MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12 -AUGUST [SIKU YA 7]

NGUVU ZA KUKABILI HALI ZA KIFO (POWER TO HANDLE DEADLY SITUATIONS).

Utangulizi;

Image result for a black fighter free stock

Kwenye maisha kuna hali ambazo zimekaa kama kifo, au ukizubaa zinaweza kupelekea kifo cha kiroho, mwili, ndoa, biashara au jambo fulani maishani mwako.
Hali hizi huwa kama moto mkubwa, mzigo mzito unaoonekana kama haubebeki, msimu mrefu wa hali ngumu na mbaya, mlima mkubwa unaoonekana kutosogea hata kidogo au maji mengi yanayotaka kukugharikisha.
Katika hali hizi, Mungu huonekana kama amelala, au amekuzibia masikio!
Hapo ndipo Ibilisi huja na kuanza kukuaminisha kwamba Mungu amekuacha au amekusahau!
Kama huna maarifa sahihi na bora katika Neno la Mungu kuhusu HALI HIZI ZA KIFO, HAKIKA ZINAKUUA NA WENGINE WAFAO!
Hizi ni hali zinazotikisa mno imani zetu.
Hali hizi huwafanya adui zetu waongee sana au kutudhihaki sisi na Mungu wetu!
Hali hizi huonekana kama ndiyo mwisho wetu na hatutatoka kamwe!
Hali hizi hufanya wengi waone Mungu ni muongo na Neno lake halifanyi kazi!
Lakini ukishinda na kuvuka huwa kuna utukufu mkubwa unakusubiri!
Kiwango kipya hutokea katika hilo jambo ambalo lilionekana tishio na linakumaliza!

MIFANO KATIKA MAANDIKO;

1. SARA NA IBRAHIM KATIKA UTASA WA MIAKA MINGI MNO.

Watu hawa walipewa ahadi na Mungu (Mungu alisema na kuahidi kwa kinywa chake) kuwa atawapa uzao, na watakuwa na watoto wengi kama nyota za mbinguni na mchanga wa bahari!
Lakini ilipita miaka 25 kutimia kwa ahadi hiyo!
Hapa katikati “walijaribiwa” na wakatafuta SHORTCUT kwa Ibrahimu kuzaa na kijakazi wake Hajiri kwa shinikizo la Sara mkewe!
Ilionekana hawana uwezo wa kupata mtoto kupitia TUMBO LA SARA mpaka malaika walipomtembelea wakati wakielekea Sodoma na Gomora na kutoa Neno la kinabii kuwa MWAKANI MAJIRA KAMA YALE ANGEPATA MTOTO WA KIUME… NA IKAWA HIVYO!
Hii ilikuwa hali ya kifo ambayo iliwachosha, kuwaminya, kuwavuruga, kupelekea watumie mbinu mbadala, LAKINI KWA SABABU HAWAKUPOTEZA UHUSIANO WAO NA MUNGU, WALIVUKA!
(Summary ya Mwanzo 12-22)!

2. WANA WA ISRAEL KATIKATI YA JESHI LA FARAO NA BAHARI YA SHAMU NA MILIMA!

Watu hawa walifika mahali ambapo ni kama walikuwa wamekwisha!
Jeshi kubwa lenye silaha kubwa na nzito likiwajia nyuma, mbele bahari ya shamu na wakiwa hawana meli, mtumbwi, jahazi wala boya la kuwavusha, na pembeni milima ambayo wasingekwenda kokote bali kufia mikononi mwa adui zao!
Wa kulia walilia
Wa kulaumu walilaumu
Wa kumtukana Musa walitukana
Wa kumuona Mungu muongo, walimuona muongo!
Lakini, Mbali ya Mungu kutofanya muujiza chapchap, bado aliendelea _kuwa nao taabuni_ kupitia nguzo ya wingu na nguzo ya moto!
Mwisho Mungu alifanya muujiza na kuigawa bahari ya Shamu mbele yao, akaitumia kama kaburi la kuzikia jeshi la Farao lililokuwa linawafuatia!
Mwisho wa siku HALI YA KIFO ILIYOKUWA IMEWAZUNGUK iligeuka ushuhuda na muujiza mkubwa!
(Kutoka sura 13-15)!

Ndiyo itakavyotokea kwako katika jina la Yesu!
Adui wanaokutesa hautawaona tena!
Watazama na kupotea na utaona hakika wokovu mkuu wa Bwana maishani mwako!
Bahari iliyoko mbele yako itatumika kulimeza jeshi linalokufuatia nyuma yako katika jina la Yesu!

3. JESHI LA ISRAEL NA GOLIATI

Hili jeshi la Mungu lilikutana na hali ya kifo.
Lilikutana na shujaa wa vita Goliati wa Gati, ambaye mbali ya kuwa hodari vitani, pia alikuwa hodari wa matusi!

Kwa siku 40 (mwezi mmoja na siku 10), wana wa Israeli walitukanwa, walitiwa hofu, walidhalilishwa, Mungu wao alionekana si lolote wala chochote, maombi yao ilionekana kama hayavuki kumfikia Mungu… Kifupi walichoka roho, nafsi na miili yao!
Lakini wakiwa katika hali hiyo, Mungu alileta wokovu kupitia kwa kijana mdogo, asiye na uzoefu wa vita aitwaye Daudi na jitu likauwawa!*
Unaweza kuwa umeomba Mungu akukwamue kiuchumi, halafu akakupa wazo dogo mno la biashara au kitu kidogo cha kusukuma muujiza wako, lakini ukakidharau na kupishana na majibu uliyosubiri kwa siku nyingi!
Hata Sauli na jeshi la Israeli walitaka kumpuuza Daudi ambaye alibeba suluhu ya hali ya kifo iliyowatesa kwa siku 40 mchana na usiku!

Nakuombea, Mungu akufungue macho ya moyo wako, na ufahamu wako, uweze kumpokea Daudi wako atakayemuua Goliati aliyekutesa kwa muda mrefu!
Daudi anaweza kuwa jambo fulani ambalo Mungu anakusukuma moyoni kulifanya, au ufunuo fulani moyoni au Neno fulani ulilosikia kwenye redio, TV, madhabahuni au kusoma kitabuni ambalo limebeba suluhu ya hali ya kifo uliyonayo!
Nakuombea Roho Mtakatifu akupe akili na ufahamu wa kujua mambo yakupasayo kutenda ili uvuke hapo ulipo!
(1Samweli 17 yote)!

4. SHEDRAKA, MESHAKI NA ABEDNEGO KWENYE TANURU YA MOTO!

Hawa vijana watatu wa Kiyahudi waligoma kuisujudia sanamu iliyochongwa na Mfalme Nebukadreza, kwa sababu walijua Mungu wao aliyezifanya Mbingu na nchi ndiye astahiliye ibada na si mtu au kitu kingine chochote!
Mbali ya kuona tanuru iliyochochewa moto mara saba zaidi mbele yao,HAWAKUIKANA IMANI YAO wala kushusha viwango vya Kumcha na kumheshimu Mungu wao hata katika nchi ya ugeni!

Mwisho wa siku, Mungu aliingia kwenye tanuru ya moto na kuwa nao humo na kuwatoa salama, na Mungu wao akawa ndiye Mungu pekee anayeabudiwa!
(Danieli sura ya 3 yote)!

Ninaona kila hali ngumu, mbaya na nzito maishani mwako ikitumika kuwa njia ya kukutangaza wewe na Mungu wako, katika jina la Yesu!

Ninaona wote waliokudhihaki na kumtukana Mungu wako wakiokoka kupitia miujiza mikubwa inayokuja maishani mwako kuanzia leo!

MAMBO YA KUFANYA UNAPOKUWA KATIKA HALI ZA KIFO ILI KUZALISHA MUUJIZA.

1. Tawala mdomo wako na maneno yako.
-Uzima au mauti yako iko kwenye maneno yako (Mithali 18:20-21).
-Kunaswa au kunasuliwa, kukamatwa au kuachiwa vyote vinategemea maneno yako unayosema (Mithali 6:2)!
-Utendaji wa Mungu kukusaidia au la, unategemea unachotamka (Hesabu 14:28, Isaya 57:19)!
-Malaika wanafanyia kazi kile unachosema ili kukusaidia au kutokusaidia (Danieli 10:10-12)!
CHUNGA MDOMO WAKO, LINDA KINYWA CHAKO!

2. Sifa ziwe kinywani mwako badala ya manung’uniko na lawama!

-Kila wakati sifa ziwe kinywani mwako (Zaburi 34:1)!
Sifa zinaangusha kuta (Yoshua 6:20)!
Sifa zinafungua magereza bila funguo za aliyekufunga ( Matendo 16:25-26)!
Sifa ni kiti anachokalia Mungu, ukimsifu ataonekana na kupangua kila hali ya kifo maishani mwako (Zaburi 22:3)!
ACHA KULALAMIKA, ANZA KUSIFU.

3. Imani na msimamo

Kama unataka kutoka kwenye hali yoyote ya mauti, lazima uunganishe imani yako na msimamo wako!

Lazima uwe kama wale Wakoma wanne waliosema, “KAMA TUKIFA NA TUFE” lakini hatutafia hapa tunawaendea Washami kuchukua chakula! (2Wafalme 7:3-7).

Lazima uwe kama Daudi, “MUNGU ALIYENIOKOA NA MAKUCHA YA SIMBA NA YA DUBU, ATANIOKOA NA MFILISTI HUYU…SITAKAA TU NA KUMUACHA AENDELEE KUTUKANA BILA KUSHUGHULIKIWA…NITAMUENDEA KWA JINA LA BWANA WA MAJESHI, NA NITAKATA KICHWA CHAKE!” (1Samweli 17).

Lazima uwe kama Shadraka Meshaki na Abednego!
Hawa walimwambia Mfalme, “MUNGU WETU AWEZA KUTUOKOA NA MOTO HUU ULIOTUWASHIA…HATA KAMA HATUTAPONA NA MOTO, HATUTAANGUKA NA KUISUJUDIA SANAMU YAKO” (Danieli 3).

Ukiwa na imani na misimamo kama hii, hakika utaongezeka kwenye orodha ya mashujaa waliotajwa kwenye Waebrania 11:32-38!

4. INUA MACHO YAKO JUU

Maana yake, omba kwa Bwana bila kujali unaona matokeo au la!
INUA MACHO YAKO JUU, MPAZIE MUNGU SAUTI YAKO, ELEZA MATATIZO YAKO, ELEZA MAUMIVU YAKO, ZAIDI ELEZA UAMINIFU WAKE KATIKA NENO, NA NAMNA UNAVYOMUAMINI NO MATTER WHAT!
(Zaburi 68:20, Hosea 13:14, 1Samweli 2:1-14, 1Nyakati 4:9-10).

5. AMBATANISHA NA KUFUNGA KWA KADRI UNAVYOWEZA

-Kupitia kufunga, Esta na taifa la Israel WALIEPUKA KIFO ambacho kilikuwa kinawakaribia muda wowote, na maadui zao wakafa badala yao (Esta 4:16 hadi Esta 10 utaona hii kitu waziwazi)

– Nabii Ezra na wana wa Israel walikuwa katika hatari ya kuuwawa na kuangamizwa kabisa na adui zao, wakiwa hawana msaada wa kijeshi wa mwanadamu, WALIJILETA MIKONONI MWA BWANA WA MAJESHI, MUNGU ALIYE NA NGUVU KULIKO MAUTI, NA AKAWATOA MIKONONI MWA ADUI ZAO (Ezra 8:21-22)!

-Wakati wa nabii Yoeli, watu wa Israel walikuwa wanapitia HALI MBAYA KIUCHUMI, ILIYOTISHIA KUUA MAISHA YAO, MIFUGO NA KILA KITU, lakini kupitia KUJINYENYEKEZA MBELE ZA MUNGU KUPITIA MFUNGO, Mungu aligeuza UTEKA WAO NA KUWARUDISHIA YOTE YALIYOPOTEA (Yoeli 1 yote na Yoeli 2:1-27).

DON’T UNDERMINE THE POWER OF FASTING, ESPECIALLY LONG DRY FASTINGS!

Hata kama una struggle na vifungo vya kitabia, kama ulevi, uzinzi, ulawiti, ushoga, usagaji, madawa ya kulevya na hata utumiaji madawa ya kulevya, UKIAMUA KUJIDHABIHU KUPITIA KUFUNGA NA KUJILETA MIGUUNI KWA MUNGU, VIFUNGO VYAKO VITAKUACHIA (Isaya 58:1-11).

MAOMBI

ASUBUHI

1. Muombe Mungu akupe neema ya kukusaidia nyakati kama hizi (Waebrania 4:16).

2. Muombe Mungu akupe lugha nzuri (abadili ulimi wako) usiongee na kutamka maneno ya kipumbavu yanayokumaliza na kukuzika kwenye hali za kifo (Zaburi 45:1, Zaburi 141:3)!

MCHANA

1. Muombe Mungu akupe Roho yake inayoambatana na Vazi la sifa (Isaya 61:3).

2. Muombe Mungu akuimarishe katika imani na msimamo (Isaya 43:1-2, Zaburi 118:10-12, Zaburi 143:12)!

JIONI

1. Tamka Neno kwa Bwana Yesu kwa ajili yangu Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila.
Unaponiombea, Mungu anakufungua na kugeuza uteka wako (Ayubu 42:10)!

2. Mshukuru Mungu kwa kukupa miujiza mikubwa leo kupitia mfungo huu.
(Zaburi 126:1-3, 1Yohana 5:14)!

Umebarikiwa sana,
Wewe ni jibu la mamilioni ya watu,
Tukutane kesho siku ya nane!

Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila,
Mchungaji Mwanzilishi,
ABC GLOBAL.

USIACHE KUTEMBELEA TOVUTI YETU KUJIFUNZA ZAIDI:
www.yesunibwana.co.tz

INSTAGRAM NIFUATE:
@mwalimukabigumila

TAFUTA CHANNEL HIZI YOUTUBE:

CHURCH STATION
AU
PASTOR DICKSON CORNEL KABIGUMILA

NB: ENDELEA KUANDAA SADAKA YAKO NZURI YA KUAMBATANISHA NA MFUNGO HUU KADRI UNAVYOGUSWA MOYONI, ITATOLEWA SIKU YA MWISHO YA MFUNGO

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »