISHI MAISHA MATAKATIFU

(THE SPECIAL GRACE TO OVERCOME SIN AND LIVE HOLY LIFE)!

Kama tulivyotangulia kuona katika masomo ya mfululizo huu yaliyopita, ya kuwa Mungu anazo aina mbali mbali za neema ambazo anaweza kuwapa watu wake (1Petro 4:10)!

Na mojawapo kati ya neema anayotoa Mungu kwa mwamini ni *neema ya Mungu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu.

Imeandikwa, *”Maana NEEMA YA MUNGU iwaokoayo watu wote imefunuliwa; NAYO YATUFUNDISHA KUUKATAA UBAYA NA TAMAA ZA KIDUNIA; TUPATE KUISHI KWA KIASI, NA HAKI, NA UTAUWA KATIKA ULIMWENGU WA SASA…”*

(Tito 2:11-12).

Ukilichambua andiko hili utajifunza mambo kadhaa;

i) Neema ya Mungu pekee ndiyo iliyobeba wokovu wa mtu katika maeneo yote ya maisha, na eneo mojawapo ambalo Yesu alikuja kumuokoa mwanadamu ni eneo la dhambi:

*”…jina lake utamwita Yesu kwa maana NDIYE ATAKAYEWAOKOA WATU WAKE NA DHAMBI ZAO…”*

(Mathayo 1:21).

Hivyo neema ya Mungu aliyoileta Yesu na kutufunulia sisi (Yohana 1:14,16-17, Tito 2:11-12), ina uwezo ndani yake wa *KUKOMESHA KIU NA NGUVU YA DHAMBI MAISHANI MWA KILA MTU ANAYEIPOKEA!*

Paulo alieleza ukweli huu pale alipotuthibitishia nini kilichotokea msalabani;

*”Yeye asiyeijua dhambi (Yesu), ALIFANYIKA DHAMBI KWA AJILI YETU ili SISI TUPATE KUWA HAKI YA MUNGU…”*

Mleta neema Yesu Kristo, alikubali kukaa mahali petu pa dhambi ili sisi tuliomwamini na kumpokea tuishi na kutembea katika NEEMA YAKE YA UTAKATIFU MBALI NA DHAMBI!

Mtume Petro naye alisema juu ya hili namna hii;

*”Yeye mwenyewe (Yesu) ALIZICHUKUA DHAMBI ZETU JUU YA MTI (MSALABA), ili TUWE WAFU KWA HABARI YA DHAMBI NA HAI KWA AJILI YA MAMBO YA HAKI…”*

(1Petro 2:24).

*Kwa maneno haya, ni ukweli kwamba MTU ALIYEOKOKA ANAPASWA AWE MFU KWA HABARI YA MAMBO YA DHAMBI… Anapaswa apoteze kiu na shauku ya kutenda dhambi, na awe na kiu na shauku ya kutembea katika utakatifu na haki!*

Na hilo lilikamilishwa na YESU msalabani pale ALIPOZICHUKUA DHAMBI ZETU MWILINI MWAKE JUU YA MSALABA (MTI), halelluyaa!

Dhambi imeharibiwa na nguvu ya neema ya Mungu iliyoachiliwa msalabani.

Ndio maana kwa ujasiri wote Petro anatuagiza akisema, *”Basi iweni WATAKATIFU KAMA BABA YENU WA MBINGUNI ALIVYO MTAKATIFU…Kwa maana imeandikwa, nanyi mtakuwa watakatifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mtakatifu…”*

(1Petro 1:15-16).

Petro kama mtume kiongozi aliyeachiwa kanisa na Yesu, asingetuambia kufanya kitu ambacho HAKUNA NEEMA YA KUTUSAIDIA KUKIISHI.

Mungu anapokupa agizo, anakupa nguvu ya kulitimiza (Zaburi 60:12, Wafilipi 4:13).

Tumepewa Roho Mtakatifu ambaye ni *ROHO WA NEEMA (Waebrania 10:29)*, na ambaye anafanya kazi ya *KUTUFUNDISHA KUUKATAA UBAYA NA TAMAA ZA KIDUNIA ILI TUPATE KUISHI MAISHA YA HAKI, KIASI NA UTAUWA KATIKA DUNIA HII YA SASA AMBAYO WENGINE DHAMBI KWAO IMEKUWA MFUMO WA KAWAIDA WA MAISHA* (Tito 2:11-12).

Nisikilize Mwana wa Mungu, hauwezi kuishinda dhambi kwa nguvu na akili yako, unahitaji *NEEMA YA MUNGU*, ambayo tayari Yesu ameshailipia msalabani!

Ni mapenzi ya Mungu kwamba *”Dhambi isitawale katika mwili wako kwa maana hauko chini ya sheria bali NEEMA YAKE…”* (Warumi 6:14).

Kuna neema ya Mungu mpendwa wangu ambayo inakufanya uthibitike katika utakatifu, na kukupa nguvu ya kujilinda na dhambi na hivyo kukufanya USITENDE DHAMBI TENA, *”Kila aliyezaliwa na Mungu (aliyeokoka) HATENDI DHAMBI, BALI HUJILINDA…”* (1Yohana 5:18)!

*Neema inatufundisha mioyoni mwetu namna ya kuiepuka dhambi na namna ya kuishi maisha masafi, ya haki na utauwa na kiasi tena huku huku duniani kwenye ulimwengu huu ULIOJAA DHAMBI NA UOVU WA NAMNA ZOTE!*

Pokea neema hii maalum ya kuishinda dhambi katika jina la Yesu!

Pokea neema ya kujilinda mbali na uovu katika jina la Yesu!

Pokea neema ya kuwa hai katika haki na kuwa mfu kwa habari ya dhambi!

Ni maombi yangu kwa Bwana Yesu, unaposoma ujumbe huu, Kila mzigo uliokuwa unakulemea na kila dhambi iliyokuwa inakuzinga upesi, viharibiwe katika jina bora la Yesu Kristo!

*MAMBO YANAYOFANYA NEEMA YA UTAKATIFU IFANYE KAZI;*

1. Kubali kuwa neema iliyokuokoa ndiyo hiyohiyo inayoweza kukuwezesha KUKATAA UBAYA WA KILA NAMNA NA TAMAA ZA KIDUNIA ILI UPATE KUISHI MAISHA YA HAKI, UTAUWA (UTAKATIFU) NA KIASI KATIKA DUNIA HII YA SASA YA DHAMBI (Tito 2:11-12).

2. Kubali kuwa YESU ALICHUKUA DHAMBI ZETU MWILINI MWAKE ili sisi TUWE WAFU KWA HABARI YA DHAMBI NA HAI KWA MAMBO YA HAKI (1Petro 2:24).

3. Kubali ukweli kuwa YESU ALIKUJA DUNIANI KWA KUSUDI LA KUMUOKOA MWANADAMU TOKA NGUVU NA UTUMWA WA DHAMBI (Mathayo 1:21).

4. Kubali kuwa INAWEZEKANA KUWA MTAKATIFU HAPA DUNIANI ambako DHAMBI NA UOVU VINATAWALA WENGINE (Zaburi 16:3, Tito 2:11-12).

5. Kubali kuwa ni WAJIBU WAKO KUWA MTAKATIFU KAMA BABA YAKO WA MBINGUNI ALIVYO MTAKATIFU, na usijaribu kuishi tofauti na wajibu wako huu ndani ya Kristo (1Petro 1:15-16).

6. Amini na kubali ukweli kuwa YESU ALICHUKUA DHAMBI ZAKO NA KUKUPA UTAKATIFU WAKE (2Wakorintho 5:21).

7. Kubali ukweli kuwa UNAO UZAO WA MUNGU (ASILI YA MUNGU) NDANI YAKO inayokufanya USITENDE DHAMBI BALI UJILINDE DHIDI YA DHAMBI (1Yohana 5:18).

8. Kubali ukweli kuwa HAUTAWALIWI NA NGUVU YA DHAMBI TENA ukiwa ndani ya Kristo, Kupitia kazi ya msalaba UMESHAIFIA DHAMBI NA HAUISHI DHAMBINI TENA KAMA WASIO NDANI YA YESU (Warumi 6:1-14).

MAOMBI

ASUBUHI

1. Mshukuru Mungu kwa kukufanya mtakatifu upendwaye ndani ya Kristo (Wafilipi 1:1, Waefeso 1:1, Warumi 1:7).

2. Mshukuru Mungu kwa kukuokoa na kukupa neema yake ikufundishayo kuukataa ubaya na tamaa za kidunia ili upate kuishi maisha matakatifu katika dunia hii ya sasa (Tito 2:11-12).

MCHANA

1. Muombe Roho MTAKATIFU ambaye ni ROHO WA NEEMA ayaongoze maisha yako kila siku ili usizitimize kamwe tamaa za mwili (Waebrania 10:29, Warumi 8:6-14).

4. Muombe Mungu akusaidie USIIPUNGUKIE NEEMA YAKE aliyokupa, shina la uchungu na dhambi lisije likachipuka maishani mwako (Waebrania 12:15).

JIONI

1. Muombe Mungu akuwezeshe kudumu kuwa miongoni mwa WATAKATIFU WALIOMO DUNIANI WALIO BORA ANAOPENDEZWA NAO (Zaburi 16:3).

2. Muombe BWANA YESU AKULINDE USIJIKWAE NA AKUSIMAMISHE MBELE ZA MUNGU SIKU YA MWISHO BILA WAA WALA HILA (Yuda 1:24).

NB: Andaa sadaka yako maalum ya shukurani kwa ajili ya mfungo huu, ambayo UTAITUMA KESHO SIKU YA 10 YA KUHITIMISHA! Mungu akubariki na kukuwezesha.

Mungu akubariki, wewe ni jibu na suluhu ya wengi katika kizazi chako!

Tukutane kesho siku ya 10 tuhitimishe wote!

MAALUM: WALE TULIO DAR ES SALAAM TUKUTANE LEO JUMAMOSI, SAA 1:30 JIONI KWA AJILI YA KUMALIZIA SIKU YA LEO YA TISA PAMOJA KWA MAOMBI.

Pst. Dickson Cornel Kabigumila,

Mchungaji kiongozi,

Assembly Of Believers Church (ABC),

30/03/2019.

Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »