MAMBO KADHAA NILIYOJIFUNZA KWENYE MIAKA MITATU YA KUWA MCHUNGAJI!Bwana Yesu Asifiwe sana!Nina kila sababu ya kumpa Bwana Yesu UTUKUFU na kumshukuru kwa wingi wa neema yake na fadhili zake, ZILIZOTEMBEA NAMIMI WALAU KUELEKEA MIAKA MITATU SASA YA HUDUMA!Namshukuru Mungu kwa miaka mitatu ya kujengwa, kufundishwa na kufundwa kwa habari ya utumishi na huduma!Imekuwa miaka ya kukaa kwenye darasa la Bwana haswaa! Nikiwa naelekea KWENYE SHUKRANI YA PEKEE KWA MUNGU WANGU KWA KUNISAIDIA NA KUNIBEBA KWA MBAWA ZAKE NDANI YA MIAKA MITATU YA HUDUMA (FULL TIME PASTORING), NIMEONELEA NIWEZE KU-SHARE MAMBO MAWILI MATATU NA NDUGU ZANGU KATIKA MWILI WA KRISTO KAMA SHULE YA HUDUMA NILIYOJIFUNZA NDANI YA MUDA HUO!Haya ni sehemu tu, ya mengi, niliyojifunza ndani ya muda mfupi sana wa huduma!6. Usiingie kwenye mtego wa kudhani kuwa wewe ni bora kuliko waliotangulia, heshimu mwili wa Kristo!Kwa miaka hii mitatu ya kwenda mahali ambapo palikuwa hapana aina ya huduma ambayo nimepandwa kuwa chini yake.Nimejifunza jambo moja dogo lakini linaweza kuamua sana MAHUSIANO YAKO NA WAZEE AU WATU WALIOTANGULIA KWENYE IMANI!Moja kati ya mtego mkubwa ambao vijana tunapitia na tunapaswa kuushinda KAMA TUNATAMANI KUFANYA VYEMA KAMA AU ZAIDI YA BABA ZETU WA VIZAZI VILIVYOPITA ni kuamua kuikumbatia kanuni ya heshima kwa waliotutangulia!Kwa sababu ya kuongezeka kwa maarifa na exposure na aina ya mtembeo ambao Bwana ameuachilia kwenye majira haya UNAWEZA KUINGIA KWENYE MTEGO WA KUJIONA KUWA WEWE NI BORA KULIKO WALE AMBAO WAMETANGULIA MBELE YETU!Kwa sababu Eli hafanyi yale ambayo ungetamani awe anayafanya au unayodhani ndio yalipaswa kufanyika IWE NI KWA SABABU YA KUACHWA NA BWANA, UZEE, AU KURIDHIKA NA MATOKEO ALIYOWAHI KUYAPATA HAPO NYUMA, BADO JAMBO MBONA NIMEJUA WATU HAWA WANAMJUA MUNGU, WANAJUA MTEMBEO WA MUNGU, WNAAIJUA NJIA, WANAJUA KIPI CHA KUFANYA NA KIPI CHA KUTOKUFANYA KWENYE HUDUMA!1 Samweli 3:1-9[1]Basi, mtoto Samweli akamtumikia BWANA mbele ya Eli. Na neno la BWANA lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri. [2]Ikawa wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona), [3]na taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la BWANA, palipokuwa na sanduku la Mungu; [4]basi, wakati huo BWANA akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa. [5]Akamwendea Eli kwa haraka, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akasema, Sikukuita; kalale tena. Naye akaenda, akalala tena. [6]BWANA akaita mara ya pili, Samweli! Samweli! Akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, Sikukuita, mwanangu; kalale tena. [7]Basi Samweli alikuwa hamjui BWANA bado, na neno la BWANA lilikuwa bado halijafunuliwa kwake. [8]BWANA akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli akatambua ya kuwa BWANA ndiye aliyemwita yule mtoto. [9]Kwa hivyo Eli akamwambia Samweli, Enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena, BWANA; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Basi Samweli akaenda akalala mahali pake. Kwa miaka mitatu nimejifunza kwa uwqzo, kuna majira mtumishi kijana ATASHAWISHIKA KUAMINI KWAMBA YEYE NI BORA KULIKO WALIOPITA, NA UONGO MWINGINE WA SHETANI UNAWEZA KUMUINGIA NA KUDHANI KUWA YEYE NDIO MTUMISHI KIJANA MWENYE MOTO NA KITU CHA UPEKEE SANA KULIKO WENGINE..Kwangu mimi nimejifunza, kila mtu aliyenitangulia kwenye kufanya hiki nachofanya KUNA JAMBO ANALIJUA AMBALO MIMI SILIJUI NA NAPASWA KUMSIKILIZA NA KUJIFUNZA KWAKE! Kwa kujua haya, niliamua kutoshindana wala kugombana na mtumishi yeyote ambaye yupo mbele yangu!Nikiwa nimekuja mbeya mara ya kwanza I WAS VERY AGGRESSIVE ON MY APPROACH TO MINISTRY, Nilijiingia mitaani na VYUONI kwa kasi na nguvu kubwa (HATA SASA NAFANYA JAPO KWA HEKIMA KUBWA SANA), Kwa sababu hiyo nilipata ushawishi mkubwa sana wa vijana wengi kunifuata NA WAKATI MWINGINE KUANZA KUPOST MASOMO YANGU KWA NGUVU, Jambo hili liliniletea shida kwa mababa kadhaa wa imani wa taasisi MBALIMBALI za kiimani!KUNA AMBAO WALIENDA MBALI ZAIDI MPAKA KUWATISHA NA KUWAPA LAANA BAADHI YA VIJANA AMBAO WALIJARIBU NA KUTHUBUTU WALAU KUHUDHURIA IBADA ZA ABC GLOBAL MBEYA, KUNA AMBAO WALIWAPIGA MARUFUKU VIJANA WAO KUNIPOST NA KUPOST JUMBE ZANGU!WENGINE WALIJIKWAA NA KUANZA KUNIHUBIRI MAKANISANI NA KUSEMA MIMI NI NABII WA UONGO, WALIJIKWA KWA KUSEMA HUDUMA GANI IPO NDANI YA KIBANDA CHA MPIRA NA MANENO MENGI MENGI YA KASHFA ILI KUNIPOTEZEA MVUTO NA KUZUIA WATU WASINIFATE, JAPO HII ILIKUWA FREE PUBLICITY KWANGU, KUNA WATU WALIBIDI WAJE ILI WAMUONE NABII WA UONGO NA UONGO WAKE UNAOBEBA VIJANA WA CHUO NA WASOMI!Mwanzoni nilikuwa naumia sana nikisikia baba amenisema au ananitazama kwa jicho la husuda, LAKINI BAADAE MUNGU AKANISAIDIA KWAMBA MIMI NAPASWA KUTEMBEA KATIKA UPENDO NA KUHESHIMU KILA ALIYE MBELE YANGU BILA KUJALI YEYE ANANICHUKULIAJE!Nikaanza kuwapenda na kuwazungumzia kwa mema tu, na nikaacha kabisa kusikiliza upande wa wao kunisema, MUNGU ALINIAMINI NA KUTENGENEZA WAINJILISTI KADHAA AMBAO NILIKUWA NAWAPA RUHUSA YA KWENDA KUHUBIRI MIKUTANO YAO NA KUFUNDISHA MAKANISA YAO KILA WALIPONIOMBA RUHUSA! Lakini pia najua kuna siku namimi nitazeeka, kuna siku namimi watakuja kuinuka vijana wenye moto sana NA WATU WA MAJIRA HAYO, NATAMANI KWENYE UZEE WANGU VIJANA WANIHESHIMU NA KUNITAMBUA KUWA MIONGONI WA WAZEE WALIOIITAABIKIA INJILI NA KUCHONGA RAMI KWA AJILI YA VIZAZI NA SIO KUINUA WAPINZANI NA WATU WATAKAO KUWA WASHINDANI WANGU.HAKIKISHA WATU WALIOKUTANGULIA UNAWAPA HESHIMA YAO!Inaendelea…#BilaYesuSinaMaisha #JesusGlorified #JesusExalted Pst Eskaka Chaula ABC GLOBAL MBEYA CITY #0718578313
HEKIMA ZA NDOA 3
“Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko