MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12 -AUGUST [SIKU YA 6]

NGUVU YA KUKABILI HABARI MBAYA (THE POWER TO WITHSTAND BAD REPORTS).

Maandiko:

“Watu waliposikia HABARI HIZO MBAYA wakaomboleza wala hapana mtu aliyevaa vyombo vyake vya uzuri”
(Kutoka 33:4).

1. Habari mbaya zinaweza kuleta kilio na maombolezo kwa wanaozipokea

2. Habari mbaya anazopokea mtu zinaweza kuathiri hata uvaaji na mwonekano wake wa nje!

“Wakawaletea wana wa Israeli HABARI MBAYA ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni warefu mno. Kisha huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili, tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona….Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule. Kisha wana wa Israeli wakamnung’unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, ingekuwa heri kama tungelikufa katika nchi ya Misri, au ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili. Mbona Bwana anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa mateka; je si afadhali turudi Misri? Wakaambiana, na tumweke mtu mmoja awe akida, tukarudi Misri”
(Walawi 13:32-33, Walawi 14:1-4).

3. Habari mbaya zinaweza kukufanya uwe na shaka na ahadi za Mungu.

4. Habari mbaya zinaweza kukufanya uziamini haraka na kusahau ahadi nyingi za Mungu ulizojaza ndani yako!

5. Habari mbaya ni silaha ambayo adui anaitumia kuharibu hatma za watu wengi kwa kuwafanya watu WASEME MANENO YATAKAYOHARIBU MAISHA YAO WENYEWE!

6. Habari mbaya huzalisha manung’uniko kwa anayezipokea, na hii hupelekea Mungu kumkasirikia na kumpiga!

7. Habari mbaya huua ndoto alizokuwa amebeba mtu kana kwamba haziwezekani tena kwa sababu tu ya alichoambiwa, kinachoonekana kama kikwazo cha mafanikio anayoyataka!

8. Habari mbaya ni kipimo anachokitumia adui kumuonesha Mungu udhaifu wa mtu.
Wengi wamekwama hapa wasijue adui anakupima ili umkane Mungu kutokana na habari hizo ili akupate na kukumaliza!

“Kwa sababu hii, aliajiriwa, ili mimi niogope, nikafanye hivyo na kutenda dhambi, kisha wao wawe nazo HABARI MBAYA, ili wanishutumie”
(Nehemia 6:13).

9. Adui hutumia habari mbaya kama njia ya kupanda woga ndani ya watu!

10. Ibilisi hutumia habari mbaya kama njia ya kupitishia maamuzi ambayo mwisho wake mhusika atatenda dhambi!

11. Habari mbaya ni njia anayotumia Ibilisi ili akuchafulie sifa yako njema uliyojijengea kwa muda mrefu na gharama kubwa!

“Hataogopa HABARI MBAYA; Moyo wake u imara ukimtumaini Bwana”
(Zaburi 112:7).

12. Habari mbaya ni kipimo kinachotumika kupima kiasi gani unamtumaini Bwana!

13. Habari mbaya ni kipimo cha uimara au ulegevu wa moyo wako…. Ukiwa legevu matatizo kama pressure, ugonjwa wa moyo, uchungu, huzuni, kukurupuka vinajitokeza!

MAMBO YATAKAYOKUSAIDIA KUJENGA MSULI DHIDI YA HABARI MBAYA;

1. Jaza habari njema za Neno la Mungu moyoni mwako.
(Wakolosai 3:16-17, Zaburi 119:9-11).

2. Kuwa mtu wa kusifu (kumsifu Mungu kwa maneno na nyimbo) na maombi.
(Yakobo 5:13).

3. Jikumbushe shuhuda za matendo makuu aliyokwisha kukutendea Mungu au aliyokwishatenda kwa wengine!
Daudi alipopewa habari mbaya na za kutisha kuhusu jitu Goliati, alifungua moyo wake na kujikumbusha shuhuda zake mbili, kuhusu dubu na simba machungani.
(1Samweli 17:33-38).

4. Jijengee mtazamo wa kuwa “kila jaribu linalokuja kwako, TAYARI KUNA MLANGO WA KUTOKEA” hata kabla halijaja, na pia “LIKO NDANI YA UWEZO WAKO” ndio maana Mungu mwaminifu kaliruhusu lije kwako wakati huu…. Hii itakusaidia kufikiria zaidi KUTAFUTA MLANGO WA KUTOKEA badala ya jaribu!
(1Wakorintho 10:13).

MAOMBI

Asubuhi

1. Muombe Mungu akupe kiu na njaa isiyoisha ya Neno la Mungu na mafundisho, ambavyo vitakujenga mno moyo wako na kukusaidia ili habari mbaya zikija zisikuletee shida.
(Zaburi 112:7, Zaburi 119:9-11).

2. Omba Mungu akupe “Roho ya sifa” na “Roho ya neema na maombi” ambazo zitakusaidia kukabili kila habari mbaya inayokujia.
(Yakobo 5:13, Isaya 61:3, Zekaria 12:10).

Mchana:

1. Muombe Mungu akukumbushe shuhuda za matendo yake makuu aliyokwisha kukutendea, ambazo zitainua imani yako kukata kila kichwa cha Goliati aliye mbele zako.
(1Samweli 17:32-37, Ufunuo 12:11).

2. Muombe Mungu akusaidie kutafuta mlango wa kutoka kwenye majaribu badala ya kupoteza muda kuliangalia jaribu/habari mbaya!
(1Wakorintho 10:13).

Jioni

1. Omba lolote unalotaka Yesu akutendee.
(Marko 10:51, Luka 18:41).

2. Niombee mimi Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila.
(Isaya 52:13, Zaburi 89:20-37).

3. Mshukuru Mungu kwa kujibu kila ombi tuliloomba leo.
(Zaburi 66:20, Isaya 65:24).

Tukutane kesho Jumapili siku ya saba,
Umebarikiwa mno,
Wewe ni wa thamani mno,
Umebeba majibu ya mamilioni!

Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila
Mchungaji mwanzilishi,
ABC GLOBAL.

NIFUATE (FOLLOW) INSTAGRAM:
@mwalimukabigumila

USIACHE KUTEMBELEA TOVUTI YANGU YA:
www.yesunibwana.co.tz

YOUTUBE TAFUTA CHANNEL HIZI KUJIFUNZA ZAIDI:

CHURCH STATION

NA

PASTOR DICKSON CORNEL KABIGUMILA

NB: ENDELEA KUANDAA SADAKA YAKO UNAYOGUSWA KUAMBATANISHA NA MFUNGO HUU, UTAITOA MWISHO WA MFUNGO

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »

USIOE KWA SABABU :2

  “Wenzako wote uliokua nao au kusoma nao wanaoa. Ndoa si ALISEREMA ARIJA AU MWENGE TUNAUKIMBIZA. Ndoa ni taasisi ambayo Mungu amemuwekea kila mmoja wetu

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »