MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12 -APRIL [SIKU YA 4]

 

KANUNI YA ULICHONACHO (THE PRINCIPLE OF WHAT YOU HAVE).

Utangulizi

Maisha ni mchezo wa kanuni, anayezijua na kuzipatia anaishi maisha ya mafanikio yasiyo na jasho.
Asiyejua na anayezikosea anaishia kuishi maisha ya kubahatisha.

Mojawapo ya kanuni ambayo Mungu ameiweka ambayo ni ya muhimu mno, ni kanuni ya ulichonacho!

Kanuni hii inasema, “Kila mtu ana kitu au vitu, ndani yake, kwenye mazingira yake na kwenye uwezo wa maamuzi yake”
Kanuni hii, nimeigundua kwenye maandiko matakatifu na nikaona niiweke kwenye maandishi kwa faida ya kizazi changu na vizazi vingi vijavyo!

Ukweli ni kwamba ndani ya kila mtu, kuna hazina zilizofichwa (2Wakorintho 4:7).

Pia kwenye mazingira yetu tuna hazina nyingi tulizonazo kama vile:
-Mungu (Ayubu 22:25).
-Vilivyofichika kwenye mazingira (Isaya 45:3).
-Watu (Isaya 43:4, Isaya 60:11, Luka 6:38).

Kwa pamoja, ukijumuisha hazina ndani ya mtu na kwenye mazingira ya mtu, utagundua, HAKUNA MTU ASIYE NA KITU.
NA HIKI NDICHO KINACHOZALISHA KANUNI YA ULICHONACHO.

Kanuni hii inalenga kumsaidia mtu kutambua alivyo navyo, namna ya kuvitunza, kuviendeleza, na kuvitumia ili vimsaidie kutimiza kusudi la kuumbwa kwake!!

BAADHI YA VITU ALIVYONAVYO MTU NDANI & KWENYE MAZINGIRA YAKE VINAVYOWEZA KUMFANYA AFANIKIWE NA KUSTAWI;

1. Sura na Mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26-27).

2. Nguvu ya baraka (Mwanzo 1:28).
Kila mtu aliyeumbwa na Mungu tayari ana baraka ndani yake, ni suala la kuileta nje.
Nguvu hii ya baraka ina nguvu kuu tano ndani yake kwa mjibu wa Mwanzo 1:28;
-Nguvu ya kuzaa
-Nguvu ya kuongezeka
-Nguvu ya kuenea (kuijaza nchi)
-Nguvu ya kutawala
-Nguvu ya utiisho

3. Akili
(Ayubu 32:8)

4. Mawazo
(Zaburi 19:14, Mithali 16:3).

5. Moyo
(Mithali 4:23, Luka 15:17).

6. Maamuzi & Machaguo
(Kumbukumbuku 30:15,19, Joshua 24:15).

7. Watu
(Isaya 43:4, Isaya 60:11, Mithali 14:28).

8. Muda
(Mhubiri 3:1-14, Ayubu 14:1-6, Yohana 9:4).

Kwa mtaji huu, KILA MTU ANA KITU, NA KILA MTU ANAWEZA KUFANIKIWA!

MAMBO YA KUJIFUNZA KUHUSU KANUNI YA ULICHONACHO;

1. Kila jaribu, changamoto au gumu lililoko mbele yako (wanalopitia watu wanaokuzunguka), ulichonacho ni jibu la kukitatua.
“NILICHONACHO ndicho nikupacho…”
(Matendo 3:6-8).

2. Watu wengi wamepofushwa na Shetani kukazania VISIVYO NA SULUHU YA KUDUMU, KIASI CHA KUACHA KUTAZAMA VYA MUHIMU WANAVYOVIHITAJI.
Huyu kiwete, alikazana kuomba pesa na dhahabu ambavyo haviponyi tatizo lake, badala ya kukazania UPONYAJI (Matendo 3:1-6).

3. Tutakapojua NGUVU YA TULICHONACHO tutapuuza udhaifu wetu katika tusichokuwa nacho, tutajiboresha kwenye TULICHONACHO na tutakuwa msaada na suluhu kwa wengi (Matendo 3:6).

4. Tulichonacho ni kikubwa, endapo tutaamua kufikiri sawasawa na vya kutosha (2Wafalme 4:1-7).

5. Tulichonacho kinatosha kutukwamua toka kwenye matatizo tuliyomo endapo tutakitambua na kujua namna ya kukitumia (2Wafalme 4:1-7).

6. Tulichonacho kinaweza kuleta mageuzi maishani mwetu, endapo tutapata mtu sahihi wa kutusaidia kukitambua na kukitumia ipasavyo (2Wafalme 4:1-7).

7. Ulichonacho ni kizuri, cha thamani, cha kukusaidia, lakini kinahitaji watu ili kitoe matokeo (2Wafalme 4:1-7).

8. Ulichonacho kinabeba utambulisho wako na ni kiashiria cha kusudi la kuumbwa kwako!

9. Shetani amekuwa akitumia mbinu ya kutuonesha tusivyokuwa navyo, ili tusipate muda wa kugundua tulivyonavyo tayari (1Wakorintho 2:9-12).

MAOMBI

1. Muombe Mungu akusaidie kugundua ulivyonavyo, ili vitumike kuinua maisha yako na watu wanaokuzunguka (Isaya 60:1-4, 1Wakorintho 2:9-12).

2. Muombe Roho Mtakatifu akusaidie usipagawe na usivyokuwa navyo, ili utumie muda mwingi kujinoa kwenye ulivyonavyo ili uwe bora katika hivyo.

3. Viorodheshe vitu ulivyonavyo, na uweke utaratibu mzuri wa kuviombea mpaka vianze kuzaa matokeo!

Umebarikiwa mno,
Wewe ni mtu mkuu sana,
Dunia inasubiri majibu toka kwako.
Tukutane kesho siku ya tano,

 

NB:USISAHAU KUANDAA SADAKA YAKO KAMA UNAVYOKUGUSWA NA MUNGU, KWA AJILI YA KUAMBATANISHA NA MFUNGO

USIOE KWA SABABU :2

  “Wenzako wote uliokua nao au kusoma nao wanaoa. Ndoa si ALISEREMA ARIJA AU MWENGE TUNAUKIMBIZA. Ndoa ni taasisi ambayo Mungu amemuwekea kila mmoja wetu

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »