MFUNGO MAALUM WA SIKU KUMI [SIKU YA 2]- JULAI 2019

UWEPO WA MUNGU UPANDE WETU KATIKA MIEZI SITA IJAYO

 

Utangulizi

Hakuna kitu cha thamani kwenye maisha ya mtu hapa duniani kama uwepo wa Mungu!

Mungu akiwa upande wa mtu, HAKUNA WA KUWA JUU YAKE NA WA KUWA DHIDI YAKE AKASHINDA (Warumi 8:31).

Mungu akiwa pamoja na mtu, KILA GEREZA NA KIFUNGO VINAPOTEZA NGUVU DHIDI YAKE/ VINALEGEZWA (Matendo 16:25-28).

Mungu akiwa upande wa mtu, ISHARA, AJABU NA MIUJIZA vinakuwa sehemu ya maisha yake (Yohana 3:1-2).

Mungu akiwa upande wa mtu, MTU HUYO ATATHIBITIKA KATIKA LILE JAMBO ALILOPEWA KUFANYA NA MUNGU (1Samweli 3:19-20).

Mungu akiwa upande wa mtu, HAKUNA NDOTO, MAONO AU PICHA AMBAYO MTU HUYU HATAWEZA KUTIMIZA (Yoshua 1:1-8).

Mungu akiwa upande wa mtu, KILA HALI ILIYOKUFA NA KUOZA MAISHANI MWAKE (MZOGA) ITATOA ASALI/ ITAGEUKA KUWA WEMA NA UZURI (Waamuzi 14:5-9).

Mungu akiwa upande wa mtu, MILIMA (VIZUIZI) ITATOA NYIMBO, NA MITI YA KONDENI ITAMPIGIA MAKOFI (ATASHANGILIWA NA WATU) BILA KUJALI MAZINGIRA YA KIBINADAMU YALIONEKANA KAMA HANA TENA TUMAINI (Isaya 55:10-12).

Kwa sababu ya umuhimu wa UWEPO WA MUNGU (MUNGU KUWA NASI) KATIKA MIEZI HII SITA IJAYO, ndiyo maana tunataka TUMSIHI BWANA LEO, awe pamoja nasi na aende nasi katika miezi sita ijayo!

Musa alikataa KUSAFIRI NA WANA WA ISRAEL BILA UWEPO WA MUNGU! Alisema kama UWEPO WAKO HAUTAKWENDA NASI, USITUTOE HAPA (Kutoka 33:1-19).

Alijua kujaribu maisha BILA UHAKIKA WA UWEPO WAKE ni kufanya pata potea!

Alijua kujaribu KUTEMBEA MIEZI SITA IJAYO peke yetu, ni kujiweka kwenye hatari ya kushambuliwa na dhambi, dunia, Shetani na hila zake na kila namna ya vita na vikwazo ambavyo KIBINADAMU HATUNA UWEZO WA KUVITATUA!

Kama Musa alivyomng’ang’ana na kumlingana Mungu AENDE PAMOJA NAO, nasi leo siku hii ya pili, TUTAMUOMBA MUNGU AENDE NASI KATIKA MIEZI SITA YA MWISHO YA MWAKA 2019!

MAMBO YA KUOMBEA;

ASUBUHI

*”Na wanifanyie mahali (nafasi) ili NIPATE KUKAA KATIKATI YAO…”*
(Kutoka 25:8).

*”Bali mtu huyu ndiye NITAKAYE MTAZAMA, mtu mwenye MOYO ULIOPONDEKA, atetemekaye (anyenyekeaye na kutii) asikiapo NENO LANGU…”*
(Isaya 66:1-2, Msisitizo nimeweka mimi kama mwalimu)

OMBI
Muombe Mungu akusaidie KUSAFISHA MOYO WAKO NA KUONDOA KILA UCHAFU ULIO MOYONI MWAKO, MAANA NI WALE WENYE MOYO SAFI TU NDIO WANAOWEZA KUMUONA MUNGU NA KUMFAIDI (Mathayo 5:8, Waebrania 12:14).
NI WALE WENYE MIOYO SAFI, WASIO NA HILA MOYONI, HAO NDIO AMBAO HATA MAOMBI YAO YATAJIBIWA MIEZI SITA HII IJAYO (Zaburi 66:18-20)!
Hivyo basi, UMIMINE MOYO WAKO KWA UWAZI MBELE ZA MUNGU, KAMA MAJI (Maombolezo 2:19), MWAMBIE AKUSAIDIE KUONDOA KILA KINYAGO NA KILA UCHAFU ULIO KATIKA MOYO WAKO unaokuzuia USIMUONE MUNGU NA KUTEMBEA NAYE!
Vinyago hivyo ni pamoja na:
Mawazo mabaya (Zaburi 19:14, Zaburi 66:18),
Udanganyifu (Yeremia 17:9-10),
Uongo, kutokusamehe, uchungu, hasira, kuumizwa moyo na vitu vingine vichafu VINAVYOWEZA KUWA NDANI YA MOYO WA MTU HATA KAMA AMEOKOKA, KWA VILE TU HAJAWAHI KUUMIMINA MOYO WAKE WAZI MBELE ZA MUNGU ILI APONYWE NA KUTENGENEZWA APATE KUWA MTI WA HAKI WA MUNGU UNAOFANYA ATUKUZWE (Isaya 61:1-3)!
Hakikisha UMEUFUNUA MOYO WAKO KWA UWAZI MBELE ZA MUNGU, MRUHUSU AKAGUE KILA CHUMBA CHA MOYO WAKO, MRUHUSU AKUONESHE UDHAIFU NA UCHAFU ULIOMO HUMO, TUBU KWA DHATI, NA MUOMBE AKUPE MOYO SAFI NA ROHO ILIYOTULIA NDANI YAKO (Zaburi 51:1-17)!
Hakikisha UMEKUWA MKWELI NA MUWAZI NA MKWELI MBELE ZA MUNGU, ILI AKUPE MOYO WA NYAMA NA KUONDOA ULE WA JIWE, HAPO NDIPO ATAKAPOTEMBEA NA WEWE NA KUKUSHANGAZA KWA MEMA YAKE (Ezekieli 11:19, Ezekieli 36:25-27).
(Hakikisha umeomba ombi hili na kusoma kwa uaminifu kila andiko, na kuruhusu Mungu AGEUZE MOYO WAKO NA KUKUTAKASA ILI UWEZE KUTEMBEA PAMOJA NAYE)!
Wengine mtaponywa majeraha ya mioyo yaliyokaa muda mrefu,
Wasioweza kusamehe mtasamehe,
Wengine magonjwa yataponywa kwa sababu shida ilianzia kwenye moyo, ukisafishwa na kutakaswa yanaondolewa,
Wengine maisha yenu ya maombi, Neno na kumtafuta Mungu vitaongezeka, kwa sababu VILIVYOKUWA VIMECHUKUA NAFASI YA MUNGU VITANG’OLEWA MOYONI MWAKO!
Kikubwa, kila mmoja wetu ATAKUWA NA USHUHUDA YA KUWA JAMBO JIPYA LIMEZALIWA NDANI YAKE NA MAISHANI MWAKE (Isaya 43:18-19)!
UNAPOTENGENEZA HALI YA MOYO WAKO, UTAMUONA MUNGU HAKIKA (Yeremia 29:11-13).

MCHANA

*”MTAFUTENI BWANA MUNGU, MAADAMU ANAPATIKANA, MUITENI MAADAMU YU KARIBU, MTU MBAYA NA AZIACHE NJIA ZAKE, AMRUDIE MUNGU NAYE ATAMREHEMU, NA AREJEE KWA MUNGU WETU, NAYE ATAMSAMEHE KABISA…”*
(Isaya 55:6-12).

OMBI

Muombe Mungu arudishe mahusiano na ushirika na wewe uliokuwa umeharibika!
MWAMBIE BABA YAKO WA MBINGUNI YA KUWA UMEAMUA KUREJEA NAYE ATAKUSAMEHE KABISA, MWAMBIE UMEAMUA KUMRUDIA NAYE ATAKUREHEMU (Isaya 55:7).
MWAMBIE MUNGU KWA UWAZI KABISA YA KUWA UMEAMUA KUACHA KILA NJIA MBAYA MAISHANI MWAKO NA UMEAMUA KUTEMBEA NAYE KWA UAMINIFU!
Mwambie umeamua KUJITIA NIRA YAKE NA KUJITWIKA MZIGO WAKE, HIVYO UNAOMBA AKUPE RAHA TENA NAFSINI MWAKO NA MAISHANI MWAKO (Mathayo 11:2829)!
Uwepo wake ukija maishani mwako, UTAPATA RAHA KWEYE MIEZI YOTE SITA IJAYO na maisha yako yote yaliyobakia hapa DUNIANI (Hesabu 33:14-19)!

JIONI

*”Neno moja nimelitaka kwa BWANA, nalo ndilo nitakalolitafuta, NIKAE UWEPONI MWAKE SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU, NIUTAZAME UZURI WA BWANA (NIONE MAMBO MAZURI ALIYONAYO MUNGU KWA AJILI YANGU, WALA HATA MOJA LISINIPITE BALI YOTE YANIJIE), NA KUTAFAKARI HEKALUNI MWAKE…”*
(Zaburi 27:4 Msisitizo ni wangu kama mwalimu).

OMBI

JIACHIE UWEPONI MWA MUNGU, MWAMBIE NAMNA AMBAVYO NAFSI YAKO INAMTAMANI NA MOYO WAKO UNAMUONEA SHAUKU ILI UZIONE NGUVU NA UTUKUFU WAKE MAISHANI MWAKO (Zaburi 63:1-3)!
Mwambie JAMBO NAMBA MOJA UNALOLITAKA KWAKE SI PESA, UTAJIRI, MALI, UMAARUFU AU UKUU BALI UNAMTAKA YEYE NA UZURI WAKE MAISHANI MWAKO!

JIELEZE TU UWEPONI MWAKE, MWAMBIE KAMA VILE AYALA ATAMANIVYO MAJI YA MTO, NDIVYO WEWE PIA UNAVYOMTAMANI NA KUMHITAJI MAISHANI MWAKO (Zaburi 42:1-2)!

(Tumia jioni hii KUMUONESHA MUNGU KIU NA SHAUKU ULIYONAYO KWA AJILI YAKE: Isaya 55:1, Isaya 44:3, Mathayo 5:6).
Kama utaomba ombi hili kwa dhati, UWEPO WA MUNGU UTAKUFUNIKA NA UTAJUA WEWE NA BABA MU UMOJA SASA!

WEWE NI WA THAMANI,
WEWE NI MBARIKIWA,
WEWE NI JIBU LA DUNIA YAKO,
UMEBEBA MASULUHISHO YA WENGI,
HONGERA KWA KUMALIZA SIKU HII YA PILI KWA USHINDI.

TUKUTANE KESHO SIKU YETU YA TATU YA MFUNGO, JITAHIDI KUFUNGA KWA UAMINIFU, USIKUBALI CHAKULA AU RATIBA YOYOTE KUKUZUIA KUFUNGA SIKU ZOTE 10 KWA UAMINIFU NA UBORA!

Mchungaji kiongozi,
Makanisa ya ABC duniani,
Dickson Cornel Kabigumila,
23/07/2019.

NB: USIACHE KUANDAA SADAKA YAKO NZURI ITAKAYOAMBATANA NA MFUNGO HUU, MUOMBE MUNGU AKUSAIDIE KUJUA NINI UTOE NA KIASI GANI, KITAKACHOUGUSA MOYO WAKE, LAKINI KWA MOYO WA KUPENDA NA SI KWA KULAZIMISHWA! SADAKA HIYO ITATOLEWA SIKU YA MWISHO YA MFUNGO HUU.

Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »