MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12 -APRIL [SIKU YA 8]

AINA TATU ZA NGUVU ATOAZO MUNGU KWA MTU ILI AWEZE KUPATA UTAJIRI NA MAFANIKIO

“Bali Utamkumbuka BWANA, Mungu Wako, MAANA NDIYE AKUPAYE NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI…” (Kumbukumbu 8:18).

Hapa Tumesoma Ya Kuwa Mungu Anatoa NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI, Na Haisemi Mungu Anatoa UTAJIRI!

Mungu Anakupa Wewe NGUVU Itakayokusaidia (KAMA UTAITUMIA) Ili Ikusaidie UUPATE UTAJIRI.
Kwa Lugha Nyepesi, Unaweza Kuwa Na Nguvu Hizi Tatu, Lakini Usipoziweka Kwenye UTENDAJI, Ukakaa Tu, UTAKUFA NA UMASIKINI WAKO!
Yeye Mungu Anakupa NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI; Wewe Ndiwe Unayechukua Hatua Ya “KUUTAFUTA UTAJIRI” Maana Hizo Nguvu Zinakusaidia Wewe “KUUPATA UTAJIRI”

Nguvu Anazotoa Mungu Kwa Mtu Ili Aweze Kuupata Utajiri Ni Hizi Hapa Tatu;

1.NGUVU ZA KIROHO/ NGUVU ZA ROHONI
Kwakweli, Kila Kitu Unachokitaka Kwenye Maisha Haya Ya Hapa Duniani Kina Msingi Na Asili Au Mwanzo Kwenye Ulimwengu Wa Roho/ Rohoni.
Na Ulimwengu Wa Roho Una Serikali Kuu Mbili; Serikali Ya Mungu Aliye Hai, Na Serikali Ya Ibilisi, Shetani.
Hizi Serikali Mbili Ndizo Zinazoamua Mafanikio Au Kushindwa Kwa Mwanadamu Huku Duniani.
Na Hakuna Mwanadamu Ambaye YUKO SEHEMU ZOTE MBILI; Ni Aidha Uko Kwa Mungu Ama Kwa Ibilisi.
Ukiwa Kwa Ibilisi Kupitia Mfumo Wako Ulio Kinyume Na Mapenzi Ya Mungu Na Maagizo Ya Neno Lake, Kufanikiwa Kwako Kutategemea KUVUNJA SHERIA, WIZI, RUSHWA NA KUKWEPA HAKI!
Ukiwa Kwenye Serikali Ya Mungu Ili Ufanikiwe Ni Lazima Uzingatie SHERIA, UWE MWAMINIFU, MWENYE HAKI NA UKWEPE NJIA ZOTE ZISIZO HALALI KWA MUNGU NA WANADAMU!
Ukimtii Mungu Na Kuvumilia Kudumu Katika Kutenda Yake, Baada Ya MUDA Utachomoza Na Kuanza Kwenda Mahali, NURU YAKO ITATOKEA MARA Kama MATOKEO YA UTIIFU WAKO KWA MUNGU.
Ukiwa Upande Wa Ibilisi, Kufanikiwa Kwako Na Kustawi Kunategemea Kudumu Katika Kutenda Uovu Na Kuvunja Taratibu Halali Za Mungu Na Wanadamu. Na Utafanikiwa Na Kuchomoza HARAKAHARAKA Lakini ANGUKO LAKE PIA NI KUBWA NA LA GHAFLA; UTATOWEKA KAMA MOSHI, UTATOWEKA KAMA UMANDE WA ASUBUHI, Mafanikio Na Utajiri Wako Unakuwa Wa Muda, Na Unaiangamiza Roho Yako Kama HAUTAGHAIRI NA KUMREJEA MUNGU MAPEMA!
Wanaodumu Na Mungu, Na Kukubali KUSOTA KWA HAKI NA UAMINIFU, Hawa HUKUSANYA TARATIBU Lakini UTAJIRI NA HESHIMA YAO HUDUMU; Maana Kuna Nguvu Ya Mungu Nyuma Kulinda Kila Walichonacho Na Wakipatacho!
HII NDIYO NGUVU YA KIROHO AITOAYO MUNGU; INAYOKUSAIDIA UFANIKIWE NA KUMZUIA YULE ALAYE!
Baadhi Ya Mambo Ya Kufanya Ili Uwe Na Nguvu Za Kiroho Kwenye Eneo La MAFANIKIO NA UTAJIRI; Uwe Mwaminifu Kwenye Fungu La Kumi Na Sadaka Za Kawaida (Malaki 3:8-11), Wahurumie Na Kuwasaidia Masikini, Wahitaji; WAJANE, YATIMA, WAGONJWA, WAFUNGWA (Mithali 19:17), Jizoeze Kuwa MTOAJI Kwa Watu Wengine Kwanza Kama Unataka Watu Wakupe Vitu (Luka 6:38), Hakikisha Mahusiano Yako Na Wazazi Wako Wa Kiroho Yako Sawa (Waefeso 6:1), Linda Uhusiano Wako Na Wazazi Wako Wa Kimwili; Baba Na Mama (Waefeso 6:2-3).
Wekeza Pesa Yako Na Nguvu Yako Kwenye Kazi Ya Mungu (Unamkumbuka Kornelio, Matendo 10? Unamkumbuka Dorkasi, Matendo 9:36-42? Unamkumbuka Mfalme Hezekia, Isaya 38?).
KAZI NI KWAKO; UFALME WA MUNGU UNATEKWA NA WENYE NGUVU!

2.NGUVU ZA KIAKILI/ NGUVU ZA UFAHAMU
Hizi Ni Nguvu Za Kiakili Na Kiufajhamu Atoazo Mungu Kwa Mtu Wake, Ili Aweze KUBUNI, KUWAZA NA KUFIKIRIA Vitu Ambavyo Vinahitajika Kwenye Maeneo Yaliyomzunguka.
Hii Ni Nguvu Ya Kimungu Inayofungua MACHO YAKO YA MOYONI Ili Uweze KUONA FURSA Za KIUCHUMI NA KIMAENDELEO Ambazo Wengine Waliokuzunguka HAWAZIONI!
Mungu Akikupatia Nguvu Ya KIAKILI; Ufahamu Wako Unafunguliwa, Na Unaweza Kuona Zaidi Ya Macho Haya Mawili Yaonavyo.
Unajikuta Umepata UWEZO Wa Kuona Yasiyokuwepo Lakini Yanayoweza Kuwepo. Na Kama Ukichukua Hatua Kuyatendea Kazi Yanageuza Kabisa MAISHA YAKO Kabisa.
Hii Ndiyo NGUVU YA KIAKILI Aliyompa BEZAREL MWANA WA HURI (Kutoka 31: 1-11).
Hii Ndiyo NGUVU YA KIAKILI Aliyompa DANIEL, SHEDRACK, MESHAKI NA ABEDNEGO (Daniel 1:17).
Hii Ndiyo NGUVU YA KIAKILI Aliyompa Nuhu Wakati Wa Kutengeneza Safina (Mwanzo 6:13-16,22).
Hii ndiyo NGUVU YA KIAKILI Aliyompa “MWENYE HEKIMA MASIKINI” Aliyeuokoa Mji Wake Usiangamizwe (Mhubiri 9:13-15).
KUSUDI LA MUNGU KUTUPA ROHO MTAKATIFU WAKRISTO WA SIKU HIZI ZA MWISHO NI ILI AINA HII YA AKILI YA KIMUNGU IWE NASI NA TUWEZE KUFANYA MAMBO MAKUBWA; MAMBO AMBAYO MACHO HAYAJAWAHI KUONA, WALA MASIKIO HAYAJAWAHI KUSIKIA, MAMBO AMBAYO HAYAJAWAHI KUINGIA KWENYE MIOYO YA WANADAMU WENGINE… TUMEPEWA ROHO WA MUNGU, MAKUSUDI “TUYAJUE” YOTE TULIYOKIRIMIWA NA MUNGU (TULIYOKWISHAPEWA NA MUNGU KWA UKARIMU WAKE)… (1Wakorintho 2:9-12)!

3.NGUVU YA MWILINI
Hii Ni Aina Ya Tatu Ya Nguvu Atoayo Mungu. Hii Ni Aina Ya Nguvu Inayohusika Na Kuweka Kwenye Utendaji Kile Ambacho AKILI NA UFAHAMU Vimeamua Kufanya.
Ni Nguvu Ya Kawaida Ya Mwili Ambayo Inakuwa Ndani Ya Mwili Wa Mtu Ili Kuusaidia Mwili Wake UTENDE KAZI ZAKE BILA TATIZO. Yaani Ni Ile Nguvu Ya Kiutendaji Ya Kila Siku Ya Mwili Ambayo Ni Matokeo Ya Kuwa AFYA IMARA NA TIMAMU!
Mungu Kwa Kujua Umuhimu Wa Afya (NGUVU YA MWILI) Aliwahakikishia Waisraeli Walipokuwa Wakienda Kanaani Ya Kuwa “ATAONDOA UGONJWA KATI YAO” (Kutoka 23:25), Kama Haitoshi Alisema “ATAKUWA MPONYAJI WAO” (Kutoka 15:26).
Nasi Kwenye AGANO JIPYA; Ameyatia MAGONJWA NA UDHAIFU WETU JUU YA MWILI WA YESU (Mathayo 8:17), Ili Ugonjwa Na Maradhi Visiwe Vizuizi Vya Afya Zetu Kiasi Cha Kutuzuia “KUFANIKIWA KATIKA MAMBO YETU YOTE NA KUWA NA AFYA KAMA ROHO ZETU ZIFANIKIWAVYO” (3 Yohana 1:2).

Wewe Ndiwe Uliyeshika Fnguo Za Mafanikio Yako; Nguvu Hizo Tatu Ziletazo Utajiri Umezijua, Ni Wajibu Wako KUZIJUA KWA KINA NA KUZITUMIA Kutoka Kwenye Umasikini Wako!

ANGALIZO; Hizi Kanuni Nilizoweka Hapa, Zinaweza Kugeuza Hali Yako Ya Uchumi Kama Utachukua Hatua Kutenga Muda Na Kulisoma Tena Somo Hili Mara Nyingi Uwezavyo; SOMA MISTARI YOTE KWA BIBLIA YAKO, ILI UJIONEE KILA KITU SAWA NA NENO LILIVYOSEMA; Kisha Anza Kutendea Kazi Kwenye Maisha Yako ya Kila Siku!

Pastor D.C.Kabigumila
August 3, 2012.
(Huu ni ufunuo wa Neno la Mungu wa August 03, 2012, miaka karibu 7 iliyopita, ambao ninaona moyoni mwangu, utakufaa sasa tena walau kuamsha kitu ndani yako ili uweze kupiga hatua fulani kwenye eneo la KUTAWALA UCHUMI)

Mafundisho
yesunibwana

WAZEE WA MKEKA/KUBETI MPOO!!

  USHUHUDA: AFUNGULIWA TOKA TABIA SUGU YA KUCHEZA KAMARI, MAARUFU KAMA KU-BET AU KUTANDIKA MIKEKA! Ngoja nikupe mchongo wa kukutoa jumla kwenye huu MSALA. Huu

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »