MAPOKEO

( NA ATHARI ZAKE KATIKA MWILI WA KRISTO)

Huyu ndiye Adui wa kwanza wa Neno la Mungu
“ Mapokeo yana uwezo wa kulizuia Neno la Mungu kufanya kazi ”

Marko 7:13
[13]huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokeana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo.

Mapokeo haya ni kama haya

1. Mapokeo ya #Mababa wa kimila

Yoshua 24:2
[2]Yoshua akawaambia watu wote, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Baba zenu hapo zamani walikaa ng’ambo ya Mto, maana Tera, baba yake Ibrahimu, naye ni baba yake Nahori; #wakaitumikia #miungu mingine.

Ukiona Leo Watoto wanaenda kwa waganga wa kienyeji ujue walipokea huo mfumo kutoka kwa baba zao. Ukiona watoto wanaenda kwenye matambiko ujue walipokea hiyo elimu kutoka kwa baba zao. Ukiona Ibada za kifamilia za kimila ujue walijifunza kutoka kwa baba zao.

2. Mapokeo ya #Mababa wa Kiimani.
Marko 7:13
[13]huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu #mliyopokeana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo.

Hawa nao waliweka mifumo yao Binafsi iliyo kinyume na Neno la Mungu kwa faida zao Binafsi. Hufanya hivyo kutunza waumini na kutunza makanisa yao, huku wakizisema vibaya huduma zingine.

3. Mapokeo ya #Kidini
Marko 7:13
[13]huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokeana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo.

Utakuta huduma inapinga baadhi ya utendaji kazi wa Roho Mtakatifu kwasababu ya matakwa yao Binafsi, hawana hata andiko la kuwasaidia, ila tu wanamsimano na mifumo yao. wamehalalisha Baadhi ya vitu ambavyo haviko kabisa kwenye Neno la Mungu.

4. Mapokeo ya #Elimu ya Darasani + Falsafa + Utaalamu wenye hekima za Kibinadamu.

Wakolosai 2:8
[8]Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.

Hawa utakuta wanasema
Sio lazima kuombewa, wanakejeli huduma za Roho Mtakatifu kwa sirisiri huku wanajifanya wameokoka na watumishi wa Mungu. Wanafundisha elimu zao kuwaonyesha watu kuwa kuombewa ni ujinga. wamekuja kama wataalamu wa tiba fulani fulani hivi na wamewavuta wengi waliookoka. wanapinga kazi za Roho Mtakatifu kwa elimu zao na falsafa zao.

5. Mapokeo ya #Kutumia kanuni za kibinadamu na sio lazima Kuwa na kanuni za KiMungu ( Supernatural)

Hawa ndio wengi sana siku hizi za Mwisho

2 Timotheo 3:5
[5]wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.

Hawa wanataka waku-motivate, wanaamini wakiku-motivate things will change. Na hawataki uamini Supernatural. Wanamfano wa #UTAUWA lakini wanakana NGUVU YA MUNGU ( Supernatural)

Wanapinga Shuhuda za Uponyaji, Shuhuda za Financial Breakthrough, Wanapinga Supernatural speed hata kwenye Biashara.

UKITAKA NENO LA MUNGU LIFANYE KAZI NA LIKULETEE MATOKEO
“ Epuka Haya Makundi ”

JIEPUSHE NA HAYA
Na ukifanya hivyo utamruhusu Mungu kufanya kazi kwenye maisha yako na Neno la Mungu litakuwa na Matokeo kwenye maisha yako.

God Bless you

Pastor Ibrahim Amasi
ABC-KAHAMA

LivingWord
@2019

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »