MFUNGO MAALUM WA SIKU KUMI [SIKU YA 6]- JULAI 2019

UPAKO MAALUMU WA KUTUNZA NA KUREKEBISHA MWILI WAKO/ AFYA YAKO (ANOINTING TO KEEP AND REPAIR YOUR PHYSICAL BODY

Utangulizi

Warumi 8:11
“Lakini, ikiwa ROHO YAKE yeye aliyemfufua Yesu katika wafu ANAKAA NDANI YENU, Yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ATAIHUISHA NA MIILI YENU ILIYO KATIKA HALI YA KUFA, kwa ROHO WAKE aliye ndani yenu”

Wakati nimeokoka sikuwa najua Mungu anajali wala kuthamini MWILI WA MTU ALIYEOKOKA. Kanisani kwangu tulisisitizwa Mungu anaangalia roho na si mwili kwa sababu mwili (damu na nyama) hautaurithi uzima wa milele.
Nakubali kabisa kuwa mwili hautaurithi uzima wa milele, walikuwa sahihi kabisa.
Lakini usahihi huo haukujitosheleza kwa marefu na mapana yake.
Niliposoma andiko hili la Warumi 8:11 nililiangalia mara mbili tatu.
Kwanza nilidhani nimesoma vibaya.
Nilidhani inasema ROHO WAKE ALIYEMO NDANI YETU ATAHUISHA ROHO ZETU.
Nikarudia kusoma na kusoma na kusoma nikaona mwishowe ROHO MTAKATIFU ALIYEMO NDANI YETU ANAWAJIBIKA KUHUISHA (KUIPA UZIMA) MIILI YA WOTE WALIOMWAMINI YESU KRISTO.

Nilipokuwa nikiendelea kusoma niligundua kuwa ALIYEUFUFUA NA KUUPA UHAI MWILI WA YESU NI ROHO MTAKATIFU.
Niliwaza na kutafakari kuhusu KUSULUBISHWA kwa Yesu, alivyoteswa na kuharibiwa sana mwili wake, ikiwemo kupigwa kwa mijeledi, kuchomwa mkuki, kubeba msalaba, kuburuzwa na mateso mengine makali.
Lakini siku ya tatu alipofufuliwa na ROHO MTAKATIFU kila kitu kwenye mwili wake kilirudi kana kwamba hakuwahi kuteswa au kusulubiwa.
Mungu alibakiza alama za misumari na mkuki kwa ajili ya ushuhuda kwa watu kama Thomaso wanaoamini kwa kuona!
Lakini huyu Yesu alikuwa ameponywa kila eneo na ROHO MTAKATIFU ndani ya sekunde chache za kufufuka.
Alipotoka nje (Yesu), hata akina Mariamu walishindwa kumtambua wakadhani ni Mlinzi wa kaburi, wakamsihi awaonyeshe alipomuweka Yesu wasijue ni Yesu mwenyewe.
Alikuwa FIT SANA kiasi kwamba hawa akina mama wasingeamini kwamba ule mwili uliosulubishwa uko mbele yao ukiwa mzima kabisa bila kasoro; HIKI NDICHO ANACHOWEZA KUFANYA ROHO MTAKATIFU!!!

Baadae niliendelea kuitafakari Yohana 11, Habari za Lazaro wa Bethania.
Huyu ndugu alikufa na alikuwa kaburini kwa siku nne.
Ndugu zake walisema ananuka sasa (maana yake ameoza).
Lakini kwa kauli moja ya Yesu, ROHO MTAKATIFU ALIMFUFUA NA KUUPONYA MWILI WOTE KAMA NDOTO VILE.
Viungo vilivyokuwa vimeoza vilipata uhai ndani ya sekunde tu baada ya Neno “Lazaro njoo” kutamkwa!!
HII NDIYO KAZI YA ROHO MTAKATIFU LINAPOKUJA SUALA LA KUPONYA MIILI YA WATAKATIFU.

Kinachotuponza kama watu waliookoka na Miili yetu kuendelea kuteswa na magonjwa ni kwa sababu ya KUTOJUA KWELI KAMA HIZI.
Lakini kwa waliojua wengi wamekuwa hawaamini kuwa Neno la Mungu ni kweli na lilichosema kuhusu Roho mtakatifu na miili yao ni sahihi!!
Ni wakati wa kuamka na kuacha mapokeo ya wanadamu na kuling’ang’ania Neno la Mungu.

Binafsi nina miaka 10 sasa nimeacha kuugua na kuwa rafiki wa magonjwa tangu nilipojua siri hii. Na WALA haiwezekani tena mimi kuwa mgonjwa tena kamwe!

Kumbe Roho mtakatifu aliyemo ndani yangu ana kazi ya KUHUISHA MWILI WANGU (KUUPA UHAI), na kazi yake si kugusa roho yangu na nafsi yangu tu.

Nimeondoa mipaka juu ya nguvu na utendaji wa Roho mtakatifu na nimemruhusu awe “Bwana aniponyaye” (Kutoka 15:26).
Sisubirii niugue ili niombe uponyaji.
Huwa namuambia nirekebishe na kuhuisha kila eneo langu lenye kasoro.
Na nimekuwa nikiishi kwenye AFYA YA KIUNGU (DIVINE HEALTH) kwa miaka zaidi ya kumi sasa na sina mpango wa kuumwa wala kuugua.
Nimepata tiba ya kudumu ya afya yangu.

3Yohana 1:2
*”Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote NA KUWA NA AFYA YAKO kama roho yako ifanikiwavyo”*
Mapenzi ya Mungu ya kwanza si kutuponya!
Mapenzi ya kwanza ya Mungu ni TUWE NA AFYA ZETU.
YAANI TUKAE BILA MAGONJWA kwa kadri tunavyoendelea kuwa deep katika Neno lake na ushirika naye!
Ndugu yangu kuna NGUVU YA KIUNGU MAALUM KABISA KWA AJILI YA KUTUNZA, KUPONYA NA KUREKEBISHA KASORO YOYOTE KWENYE MWILI WAKO.

Ayubu 33:4
“ROHO YA MUNGU IMENIUMBA, na pumzi za mwenyezi hunipa uhai”
Siku nilipoliona andiko hili nililia kwa uchungu!
Niliumia kwanini sikuliona au sikuwa naliona mapema?
Kwanini sikuona ufunuo unaohusu hali ya mwili wangu kwenye hilo andiko tangu mapema?
Nakumbuka wakati huo nilikuwa naugua malaria hata mara tatu kila mwezi… Nilipoliona na Mungu akanifunua macho lilinitoa sehemu na kukata jumla uonevu wa kuzimu kupitia magonjwa!

Niligundua kwa mujibu wa Ayubu 33:4, kumbe ROHO MTAKATIFU NDIYE ALIYENIUMBA.
Kama ni muumbaji na ANAKAA NDANI YANGU SASA baada ya kuokoka, basi anaweza kurekebisha, kukarabati na hata kuumba chochote kwenye mwili wangu.
Tangu wakati huo nimekuwa nikimuamini Roho wa Mungu kufanya SUPERNATURAL OBSERVATION AND PRESERVATION kwenye mwili wangu na hakika nimehama jumla kwenye orodha ya wanaofahamiana na bwana magonjwa!

Hakika ukiifahamu kweli hiyo kweli inakuweka huru kwenye hilo eneo ulilopata nuru (Yohana 8:32).

Ninakuombea uudake ufunuo huu na kuufanyia kazi.

Imagine mtu kama Musa, Ibilisi aligombea hadi mwili wake alipokufa (Yuda 1:9).
Musa ni mtu ambaye huoni rekodi yake ya kuumwa. Aliishi miaka 120, hakuwa na miwani wala mgongo wake haukupinda!

Elisha alipokufa, alikuwa na nguvu hii nyingi mno hadi kwenye mifupa yake (alijaa uzima).
Kiasi kwamba maiti ilipotupwa kwenye kaburi lenye mifupa iliyooza ya Elisha ilifufuka.
( 2Wafalme 13:21).

Natamani kila aliyeokoka ajae upako huu maalum mifupani mwake: MAGONJWA YATAJUTA KUKUFAHAMU!

Yesu alitembea kwenye upako huu.
Hakuna sehemu yenye rekodi au ushahidi kwamba Yesu aliugua au alilazwa au alikuwa hoi kwa ugonjwa.

Alitembea na haya mafuta maalumu ya kutunza na kuhuisha mwili wake.

Nakuombea hii nguvu ikuguse na kugeuza hali ya mwili wako.
Roho mtakatifu aamke ndani yako na kuanza kuhukumu kila chenye kuhatarisha hekalu la Mungu.

MAOMBI

ASUBUHI

OMBA

MUNGU ADHIHIRISHE UHALISIA WA NENO LAKE HILI, ILI NGUVU YAKE HII YA KUTUNZA AFYA NA MWILI WAKO IWE HALISI NA KUFANYA KAZI! KOMAA NA MUNGU SIKU YOTE YA LEO, USIKUBALI KWELI HIZI ZIBAKI KUWA NOTISI TU NZURI, NG’ANG’ANA ZIWE UHALISIA MAISHANI MWAKO KWA MIEZI YOTE SITA IJAYO NA MAISHA YAKO YOTE HAPA DUNIANI.
(Warumi 8:11, 1Petro 2:24).

MCHANA

OMBA
-MUNGU AKUHAMISHE VIWANGO VYA KUUMWA NA KUPONA, UHAMIE VIWANGO VYA KUWA NA AFYA MUDA WOTE (3Yohana 1:2).

-MUOMBE MUNGU AFYA YAKO IJE MARA (Isaya 58:8).

-MUOMBE MUNGU AKUPE KIU YA KUKAA NDANI YA NENO LAKE NA KUPATA SIRI ZAKE KUHUSU AFYA NA MAISHA MAREFU (Mithali 4:20-22).

JIONI

OMBA

-MUNGU AKULETEE AFYA NA UPONYAJI KWA MIEZI YOTE SITA IJAYO NA MAISHA YAKO YOTE CHINI YA JUA (Yeremia 33:6).

-MUNGU ADHIHIRISHE UHALISIA WA UTIMILIFU WA UNABII WA NENO LAKE NA MAGONJWA NA MARADHI YALIYOKUWA MAISHANI MWAKO YAHARIBIWE JUMLA (Mathayo 8:16-17).

UMEBARIKIWA MNO,
WEWE NI MTU MKUU, WEWE NI JIBU LA DUNIA YAKO.

TUKUTANE KESHO SIKU YA SABA,
PAMBANA UMALIZE SIKU ZOTE 10, USIKUBALI KUISHIA NJIANI.

Mchungaji kiongozi,
Makanisa ya ABC duniani,
Dickson Cornel Kabigumila,
27/07/2019.

 

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »