MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12 -MAY [SIKU YA 10]

 

NGUVU YA UFUFUO

1. UMEFUFULIWA PAMOJA NA KRISTO YESU; Omba nguvu ya Ufufuo (nguvu ya Roho Mtakatifu) IBADILISHE KUFIKIRI KWAKO ili UYAWAZE YALIYO JUU (Ufikiri kwa kiwango cha juu katika kila eneo la maisha yako, na utofautishwe na wanadamu wengine, kwa namna ulivyo na uwezo na akili kubwa mno). Uhakikishe umeomba kwa imani, mpaka UWEZO WA KUYAWAZA YALIYO JUU ulioupokea kwa KUFUFULIWA PAMOJA NA KRISTO YESU uanze kuonekana kila siku maishani mwako.
(Wakolosai 3:1-2).

2. Tulikufa pamoja na Kristo, tukafufuliwa pamoja naye, UHAI WETU UMEFICHWA PAMOJA NA UHAI WA KRISTO YESU KATIKA MUNGU.
Omba kinyume na kila nguvu, mamlaka, Ufalme na giza linalotishia UHAI WAKO kiroho, kiuchumi, kiafya, ndoa, mahusiano, kazi za mikono yako, familia yako; Kwa sababu UHAI WAKO KATIKA KILA ENEO umefichwa na hakuna anaye/kinachoruhusiwa kuugusa au kuuharibu au kuuchezea.
(Wakolosai 3:3).

3. Kwakuwa TUMEFUFULIWA PAMOJA NA KRISTO YESU; Ni wajibu wetu KUVIFISHA VIUNGO VYETU VILIVYO KATIKA NCHI, UASHERATI, UCHAFU, TAMAA MBAYA, MAWAZO MABAYA, NA KUTAMANI…GHADHABU, MATUKANO, UOVU, MATUSI VINYWANI, UONGO, UTU WA KALE!
Itumie NGUVU YA UFUFUO kuvifisha vitu vyote hivi vilivyo katika nchi.
Omba Mungu akupe UTU MPYA.
(Wakolosai 3:1,5-10).

4. YESU TULIYE NAYE NDANI YETU NI UFUFUO NA UZIMA.
Tumia nguvu yake KUITA KILA KILICHOKUFA MAISHANI MWAKE KIWE HAI TENA KAMA ALIVYOMUITA LAZARO AKAWA HAI TENA.
Tumia mamlaka katika jina la Yesu kuvitamkia uhai vyote vilivyokufa maishani mwako.
(Yohana 11:25-26, 43-44).

5. TUMEFUFULIWA PAMOJA NA YESU, NA TUMEKETISHWA PAMOJA NAYE JUU SANA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO… ALIKO NDIKO TULIKO (Bila kujali maisha nje yanatuoneshaje au akili zetu zinaonaje)… NGUVU YA UFUFUO IMETUWEKA JUU MNO, JUU YA KILA MAMLAKA, UFALME, USULTANI, JUU YA KILA JINA, JUU MNO MNO MNO….!
(Waefeso 2:6, Ufunuo 1:19-23).
Vitu vyote vimetiishwa chini ya MIGUU YA YESU kwa ajili yangu na wewe (kanisa)!
KIRI NAFASI YAKO HII MPYA KILA SIKU, NA USIKUBALI KITU CHOCHOTE KIONEKANE KIKO JUU YAKO MAANA NI KINYUME NA NENO LA MUNGU KUHUSU WEWE!
Amuru na kutiisha kila kilichojiinua maishani mwako, angusha kila ngome ya adui kwenye kila eneo la maisha yako, hasa mawazo yako na fikira zako zinazokataa ukweli wa KIWANGO KIPYA TULICHONACHO NDANI YA YESU.
(2Wakorintho 10:3-5).

6. ROHO YULEYULE ALIYEMFUFUA YESU ANAKAA NDANI YETU, NA NENO LA MUNGU LINASEMA KAZI YAKE KUBWA NI KUUHISHA MIILI YETU… KILA ADUI ALICHOPANDA KWENYE MWILI WAKO NA AFYA YAKO HAKIRUHUSIWI KISHERIA KUKAA HAPO!
Amuru kila ugonjwa, udhaifu, maradhi, maumivu na mateso ambayo ADUI ANAKUWEKEA KWENYE MWILI WAKO; Yaharibiwe na NGUVU YA UFUFUO ALIYONAYO ROHO WA MUNGU ULIYEMBEBA!
Usisahau hii: KAZI MOJAWAPO KUBWA YA ROHO MTAKATIFU NI KUTUNZA AFYA YA MWILI WAKO.
(Warumi 8:11).
Usikubali kuwa na AFYA MGOGORO ilhali UNA ROHO MTAKATIFU ni matusi kwa KAZI YA MSALABA.
ITUMIE HIYO NGUVU KWA HASIRA YA KIMUNGU na uhakikishe huo ugonjwa na udhaifu umekufa kwa MOTO USIOZIMIKA WA ROHO MTAKATIFU.
Kila gugu life ubaki na ngano (afya tu)!
(Mathayo 3:11-12).

7. NGUVU YA UFUFUO inaweza kusafisha dhamiri zetu na kutuondolea MATENDO MAFU, Yanayotuzuia kumwabudu Mungu katika Utakatifu na usafi.
Omba nguvu ya Ufufuo iue kila matendo mafu ndani yako na kukusafisha dhamiri yako ili upate kumuabudu Mungu kwa usahihi na kwa ubora bila mzigo wowote.
(Waebrania 9:14).

8. KAZI MOJAWAPO YA NGUVU YA UFUFUO ni Kukukomboa na nguvu za kaburi na kukuokoa na kila namna ya mauti.
Omba Mungu afute kila mauti na nguvu ya kaburi kwenye kila eneo la maisha yako.
(Hosea 13:14).

HAKIKISHA UMEOMBA KWA MUDA WA KUTOSHA KILA OMBI ALILOTUPA ROHO MTAKATIFU HAPO JUU.

HITIMISHO

Hongera kwa kujitoa siku hizi kumi za mwisho wa mwezi wa tano kukua katika Neno, maombi, mfungo na nguvu za Mungu! Nina uhakika maisha yako hayatabaki yalivyokuwa na MILANGO MIKUBWA ITAFUNGULIWA MBELE ZAKO AMBAYO KUZIMU HAWAWEZI KUIFUNGA (Ufunuo 3:8)!

Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila,
Mchungaji mwanzilishi,
ABC GLOBAL.

 

Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »

USIOE KWA SABABU :2

  “Wenzako wote uliokua nao au kusoma nao wanaoa. Ndoa si ALISEREMA ARIJA AU MWENGE TUNAUKIMBIZA. Ndoa ni taasisi ambayo Mungu amemuwekea kila mmoja wetu

Read More »