MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12 -MAY [SIKU YA 2]

AKILI BORA

(EXCELLENT UNDERSTANDING)!

“Nimesikia habari zako, kwamba roho ya miungu imo ndani yako, na kwamba nuru na ufahamu NA AKILI BORA ZIMEONEKANA KWAKO”

(Danieli 5:14).

Unajua kuna akili na akili kwenye maisha haya.

Hata anayekuwa wa mwisho darasani ana akili, ndiyo maana hajakosea na kufanya mtihani wa darasa tofauti na lake.

Kuna akili za kuzaliwa, akili za darasani, akili za maisha (uzoefu) na AKILI BORA (AKILI ZA KIUNGU)!

Akili hizi za Kiungu, ndizo AKILI BORA AMBAZO HATA WAFALME HAWANA.

Hizi ndizo akili ambazo zinaweza kutatua changamoto ambazo ELIMU NA UJUZI WA DARASANI umefeli kutatua!

Akili hizi ndizo alizokuwa nazo Yusufu kule Misri, ZILIZOWEZA KUTUNZA CHAKULA MIAKA 14 na kisiharibike!

AKili hizi ndizo zilizomfanya AKAWA BOSS nyumbani kwa Potifa ingawa alikuja akiwa mtumwa tu (Mwanzo 39:1-7).

Akili hizi ndizo zilizompa kuwa kiongozi wa wafungwa wote (nyampara) tena nchi ya ugenini (Mwanzo 39:21-23).

Akili hizi ndizo zilizomuelekeza kwa watu wenye ndoto zenye manufaa kwa maisha yake binafsi na future ya dunia yake!

Akili hizi ndizo zilizomfanya atoke gerezani hadi Ikulu ya Misri kama Waziri mkuu (Mwanzo 41:37-40).

Akili hii bora ndani ya Yusufu, Ilimfanya awe na masuluhisho ambayo waganga, wachawi, washirikina, hawana (Mwanzo 41:8-40).

HII NDIYO AKILI BORA AMBAYO NAIZUNGUMZIA NDUGU YANGU… AKILI AMBAYO MUNGU ANATAKA KUKUPATIA LEO!

Danieli pia alikuwa na AKILI HII BORA.

Akili hii ilimfanya kuwa mara kumi zaidi ya washindani wake (Danieli 1:17-20).

Akili hii bora ilimfanya awe bora kuliko wachawi, waganga, wasoma nyota, na washirikina wote (Danieli 1:20, Danieli 5:11-12).

Kila ambalo lilishindikana kwa wachawi, waganga, wasoma nyota, washirikina, lilipata suluhu kwa Danieli (Danieli 4:4-27).

Akili hii bora, ilimfanya kuwa mtu mkuu, Waziri mkuu wa Babeli kwa vipindi vya Wafalme watatu tofauti; Wakati wa Nekabuneza, Beltishaza na Dario.

Akili hii bora;

1. Inatoka kwa Roho Mtakatifu pekee (Mwanzo 41:37-40, Danieli 5:10-14).

2. Inakufanya uishi level za juu mno kuliko wachawi, waganga, wasoma nyota na watu wa giza (Daniel 1:17-21, Danieli 5:10-14).

3. Inakufanya utafutwe kokote uliko hata kama ungekuwa utumwani au gerezani!

Mwanzo 41:9-14.

4. Akili hii inakufanya uwe na masuluhisho yasiyowezekana kibinadamu.

Yusufu alikuja na suluhu ya kutunza vyakula miaka 7 bila friji, jokofu wala friza!

Danieli alijua mambo ya miaka zaidi ya 7 yatakayompata Nebukadreza!

*UNUSUAL SOLUTIONS* TO HUMANITY.

5. Inamfanya Mungu wako aheshimiwe mbele ya miungu mingine.

Mwanzo 41:37-40.

6. Inakutengenezea nafasi za uongozi na utawala ambazo hazikuwepo.

•Yusufu aliitwa Ikulu na kupewa nafasi ya uongozi ambayo haikuwepo Misri.

•Danieli pia alipata nafasi ya uongozi ambayo hakugombea, wala hakuiomba, kwa sababu tu ya akili bora!

• Daudi kwa kutumia akili bora, alipewa nafasi ya uongozi ambayo wapinzani wake walikubali bila kupinga kuwa anawazidi na anastahili (1Samweli 18:5).

Katika siku za mwisho tunazoishi, ukiwa na akili ya darasani, akili ya kuzaliwa au ya maisha peke yake, hutafika popote!

Tumepewa Roho Mtakatifu ili atutofautishe na watu wasio na Yesu katika siku hizi za mwisho.

Nataka usisahau jambo hili, Mungu yuko tayari KUKUPA AKILI YAKE BORA KATIKA MAMBO YAKO YOTE (2Timotheo 2:7)!

Nataka utafakari kila andiko kwenye ujumbe huu, na UKOMAE KWENYE MAOMBI, uhakikishe moyoni mwako ya kuwa UMEIPATA AKILI BORA!!

MAOMBI

1. Muombe Mungu akupe akili nyingi sana kama alivyowahi kumpatia Suleimani (1Wafalme 4:29).

2. Muombe Mungu akupe AKILI KATIKA MAMBO YOTE (2Timotheo 2:7).

3. Muombe Roho Mtakatifu akupe akili na hekima itakayokufanya uwe na masuluhisho yasiyo ya KAWAIDA (Mwanzo 41:37-45).

4. Muombe Mungu akupe akili bora itakayokufanya vitu unavyofanya vikupe promotion (kuinuliwa) na kila mtu akubali ya kuwa unastahili (1Samweli 18:5)

Tukutane kesho siku ya tatu,

Umebarikiwa mno,

Umebeba majibu ya mamilioni ya watu sasa na vizazi vingi vijavyo!

Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila,

Mchungaji Mwanzilishi,

ABC KAHAMA.

ENDELEA KUFUATILIA MAFUNDISHO ZAIDI KUPITIA:

www.yesunibwana.co.tz

NB: ENDELEA KUANDAA SADAKA YAKO YA MFUNGO, AMBAYO KWA MOYO WA KUPENDA UNAGUSWA KUITOA MWISHO WA MFUNGO HUU

Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »