MFUNGO MAALUM WA SIKU KUMI [SIKU YA 1]- JULAI 2019

WA KUOMBA KWA AJILI YA NUSU YA MWISHO YA MWAKA,
JULAI 22- JULAI 31, 2019

MCHUNGAJI NA MWALIMU DICKSON CORNEL KABIGUMILA.

 

UHUSIANO BINAFSI NA MUNGU

Utangulizi

Bwana Yesu alisema ya kuwa pasipo Yeye, sisi HATUWEZI JAMBO LOLOTE (Yohana 15:5).
Kuzaa kwetu na kuwa na mafanikio kama wana wa Mungu unategemea MUUNGANIKO NA MAHUSIANO YETU NA MZABIBU AMBAYE NI YESU (Yohana 15:1-6)!
Tukiwa vizuri na Yeye, MIEZI HII SITA IJAYO TUTAZAA SANA tena kwa wepesi, kwa sababu Yeye atakuwa chanzo halisi cha NGUVU nyuma ya ustawi na mafanikio yetu!

Hivyo kama tunataka kufanikiwa KWENYE MAENEO YOTE kwa miezi SITA ijayo lazima tuhakikishe MAHUSIANO YETU NA MUNGU yamekaa vizuri.

MAENEO YA KUOMBEA;

ASUBUHI

1. DHAMBI YOYOTE UKIZINGAYO UPESI NA KILA MZIGO UNAOKULEMEA
“Basi kwa kuwa tunalo wingu kubwa la mashahidi namna hii, NA TUWEKE KANDO KILA MZIGO UNAOTULEMEA NA KILA DHAMBI ITUZINGAYO UPESI, NA TUPIGE MBIO KATIKA MASHINDANO YALIYOWEKWA MBELE YETU…”
(Waebrania 12:1)

DHAMBI na MIZIGO (tabia mbaya) zilizo maishani mwa mtu ZINAMZUIA KUPIGA MBIO!
Zinakata kasi ya kiafya,
Zinakata kasi ya huduma,
Zinakata kasi ya uchumi,
Zinakata kasi ya kutembelewa na Mungu,
Zinazuia mema ya Mungu yaliyokusudiwa maishani mwa mtu yasifike!

OMBI
-Muombe Mungu AKUFUNGUE toka kwenye DHAMBI YOYOTE AMBAYO IMEKUNG’ANG’ANIA NA TABIA YOYOTE CHAFU AMBAYO INAKUTESA!
TAJA HIYO DHAMBI NA TABIA HUSIKA MBELE ZA MUNGU BILA KUIFICHA (Mithali 28:13),
MWELEZE MUNGU NAMNA AMBAVYO UNAJISIKIA VIBAYA NA UNAVYOUMIZWA NA HIYO DHAMBI.
KISHA MUOMBE AKUSAMEHE NA KUKUREHEMU (Mithali 28:13), na kisha OMBA YA KUISHINDA HIYO DHAMBI JUMLA (Mwanzo 4:7)!
Muombe Mungu AKUVISHE NGUVU YA UTAKATIFU KAMA BABA YAKO WA MBINGUNI ALIVYO MTAKATIFU (1Petro 1:15-16).

MCHANA

2. UHUSIANO ULIOPOA KATI YAKO NA MUNGU
“…KWA SABABU YA KUONGEZEKA KWA MAASI UPENDO WA WENGI UTAPOA”
(Mathayo 24:12).

OMBI
Muombe Mungu AUMIMINE TENA MOYONI MWAKO UPENDO WAKE ILI URUDI KUMPENDA KAMA KWANZA (Warumi 5:5).
Muombe akurudishie ule UPENDO uliokufanya UOMBE MNO, UKESHE SANA, UFUNGE MNO, UTOE SANA, UHUDHURIE IBADA BILA KUKOSA NA IKITOKEA UKAKOSA ILIKUWA INAKUUMA NA KUONA UMETENDA DHAMBI KUBWA LAKINI SASA UNAONA NI KAWAIDA, Msihi Mungu AURUDISHE UPENDO WAKE NDANI YAKO TENA!
Pia omba Mungu AKUPE TENA UPENDO WA KUWAPENDA WATU WENGINE WANAOKUZUNGUKA (JIRANI ZAKO) KAMA NAFSI YAKO!
Muombe akupe TABIA ZOTE ZA UPENDO AMBAZO haziko maishani mwako (1Wakorintho 13:1-10)!

JIONI

3. USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU
“…NA USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU, UKAE NASI SASA NA HATA MILELE…”
(2Wakorintho 13:14).

OMBI
Omba DHIDI ya kila kinachokula KIU YAKO YA IBADA;
-Maombi (1Thesalonike 5:16)
-Mifungo (Matendo 13:2)
-Utoaji (Matendo 10:1-3)
-Mikesha
-Usomaji wa Neno (Yeremia 15:16)
-Mahudhurio ya ibada (Waebrania 10:25)
Omba DHIDI ya kila kitu ambacho kinakupoza au kuzima moto wa uhusiano wako na Mungu, kama vile;
-Kampani na mazungumzo mabaya (1Kor 15:33),
-Mambo unayotazama (movie, tamthilia, page za mitandao, video za YouTube)
-Mambo unayosikiliza (Vipindi vya redio, stori za watu wenye mizaha, waovu ambao midomo yao haina neema),
OMBA TUNDA LA ROHO, vipande vyote tisa vya tunda la Roho VIWE HALISI MAISHANI MWAKO (Wagalatia 5:22-23),
Omba ROHO WA MUNGU aongoze kila eneo la maisha yako (Warumi 8:14)!

NB: JITAHIDI UFUNGE SIKU ZOTE 10 KWA UAMINIFU BILA KUKWEPA AU KURUKA HATA MOJA, LAKINI PIA ANDAA SADAKA UTAKAYOAMBATANISHA NA MFUNGO HUU MWISHO WA MFUNGO!

TUKUTANE KESHO SIKU YA PILI,
WEWE NI BARAKA YA WENGI,
UMEBARIKIWA SANA,

Mchungaji kiongozi,
Makanisa ya ABC duniani,
Dickson Cornel Kabigumila,
22/07/2019

WhatsApp: 0655 466 675

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

WAZEE WA MKEKA/KUBETI MPOO!!

  USHUHUDA: AFUNGULIWA TOKA TABIA SUGU YA KUCHEZA KAMARI, MAARUFU KAMA KU-BET AU KUTANDIKA MIKEKA! Ngoja nikupe mchongo wa kukutoa jumla kwenye huu MSALA. Huu

Read More »