MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12 -APRIL [SIKU YA 3]

KANUNI YA KAZI (THE PRINCIPLE OF WORK)

Utangulizi

Maisha tuliyopewa hapa duniani, yana kanuni nyingi mno.

Mojawapo ya kanuni hizo ni kanuni ya kazi.

Mungu mwenyewe ni muasisi wa kanuni hii, ALIFANYA KAZI KWA SIKU SITA, YA SABA AKAPUMZIKA TOKA KATIKA KAZI YAKE (Mwanzo 2:3).

Mungu ni mfanyakazi anayeipima na kuifanyia kazi yake tathmini kiasi cha kuona hakika ni njema (Mwanzo1:31).

Kazi ya Mungu inashangaza, kiasi cha mtunga zaburi kuisifu (Zaburi 8:3).

Mara baada ya Mungu kuumba mtu, kisha kumbariki, ALIPOMLETA TU DUNIANI, ALIMPA KAZI AFANYE (Mwanzo 2:15).

Maisha ya mwanadamu hapa duniani hayawezi kuwa nje ya kanuni ya kazi, tumekuja duniani kufanya kazi!

Siku ya hukumu, MUNGU ATAZILETA HUKUMUNI KAZI ZETU TULIZOFANYA DUNIANI (Mhubiri 12:14).

Yesu Kristo, Bwana wetu alikuwa kielelezo, ALIJUA YUKO DUNIANI KUFANYA KAZI ALIYOTUMWA NA BABA YAKE NA AIMALIZE, NA ALIHAKIKISHA AMEFANYA KAZI YAKE KATIKA MAISHA YAKE NA AKAIMALIZA (Yohana 17:4).

Ndugu yangu, siku ya hukumu, Mungu atatupima kile tulichofanya duniani; KILA KAZI YA MTU ITAPIMWA KWA MOTO (1Wakorintho 3:13).

Tupo duniani kama wabia na Mungu; TU WATENDAKAZI PAMOJA NA MUNGU HAPA DUNIANI, KUNA AGENDA YA MUNGU AMBAYO KILA MMOJA WETU AMEIBEBA (1Wakorintho 3:9).

UKWELI KUHUSU KANUNI YA KAZI;

1. Katika kila kazi kuna faida (Mithali 14:23).

2. Utukufu anaoachia Mungu juu ya mtu, unategemea kiwango na ubora wa utendaji na ukamilishaji kazi aliyopewa na Mungu (Yohana 17:4-5).

3. Ubora au udhaifu wa kazi alizofanya mtu duniani utaamua atapata thawabu/ taji mbinguni au la (1Wakorintho 3:13-15).

4. Kazi unazozifanya ndizo zitakazoamua kiwango cha utukufu anaopokea Mungu kupitia maisha yako (Mathayo 5:16, Mathayo 15:30-31).

5. Hata kama ni kibarua au ajira kwa mtu, Mungu anataka ufanye kazi hiyo kama amekuajiri yeye (Kolosai 3:22-24).

6. Kazi ndiyo inayoamua yupi awe nacho na yupi awe ombaomba (Mithali 20:4).

7. Kazi ndiyo inayoamua yupi awe mtawala na yupi atozwe kodi (Mithali 12:24).

8. Hakuna kazi inayoweza kusimama peke yake pasipo kibali na mkono wa Mungu (Zaburi 90:17).

9. Mungu ameficha baraka na utele kwenye kazi (Mithali 12:11).

10. Hata kama una mawazo mazuri kiasi gani, usipojenga ushirika na Mungu, hautafanikiwa katika kazi yoyote (Mithali 16:3).

11. Kazi uliyopewa na Mungu ndiyo inayoleta chakula chako na mahitaji yako maishani (1Wakorintho 9:1-14).

12. Ni agizo la Mungu kufanya kazi zetu wenyewe na si kuwa mizigo na mategemezi (2Wathesalonike 3:7-12).

Mungu akupe neema kuyafanya na kuyaishi haya!!

MAOMBI

1. Muombe akupe kutambua kazi aliyokupa kuifanya hapa duniani na kuimaliza kwa ubora na uaminifu (Yohana 4:31-34, Yohana 17:4).

2. Muombe Mungu akupe roho ya bidii katika kazi aliyokupa kuja kuifanya duniani (Mithali 22:29).

3. Muombe Mungu akupe kibali na upendeleo vitakavyofanya kazi aliyokupa duniani, kusimama na kuthibitika hata ukifa (Zaburi 90:17).

Umebarikiwa mno,

Umebeba majibu ya dunia yako,

Wewe ni mtu mkuu.

Tukutane kesho siku ya nne.

Pst. Dickson Cornel Kabigumila,

Mchungaji kiongozi,

Assembly Of Believers Church (ABC),

24/04/2019

Usiache kutembelea tovuti yangu kujifunza zaidi na kukua kiroho:

www.yesunibwana.co.tz

NB: ENDELEA KUMSIHI MUNGU AKUELEKEZE SADAKA GANI NA KIASI CHA KUTOA KUAMBATANA NA MFUNGO HUU, ITATOLEWA SIKU YA HITIMISHO LA MFUNGO, 01/05/2019.

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »