MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12 -APRIL [SIKU YA 6]

KANUNI YA IMANI (THE PRINCIPLE OF FAITH).

Utangulizi

Maisha yana kanuni nyingi ambazo Mungu ameziweka ambazo mwanadamu akizitendea kazi, zinaweza kuyarahisisha maisha yake na kuyafanya bora.

Mojawapo ya kanuni hizo ni kanuni ya imani.

Hii ni kanuni ambayo mwanadamu anaifanyia kazi kwa kujua au kutojua.

Mkulima anapanda mbegu wakati wa masika, anatarajia kuvuna miezi mitatu au sita mbele, HII NI IMANI.

Mme na mke wanaoana na wanapanga kuwa na mtoto mwaka mmoja ujao, HII NI IMANI.

Mfanyabiashara anafungua biashara yake, akitarajia wateja watakuja kununua bidhaa zake, HII NI IMANI.

Mwanafunzi anafanya mtihani, anasubiri matokeo miezi sita ijayo baada ya usahihishaji, anatarajia kufaulu, HII NI IMANI.

Imani ni KUWA NA HAKIKA YA MAMBO YATARAJIWAYO, YASIYOKUWEPO SASA, LAKINI UNATARAJIA YAWEPO (Waebrania 11:1).

Kutarajia mavuno baada ya kupanda mbegu ni imani.

Kutarajia mtoto baada ya mme na mke kukutana ni imani.

Kutarajia kufaulu baada ya kukusanya mtihani ni imani.

AINA ZA IMANI;

1. IMANI SAHIHI

Hii ni imani iliyojengwa kwa taarifa sahihi toka chanzo sahihi.

2. IMANI POTOFU

Hii ni imani isiyokuwa sahihi, iliyojengwa ndani ya mtu, kutokana na taarifa zisizokuwa sahihi kuhusu jambo.

Imani sahihi na imani potofu;

•Zote zinaweza kuingia ndani ya moyo wa mtu

•Zote ni imani bila kujali usahihi au upotofu wake

•Zote zina roho nyuma yake

•Zote zina chanzo chake

MAMBO UNAYOPASWA KUYAJUA KUHUSU IMANI;

1. Imani hukaa moyoni,

Marko 11:23-24, Warumi 10:9-10.

2. Imani ni mbegu,

Luka 17:6

3. Imani ni roho,

2Wakorintho 4:13

4. Imani huja kwa kusikia na tokana na kusikia,

Warumi 10:17, Marko 5:25-34.

5. Imani inaonekana,

Marko 2:5, Mathayo 8:10.

6. Imani humpa aliyenayo cha kufanya (matendo) ya kusababisha utimilifu wa anachokiamini, kama haikupi cha kufanya si imani ni matumaini,

Marko 5:25-34, Mathayo 8:5-13.

7. Imani huleta uhakika wa kinachotarajiwa kana kwamba kimekuwako,

Waebrania 11:1, Warumi 4:17-18.

8. Imani haina mipaka wala umbali katika kuzalisha matokeo,

Mathayo 8:5-13, Mathayo 15:22-28.

9. Utendaji wa nguvu za Mungu (upako) unategemea hali ya kuamini kwa wapokeaji,

Marko 6:1-6.

10. Imani moyoni mwa mtu ndiyo inayoamua matokeo ya Neno la Mungu analosikia au kusoma,

Waebrania 4:2.

MAMBO YATAKAYOKUSAIDIA KUKUZA IMANI YAKO;

1. Kulisikia Neno (Warumi 10:17).

•Kupitia semina

•Kupitia madarasa ya mafundisho

•Kupitia ibada zenye Neno

•Kupitia kujisomea mwenyewe maandiko

•Kupitia kusikiliza audio CD za mafundisho

•Kupitia kutazama video za mafundisho

•Kupitia kujisomea vitabu, majarida na notisi za Neno

2. Kwa kutenda unachoamini, imani bila matendo hufa, imani na matendo hukua.

Yakobo 2:15-26.

3. Kwa kuambatana au kuwafuatilia watu ambao tayari wanatenda mambo kwa imani.

Mithali 13:20.

Watu unaoambatana nao au kuwafuatilia wanaamua kiwango chako cha imani.

4. Kufunga na kuomba

-Wanafunzi wa Yesu walipokwama kumtoa pepo, walipouliza sababu ya wao kushindwa, aliwajibu ni kwa sababu ya UPUNGUFU WA IMANI YAO! Na akawashauri, kuwa NAMNA HII HAITOKI ISIPOKUWA KWA KUFUNGA NA KUOMBA, akimaanisha kuwa kufunga na KUOMBA kunaweza kutibu tatizo la upungufu wa imani zao, na kuinua imani (Mathayo 17:20-21).

MAOMBI

1. Muombe Mungu akupe nguvu ndani yako ya kufuatilia Neno la Mungu kwa namna mbali mbali ili uweze kukuza imani yako.

2. Muombe Mungu akupe ujasiri na msukumo wa kuitendea kazi imani uliyonayo ili ikue.

3. Muombe Mungu akukutanishe na watu sahihi watakaopelekea imani yako ikue na kuleta matokeo kwako binafsi na watu wakuzungukao.

Umebarikiwa mno,

Wewe ni mtu mkuu sana,

Hongera kwa kufunga na kukua ndani ya siku hizi kumi,

Dunia inasubiri majibu toka kwako!

Tukutane kesho siku ya saba.

Pst. Dickson Cornel Kabigumila.

Mchungaji kiongozi,

Assembly Of Believers Church (ABC),

27/04/2019.

Usiache kutembelea tovuti yangu ya mafundisho:

www.yesunibwana.co.tz

NB: ENDELEA KUANDAA SADAKA YAKO NZURI YA KUAMBATANISHA NA MFUNGO HUU, UTAITOA SIKU YA MWISHO YA MFUNGO, TAREHE 01/05/2019.

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

WAZEE WA MKEKA/KUBETI MPOO!!

  USHUHUDA: AFUNGULIWA TOKA TABIA SUGU YA KUCHEZA KAMARI, MAARUFU KAMA KU-BET AU KUTANDIKA MIKEKA! Ngoja nikupe mchongo wa kukutoa jumla kwenye huu MSALA. Huu

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »