MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12 -AUGUST [SIKU YA 4]

KANUNI YA PILI: KANUNI YA WATU (THE PRINCIPLE OF PEOPLE).

Ut

Utangulizi

Maisha ni watu na watu ni maisha!
Ili Mungu ayastawishe maisha ya mtu hapa duniani, atafanya hivyo kupitia watu alionao duniani (Isaya 43:4).

Mungu akitaka kuleta utajiri na ukuu kwenye maisha ya mtu, atafanya hivyo kupitia watu (Isaya 60:11)!

Mafanikio na urahisi wa maisha ya mtu au kukwama na ugumu wa maisha ya mtu unategemea wingi au uchache wa watu sahihi alionao mtu (Mithali 14:28).

Wingi au uchache wa alivyonavyo mtu, uthamani na utele maishani mwa mtu, vinategemea kiwango chake cha kugusa maisha ya watu ambao Mungu anawapitisha maishani mwake (Luka 6:38).

Mungu kwa kutambua kanuni ya hii ya watu, ameweka kanuni ya kuishi vizuri na watu na kutafuta amani na kila mtu (Waebrania 12:14), maana huwezi jua nani anabeba kitu chako cha kukusogeza mahali, ni vema kuwa vizuri na kila mtu labda yeye akiamua kukuita adui!

KWANINI WATU NI WA MUHIMU;

1. Watu ni wawakilishi wa Mungu tusiyemuona (Mathayo 25:34-40).

2. Watu wamebeba mavuno ya mbegu za wema tunazopanda katika maisha (Luka 6:38).

3. Watu ni mali ya BWANA, kama Mungu anasema watu ni MALI kwake, maana yake watu ni mali, tukikaa nao vizuri maisha yetu yatakuwa mepesi mno (Zaburi 24:1).

4. Watu wana mali zetu, mguso wetu kwao (nuru na utukufu) tunaowapa utapelekea watujie na utajiri na vitu vizuri tunavyovihitaji (Isaya 60:1-4,11).

5. Mungu akikupenda, akikuthamini au kukuheshimu, anadhihirisha hilo kwako kupitia watu (Isaya 43:4).

6. Mungu akitaka kufanya chochote duniani, lazima awajulishe watu wake duniani, siri za mambo tunayotaka kwenye maisha toka kwa Mungu, tayari ziko kwa watu (Amosi 3:7, Zaburi 25:11).

7. Mungu hufunga majibu ya maswali na mahitaji ya dunia kwa watu. Watu wamebeba majibu tunayotafuta.
-Nuhu alibeba majibu (safina) ya kizazi kile cha wakati wake.
-Yusufu alibeba majibu (namna ya kukusanya chakula ndani ya miaka 7 na kuepuka njaa miaka 7 mingine) ya dunia yake.
-Musa alibeba majibu ya kilio cha wana wa Israeli walicholia kwa BWANA awatoe utumwani.

8. Kila mtu ana sura na mfano wa Mungu, kila mtu ni wa thamani mno mbele za Mungu (Mwanzo 1:26-27).

9. Kila mtu anabeba baraka ndani yake, hata kama haijaanza kuonekana nje (Mwanzo 1:28).

ILI UFANIKIWE DUNIANI;

1. Unahitaji watu sahihi kwenye maisha (Isaya 43:4).

2. Unahitaji wingi wa watu sahihi kwenye maisha yako (Mithali 14:28).

3. Unahitaji watu ambao wataambatana nawe/ wataelewa ulichobeba, ulichonacho na kukupa mkono wa shirika kuliko ndugu (Mithali 18:24).

4. Unahitaji watu wa kutangulia mbele yako kukutengenezea mazingira mazuri ya ulichobeba au unachotaka kufanya.

-Yohana alikuwa mtu sahihi aliyetangulia kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya alichobeba Yesu.

-Unahitaji watu/ mtu aliyetangulia kwenye jambo au vitu unavyotaka kufanya, kama kweli unataka kufanikiwa maishani.

5. Unahitaji watu wajuao majira na nyakati na vitu vipi sahihi vya kufanya.
Hawa watakusaidia kufanikiwa kwa urahisi.
(1Nyakati 12:32).

MAOMBI

1. Muombe Mungu akusaidie kukupa moyo wa heshima kwa kila mtu bila kujali hadhi, elimu, kipato na daraja alilopo maana kila mtu ni wa muhimu (Mwanzo 1:26-27).

2. Muombe Mungu akukutanishe na watu sahihi WA KUKUNOA, KUKUJENGA NA KUKUSAIDIA KUWA BORA DUNIANI (Mithali 27:17).

3. Muombe Mungu akukutanishe na watu sahihi wa KUKUSAIDIA KUTIMIZA KUSUDI NA MPANGO WA MUNGU MAISHANI MWAKO (Isaya 43:4).

4. Muombe Mungu akukutanishe na watu ambao WEWE UMEBEBA MAJIBU YAO, NA AKUSAIDIE UGUSE MAISHA YAO, ILI SIKU YA MWISHO USIAIBIKE NA KUKATALIWA (Mathayo 5:13-16, Wagalatia 6:9-10, Mathayo 25:31-40).

Umebarikiwa mno,
Mungu ana matarajio makubwa mno na maisha yako,
Dunia nzima inasubiri majibu toka kwako.
Jikubali na jiandae kuwa suluhu.

Tukutane kesho siku ya tano ya mfungo.

Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila,
Mchungaji mwanzilishi,
ABC GLOBAL.

TEMBELEA TOVUTI KWA MAFUNDISHO ZAIDI:
www.yesunibwana.co.tz

YOUTUBE
Tafuta na fuatilia:

CHURCH STATION

NA

PASTOR DICKSON CORNEL KABIGUMILA

NIFUATE INSTAGRAM:
@mwalimukabigumila

NB: SIKU YA MWISHO YA MFUNGO, KUTAKUWA NA SADAKA KADRI MUNGU ALIVYOKUJALIA NA KWA KADRI ULIVYOGUSWA KUPITIA MFUNGO HUU, MUNGU AKUTENDEE MEMA!

Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »