MFUNGO MAALUM WA SIKU KUMI [SIKU YA 4]- JULAI 2019

 

MATUMIZI SAHIHI YA HAZINA ALIZOWEKEZA MUNGU NDANI YETU

Utangulizi

Mungu alipomuumba mtu, ALIMUUMBA KWA MFANO NA SURA YAKE (Mwanzo 1:26-27).
Hii tu ni hazina kubwa mno.

Kama haitoshi MUNGU ALIMUWEKEA KILA MWANADAMU HAZINA NYINGINE IITWAYO BARAKA, ambayo ni UWEZO WA KUZAA, UWEZO WA KUONGEZEKA, UWEZO WA KUSAMBAZA KILICHOZALIWA, KUTIISHA NA KUTAWALA (Mwanzo 1:28).

Kama haitoshi, Mungu alipomuumba mtu ALIMPULIZIA PUMZI YA UHAI (Mwanzo 2:7).
Hii PUMZI YA UHAI haikuja bure, inaambatana na hazina ya AKILI (Ayubu 32:8).

Lakini kama haitoshi, kila mwanadamu ameumbwa na HAZINA NYINGINE iitwayo UWEZO WA KUWAZA NA KUFIKIRI (Zaburi 19:14, Zaburi 66:8).
Kila wazo ni hazina ya Mungu ndani yako.
Unaweza kuitumia hazina hii vibaya kwa kuwaza na kupanga vitu viovu, au unaweza kuyatumia kuzalisha vitu vyema vinavyomtukuza Mungu!

Hazina nyingine ambayo Mungu amempa Mwanadamu ni UHURU WA KUFANYA MAAMUZI NA MACHAGUO bila kuingiliwa na Mungu (Kumbukumbu 30:14,19).
UNA UHURU WA KUAMUA NA KUCHAGUA CHOCHOTE, NA WALA MUNGU HATAKUINGILIA KAMWE!
Hii ni hazina kubwa mno ambayo ikitumiwa vema na kwa usahihi inabadilisha hali ya maisha ya mtu jumla, na ikitumiwa vibaya pia inabadili maisha ya mtu na kuyaharibu!

Sasa ndio maana leo, Mungu anataka tuombee hazina hizi zote, ZITUMIKE KAMA ZINAVYOTAKIWA NA ZITUPATIE FAIDA LAKINI BILA KUVUNJA SHERIA YA MUNGU NA NENO LAKE!

MAMBO YA KUOMBEA;

ASUBUHI

OMBA
-Mungu akupe hekima yake ya kukusaidia KUTUMIA AKILI ULIYOPEWA NA MUNGU KWA VIWANGO INAVYOPASWA KUTUMIKA (Usiitumie akili yako chini ya viwango).
Andiko la kusimamia kwenye prayer point hii ni 1Wakorintho 15:34.

-Muombe Mungu akusaidie MIEZI HII SITA IJAYO akili yako itumike kwa viwango inavyostahili na ibadilishe maisha yako.
Andiko la kusimamia 1Samweli 18:5.

-Muombe Mungu akusaidie KUTENGENEZA/ KUFANYA AKILI kwenye yale mambo ambayo AKILI YAKO HAIKUWA VIZURI.
Ili mtu awe daktari, lazima AKILI YAKE IFANYWE HIVYO, hawi kwa kutamani bali kwa KUFANYA AKILI YAKE KUWA hivyo!
*”…Enyi wafalme FANYENI AKILI…”* (Zaburi 2:10).
Muombe Mungu akukutanishe na watu, vitabu, videos, groups zitakazofanya akili yako KUWA BORA kuelekea kwenye kile unachotaka kuwa au kufanya!

-Muombe Roho Mtakatifu APULIZE PUMZI YAKE KWENYE UTU WAKO WA NDANI ILI AKILI YAKO ILIYOLALA IAMKE NA KUZAA MATOKEO MIEZI SITA IJAYO!
*”… PUMZI YA MWENYEZI HUWAPA AKILI…”* (Ayubu 32:8).

MCHANA

-Muombe Mungu akusaidie kuwaza na kutafakari MAWAZO SAHIHI NA YENYE UTUKUFU KWA MIEZI YOTE SITA IJAYO (Wafilipi 4:8).

-Muombe Mungu akusaidie KUBADILI MAWAZO MABAYA YA MOYO WAKO ILI USIMHUZUNISHE MOYO WAKE (Mwanzo 6:5-6).

-Omba mamlaka ya Roho Mtakatifu ya kukusaidia KUANGUSHA KILA WAZO NA KILA FIKRA NDANI YAKO ILIYO KINYUME NA ELIMU YA MUNGU INAYOINUKA KINYUME NA MUNGU (2Wakorintho 10:3-5).

-Angusha kila WAZO AMBALO SHETANI ALIKUWA AMEFANIKIWA KULIPANDA MOYONI MWAKO ILI UMKOSEE MUNGU (Matendo 5:1-4).

JIONI

OMBA

Mungu akusaidie KUFANYA MAAMUZI NA MACHAGUO YALIYOJAA UZIMA NA BARAKA KATIKA MIEZI SITA IJAYO (Kumbukumbu 30:19).

-Muombe Mungu akupe hekima ya kukusaidia KUTAMBUA KILA NJIA YA MAUTI IONEKANAYO KWA NJE KUWA SAWA, KABLA HUJAICHAGUA IWE KWENYE NDOA, BIASHARA, HUDUMA AU CHOCHOTE UNACHOFANYA (Mithali 14:12).

-Muombe Mungu akusaidie USIFANYE MAAMUZI YANAYOHARIBU KESHO YAKO NA YA WENGI WANAOKUTEGEMEA KAMA ADAMU NA EVA WALIVYOFANYA, BALI AKUPE ROHO ZAKE SABA ZITAKAZOKUSAIDIA KUHUKUMU (KUFANYA MAAMUZI) SI KWA KUONA AU KUSIKIA (Isaya 11:2-3).

UMEBARIKIWA MNO,
WEWE NI WA THAMANI SANA,
UMEBEBA MAJIBU YA VIZAZI VINGI.

TUKUTANE KESHO SIKU YA TANO YA MFUNGO WETU,
USIKUBALI KUISHIA NJIANI MALIZA SIKU ZOTE 10 KWA UAMINIFU.

Mchungaji kiongozi,
Makanisa ya ABC duniani,
Dickson Cornel Kabigumila.
25/07/2019

NB: USIACHE KUMUOMBA MUNGU AKUSAIDIE KUPATA NA KUANDAA SADAKA NZURI YA KUAMBATANISHA NA MFUNGO HUU WA MIEZI SITA YA MWISHO WA MWAKA! SADAKA ITATOLEWA SIKU YA MWISHO YA MFUNGO.

Mawasiliano zaidi:
Tovuti: www.yesunibwana.co.tz
WhatsApp: 0655 466 675
Instagram: @mwalimukabigumila

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »