MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12 -APRIL [SIKU YA 5 ]

KANUNI YA KUPANDA NA KUVUNA

(THE PRINCIPLE OF SOWING AND REAPING).

Utangulizi

Maisha ni shamba au ardhi ambayo inatawaliwa na kanuni ya kupanda na kuvuna.

Kila tendo tunalotenda duniani ni mbegu itakayotoa matokeo mazuri au mabaya kutegemea na uzuri au ubaya wa tendo husika.

Kila wazo tunalowaza ni mbegu, litaleta mavuno mazuri au mabaya kutegemea uzuri au ubaya wake.

Kila uamuzi tunaofanya maishani ni mbegu, kesho tutakutana na mavuno ya tulichoamua leo na tutalazimika kuyapokea.

Maneno yetu ni mbegu, tunavuna kila siku mavuno tokana na ubora au ubovu wa mbegu za maneno tulizopanda!

Bidii ni mbegu kama uvivu ulivyo mbegu.

Kila kinachofanywa kwa bidii au uvivu kitaleta matokeo (mavuno) maishani mwetu!

Sadaka tunazotoa ni mbegu.

Zikitolewa kwa ufasaha zinaleta matokeo chanya, zikitolewa ovyo zinaleta madhara na kukwama.

Kwa ujumla hatuwezi kuishi duniani na kuikwepa kanuni ya kupanda na kuvuna.

Kila mtu duniani anaiishi kanuni ya kupanda na kuvuna, kwa kujua au kutojua!

Ni vema kuijua kanuni hii ili kurahisisha maisha na kuepusha matatizo kwetu na vizazi vyetu baada yetu.

UKWELI KUHUSU KANUNI YA KUPANDA NA KUVUNA.

1. Aina ya mbegu unayopanda inaamua aina ya mavuno utakayovuna.

2. Aina ya udongo inakuchagulia aina ya mbegu ya kupanda juu yake, maana si kila mbegu inafaa katika kila udongo.

3. Ubora wa mbegu unaamua ubora wa mavuno.

4. Kiasi cha mbegu kinaamua kiasi cha mavuno.

Huwezi kupanda debe la mahindi ukavuna sawa na aliyepanda gunia zima.

5. Aina ya udongo inaweza kuathiri mavuno utakayopata.

Mbegu zilizopandwa na mpanzi zilikuwa za aina moja, lakini zilipoanguka palitofautiana, na hivyo matokeo au mavuno nayo yalikuwa tofauti.

6. Aina ya mbegu unayoipanda inaonesha aina ya imani yako uliyobeba, na aina ya imani inaonesha aina ya matarajio uliyonayo.

7. Hatua ya kupanda mbegu, inaweza kubadili majira na msimu uliokuwemo.

Isaka alikuwa kwenye kipindi cha njaa na ukame, akapanda mbegu akavuna na kuwa mkuu mahali ambapo watu wengine wanahangaika (Mwanzo 26:12).

8. Hatua ya kupanda mbegu, ndiyo inayomsukuma Mungu kuachilia baraka (Mwanzo 26:12).

9. Mpandanji hana mamlaka yote juu ya mbegu aliyoipanda kuleta akitarajiacho; Mpanzi mwenye akili anajua Mungu pekee ndiye aliye na kauli ya mwisho kwenye mbegu aliyopanda (1 Wakorintho 3:6-7).

10. Hata kutofanya kitu ni mbegu, na utapata mavuno yanayoitwa hakuna kitu/ hakuna badiliko!

11. Mungu pekee ndiye ajuaye mbegu sahihi za kupanda kwenye maisha yetu, na ameziweka kwenye Neno lake (Isaya 55:10-11).

12. Njia rahisi ya kutupa mavuno, ni kutonyamaza au kutulia, bali kudumu kupanda mbegu njema maishani mwetu kila wakati na kila tupatapo nafasi (Mhubiri 11:1-6).

BAADHI YA MBEGU TULIZONAZO KWENYE MAISHA;

1. NENO

1Petro 1:23, Luka 8:11.

2. MANENO

Mithali 18:20-21, Mathayo 12:36, Isaya 57:19.

3. DHAMBI

Isaya 3:11, Ezekieli 18:20, Ayubu 4:8-9.

4. HAKI

Isaya 3:10, Zaburi 112:2

5. IMANI

Yakobo 1:5-7, Marko 11:23-24, Luka 17:6.

6. MAAMUZI

Wagalatia 6:7-8, Mwanzo 4:6-7.

7. SADAKA

2Wakorintho 9:9-12, Waebrania 11:4.

8. BIDII

Mithali 13:4, Mithali 21:5, Mithali 22:29, Mithali 12:24.

9. MAWAZO

Isaya 55:8-10, 2Wakorintho 10:3-5, Zaburi 19:14.

10. MATENDO

Wagalatia 6:9-10, Wafilipi 2:10, Mathayo 5:13-16.

11. MAARIFA

Isaya 5:13, Mithali 11:9, Mithali 24:5.

MAOMBI

1. Muombe Mungu akupe hekima ya kukusaidia kupanda mbegu njema kila siku (Yakobo 1:5-7).

2. Muombe Mungu akurehemu na kukusamehe pale ulipopanda mbegu mbaya (Isaya 1:18, Isaya 43:25).

3. Muombe Mungu akuondolee madhara ya mbegu mbaya ulizokuwa umepanda, ili maisha mema aliyokukusudia yaonekane kwako (Matendo 3:19).

Umebarikiwa sana,

Wewe ni jibu la wengi,

Umebeba majibu ya dunia yako,

Tukutane kesho siku ya sita.

NDOA

Haikuanzishwa Na WANADAMU Bali MUNGU Ndiye Aliyeanzisha TAASISI HII… Imeanzishwa Na MUNGU Ambaye Ni Roho, Uwe Na Uhakika Haiwezi Kuendeshwa Kwa Kutegemea AKILI, HEKIMA NA

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »