MAMBO 10 AMBAYO NINGEKUSHAURI UYAFANYE KAMA KWELI UNATAKA KUWA MTU MKUU

 

1. HAKIKISHA UMEOKOKA HARAKA IWEZEKANAVYO KAMA BADO HAUJAOKOKA! NA KAMA UMEOKOKA LAKINI BADO KUNA MAENEO UNAHANGAIKA NA DHAMBI MFANO UZINZI, UASHERATI, KUJICHUA (MASTURBATION), KUTAZAMA PICHA CHAFU (PORNOGRAPHY), KIBURI, DHARAU, MATUSI, UGOMVI, HASIRA, KUTOSAMEHE, NA MENGINE YOTE UNAYOJUA SI SAWA MBELE ZA MUNGU NA WANADAMU, HAKIKISHA UNATAFUTA MTUMISHI WA KWELI WA MUNGU, JIWEKE CHINI YAKE, KUBALI AKUSAIDIE, AKULEE NA KUKUSAIDIA KUTOKA KWENYE MNYORORO WOWOTE ULIONAO WA DHAMBI NA MAISHA YASIYOFAA!

2. KAMA UMRI WA KUOA AU KUOLEWA UMEFIKA, HAKIKISHA UNA UHUSIANO WA KINA NA BINAFSI NA MUNGU ILI AKUSAIDIE KUPATA MTU SAHIHI WA MAISHA! MAANA, “IF YOU WILL GET A WRONG WIFE, SHE WILL BECOME A KNIFE AND CHOP YOUR LIFE! THE SAME APPLIES TO BEAUTIFUL LADIES OUT THERE, UKIOLEWA NA MWANAUME MSHENZI UTAGEUKA PRAYER MACHINE!
SOMA WALAU VITABU 30-50 KUHUSU NAMNA YA KUPATA MWENZA, KUHUSU NDOA, FAMILIA NA MALEZI YA WATOTO KABLA YA KUFANYA UAMUZI WA KUSEMA NAOA/ NAOLEWA!
KAMA UKIFANYA HILI MAPEMA, NAKUHAKIKISHIA NEEMA YA MUNGU ITAKUONGOZA NA HAUTAKOSEA BALI UTAPATA MTU SAHIHI WA KUONGEZA THAMANI YAKO!

NYONGEZA: KAMA TAYARI UMEOA AU KUOLEWA, NA HAUKUPATA MSHAURI, MCHUNGAJI AU MTU WA KUKUAMBIA UMUHIMU WA KUSOMA WALAU VITABU 30-50 KUHUSU NDOA, FAMILIA NA MALEZI BASI HAUJACHELEWA, HAKIKISHA UNAANZA KUVINUNUA AU KU-DOWNLOAD VITABU VYA ENEO HILO NA HAKIKISHA UNAVISOMA, UNAVIELEWA NA KUVITENDEA KAZI NA HATA KAMA ULIKUWA KWENYE HALI MBAYA KIASI GANI, UTAPATA MWANGA WA KUITOA NDOA YAKO KWENYE JANGA NA SHIMO ILIKO!
ZINGATIA HAYA TAFADHALI!

3. HAKIKISHA UMEJIWEKA CHINI YA MTU MWAMINIFU, ANAYEWEZA KUKULEA NA KUKUWAJIBISHA!
TUNAISHI KWENYE KIZAZI CHA WATU WANAOFUNDISHWA KUJITAWALA, KUJIAMRIA MAMBO, KUWA HURU, KUJIONGOZA, NA KUENDESHA MAMBO YAO KIVYAO BILA KUWAJIBISHWA, KUSIMAMIWA NA KUFUATILIWA! INAONEKANA SPIRITUAL FATHER, MENTORS, NI WATU WANAOTAKA ZAKA YAKO, SADAKA NA WANAOTAFUTA KUJULIKANA NA KUSIFIWA KUPITIA MAFANIKIO YAKO, KISHA WAJITOKEZE NA WASEME, “THAT IS MY GIRL/BOY” SIKU UKITOBOA!

HII NI “AFRICAN MENTALITY” inayozuia WENGI KUKUA NA KUFIKIA MALENGO MAKUBWA MAANA WANAISHI KIHOLELA NA HAKUNA WA KUKUSEMA, KUKUKEMEA, KUKUULIZA, NA HUWAJIBIKI KWA YEYOTE, YOU JUST LIVE YOUR SMALL (MEDIOCRE) LIFE, UKIFURAHIA UHURU USIOKUPELEKA KOKOTE PAKUBWA!
BE UNDER A SPIRITUAL FATHER, AMBAYE UNAWEZA KUMPATA, UKAJIELEZA MAJANGA YAKO, UKATUBU MAUPUUZI YAKO, NA UKAOMBA HEKIMA NA MSAADA KWA UHURU MAANA UNAJULIKANA KWAKE NAYE ANAWAJIBIKA KWAKO!
MAKE SURE YOU HAVE MENTORS WHO YOU CAN GET DIRECT ACCESS TO THEM, OR INTERACT WITH THEM THROUGH BOOKS, VIDEOS, THEIR SEMINARS AND EVERY WAY POSSIBLE!

4. HAKIKISHA UNA MAHUSIANO MAZURI NA YA KURIDHISHA NA WAZAZI WAKO, AU WALIOKULEA, PAMOJA NA WATU WA NYUMBANI MWAKO (1TIMOTHEO 5:8, WAEFESO 6:1-3)!

-HAKIKISHA UNA MAWASILIANO YA UHAKIKA NA WAZAZI/ WALEZI WAKO HASA PAMOJA NA NDUGU ZAKO!

-HAKIKISHA UNA FUNGU LA FEDHA KWA AJILI YA KUGUSA WAZAZI/ WALEZI HATA KAMA WANAJIWEZA, HIYO NI MBEGU YA BARAKA MAISHANI MWAKO! HAKIKISHA WALAU WANAPATA HATA ELFU 20, 30, 50, LAKI NA KUENDELEA KWA KADRI YA PATO LAKO, HATA KAMA NI MWANAFUNZI WA CHUO, HAKIKISHA UNAJIBARIKIA KUPITIA KINYWA CHA MZAZI/MLEZI

MZAZI/MLEZI AKIPATA HICHO KISADAKA KILA MWEZI NA KUKUTAMKIA BARAKA MOYO WAKE UKIWA UMECHANGAMKA, HIYO NI HAZINA YA MAISHA MAREFU, HERI, USTAWI NA KUTOBOA KWENYE MAISHA KIRAHISI!

WENGI WENU MNA UWEZO KUTOA MAPESA KWA MITUME, MANABII, WACHUNGAJI, BILA KUJIHURUMIA, LAKINI HUKUMBUKI NI LINI UMEWAHI KUTOA PESA INAYOUMA KWA BABA NA MAMA YAKO MZAZI AU WATU WALIOKULEA!
HUWEZI KUPINDISHA KANUNI ZA UFALME WA MUNGU NA MAISHA YAKO YAKANYOOKA (1TIMOTHEO 5:8, WAEFESO 6:1-3)!
FANYIA KAZI ENEO HILI HARAKA KUANZIA MWEZI HUU NA MIEZI ILIYOBAKI YA MAISHA YAKO!

5. WEKEZA KWENYE MAARIFA KILA SIKU (INVEST IN KNOWLEDGE ON DAILY BASIS)!

-Mtu MWENYE hekima ana nguvu, NA MTU WA MAARIFA HUONGEZA UWEZO (Mithali 24:5). Ukitaka KUONGEZA UWEZO NA THAMANI YA MAISHA YAKO, HAKIKISHA UMEJAA MAARIFA KWENYE KILA ENEO! Yaani KIROHO, KIUCHUMI, NDOA, FAMILIA, NAMNA YA KUISHI NA WATU (RELATIONSHIPS), BIASHARA NA MENGINE YA MUHIMU KWENYE MAISHA!
*USIKUBALI SIKU IISHE BILA KUINGIZA KITU KIPYA*

-Hakikisha KILA SIKU UNASOMA KITABU (WALAU KILA WIKI UNAMALIZA KITABU KIMOJA, VITABU 4 KILA MWEZI), HII NDIYO SPEED YA CHINI KABISA YA MTU AMBAYE ANA MPANGO WA KUJA KUWA MTU MKUU NA KUACHA ALAMA DUNIANI!
-HAKIKISHA UNATAZAMA WALAU VIDEO MOJA KILA SIKU (KWA WIKI VIDEO 7, KWA MWEZI 30, KWA MWAKA 360+), HAKIKA HUWEZI KUWA “AVARAGE” PERSON KAMWE!

AKILI YAKO ITAKUA, UWAJIBIKAJI WAKO UTAONGEZEKA, NA PICHA YAKO YA MAISHA ITABADILIKA!

-UKIONA SIKU IMEISHA BILA KUWEKA KITU KIPYA TOKA KWENYE VYANZO HIVYO HAPO JUU, UWE NA UHAKIKA UMEJIKWAMISHA!

UNAJUA, NINYI NDUGU ZANGU, MMEZOEA WATU AMBAO WANAWATIA MOYO KWENYE UJINGA, WANAOTAKA KUWAONA MKO PALEPALE, HUKU WAO SIRINI WANAPIGA HATUA KUBWA, ILI MWISHO WA SIKU MJE KUWALAMBA MIGUU, KUWATETEMEKEA NA KUWAOGOPA, MKIWAONA NI MAALUM SANA!

MIMI NI TOFAUTI, NATAMANI KILA MMOJA AWE BORA MNO, TUWE NA MAELFU YA WATU WA THAMANI, WALIOJENGWA KWA KANUNI SAHIHI, WENYE KULETA HESHIMA YA MUNGU KWENYE KIZAZI CHAO, WENYE KUIGUSA DUNIA NA KUIBADILISHA!
NINAAMINI KWENYE *WINGI WENYE TIJA* KULIKO KUWA NA MTU MMOJA MMOJA ANAYESHANGILIWA (CELEBRITIES)!

6. HAKIKISHA UNAKUA KWENYE TUNDA LA ROHO (Wagalatia 5:22-23).

-Hakikisha vipande vyote 9 vilivyo kwenye TUNDA LA ROHO VIPO MAISHANI MWAKO, na watu wanaviona bila hata kuvitaja!
Namaanisha Upendo, Furaha, Amani, Uvumilivu, Utu wema, Fadhili, Uaminifu, Upole na Kiasi!

HIZI NI TABIA 9 ZA MUNGU NDANI YA MWANADAMU, UKIWA NA HAYA YOTE, YEMEJENGEKA NA KUWA LIFESTYLE, YAANI HAUIGIZI, YANA FLOW NJE AUTOMATIC, WEWE HAUWEZI KUKWAMA KOKOTE!

-KUTENDA DHAMBI NI MATOKEO YA KUTOFANYA KAZI KWA TUNDA LA ROHO

-Matendo ya mwili (dhambi) ni kinyume cha UTENDAJI WA TUNDA LA ROHO (Wagalatia 5:16-22)!

-Uki-flow kwenye TUNDA LA ROHO kama LIFESTYLE YAKO, dhambi itakuwa msamiati usiokuwepo maishani mwako!

– Roho Mtakatifu ULIYENAYE, jumlisha KUTUMIA MUDA WAKO WALAU DK 30 AU SAA 1 KUOMBA HII KITU IUMBIKE NDANI YAKO, vitakubadili na KUKUFANYA MTU MWINGINE!

-TUNDA LA ROHO NDIYO MAANA HALISI YA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU.

7. MAHUSIANO YAKO NA WATU WENGINE!

-Mungu ametuumba tuishi na watu hapa duniani, na hautakwepa watu kamwe!
-Mipenyo, baraka, pesa, ustawi, na hatua zetu za maendeleo ZINAWATEGEMEA WATU NA ZIMESHAFUNGWA KWA WATU!

-Ukiwa na huduma ya kiroho HAITAKUWA NA MASHIKO BILA WATU!

-Ukiwa na biashara bila WATEJA (watu), unapoteza muda!

-Ukiwa na kipawa bila WATU unajitekenya tu na kucheka mwenyewe, hakitakunufaisha kamwe!

-Mungu hutoa WATU kwa ajili yetu na kabila za watu kwa ajili ya maisha yetu (Isaya 43:4).

-Mambo tunayoyahitaji tayari yako kwa watu, lakini INATULAZIMU KUYAGUSA NA KUYABARIKI MAISHA YAO KWANZA ndipo watatupa waliyonayo (Luka 6:38)!

-Ili uweze kuvuta watu maishani mwako wenye baraka zako, tafuta NURU NA UTUKUFU WA MUNGU UNAOONEKANA WAZI KWA KILA MTU/ BE EXCEPTIONAL (Isaya 60:1-10)!

-Utukufu wa mfalme ni WINGI WA WATU WAKE (Mithali 14:28)!
Maana yake, KADRI ULIVYOZUNGUKWA NA WATU SAHIHI, MAISHA YAKO YATAKUWA BORA MNO kuliko wale ambao WANAJIFANYA WANAYASUKUMA PEKE YAO!

BE SURROUNDED BY RIGHT PEOPLE, ASK GOD FOR RIGHT PEOPLE (Psalms 2:8)!

-Tunza MAHUSIANO YAKO NA WATU WAZURI ULIONAO, na hakikisha UNATAFUTA AMANI NA SULUHU NA WALE AMBAO HAMUONGEI AU HAMUELEWANI (Waebrania 12:14)!

8. FANYA VITU KUELEKEA MAHALI FULANI UNAPOJIONA KILA SIKU

-Kama una mpango wa kuwa MHUDUMU WA INJILI MWENYE MGUSO, hakikisha UNAKUZA UFAHAMU WAKO KWENYE ENEO HUSIKA KILA SIKU!
•Tumia muda wako na vitu vya upande huo

-Kama una mpango wa kuwa MFANYABIASHARA MKUBWA wekeza kwenye kujua sana eneo hilo

-Kama una mpango WA KUWA KIONGOZI MKUBWA WA NAFASI ZA KIUTAWALA hakikisha UNAJIKUZA KWENYE ENEO HILO kila siku!

-HAKIKISHA HUTUMII MUDA WAKO KWENYE VITU AMBAVYO HAVICHANGII KUKUPELEKA UNAPOTAKA KUWA KESHO!

-USITUMIE MUDA WAKO KWENYE VITU VINAVYOKUBURUDISHA TU, LAKINI HAVIJENGI MNARA WA KESHO UNAYOITAKA!

-USISEME NI GAME TU NACHEZA, NI COMEDY TU NAPENDA, NI MOVIE NIMEZOEA… KAMA HAZIKUPI HATUA KUELEKEA KWENYE ENEO UNALOTAKA DUNIA IKUTAMBUE NA KUKUHESHIMU, NI SUMU HIYO HAITAKIWI!

9. TENGENEZA TABIA ZAKO AMBAZO SI NZURI AMBAZO UNAJUA KABISA ZINAKUSUMBUA, ILI UKIWA JUU ZISIJE KUWA SABABU YA AIBU NA ANGUKO LAKO!

Maandiko yanasema, “MAINZI MAFU HUVUNDISHA MARHAMU YA MUUZA MAFUTA…” (Mhubiri 10:1).
Hii ina maana ya kwamba HAYA MAINZI YALIKUWA YANACHEZA CHEZA NA KURUKA RUKA JUU YA MARHAMU (MAFUTA YENYE HARUFU NZURI) na muuzaji HAKUWA SERIOUS KUWAFUKUZA HAWA NZI MAPEMA! Alijivunia HARUFU NZURI YA BIDHAA YAKE akiamini ya kuwa ITANUNULIKA TU MAANA INA HARUFU NZURI! Matokeo yake YALE MAINZI (TABIA MBAYA) YAKATUA KWENYE MARHAMU (MANUKATO YALE MAZURI)… Harufu haikubadilika, lakini KILA WANUNUZI WALIPOKUWA WAKIJA KUNUNUA, anashangaa HAWANUNUI WANAISHIA KUTAZAMA NA KUONDOKA!

Kumbe yale MAINZI YAMEANGUKIA MLE, YAMEKUNYA HUMO, YAMEFIA HUMO, NA KILA MMOJA ANAWEZA KUONA WAZI YA KUWA ile MARHAMU “si pure tena” iko CONTAMINATED NA UCHAFU, soko lake LIKAFA GHAFLA BIN VUUUU!

HUU NDIO UHALISIA UNAOWATOKEA WATU WENGI WENYE VIPAWA NA UKUU NDANI YAO (MARHAMU);

-Kuna MANZI MAFU (tabia mbaya ambazo wao tu ndio wanajua wanazo na wana struggle nazo), ambazo WENGINE HUSEMA ilimradi HAZIATHIRI kuhubiri kwangu, kuimba kwangu, uandishi wangu, utume, uchungaji, unabii au uwezo wangu wa kufanya biashara, HAINA HAJA YA KUDEAL NA HII KITU INIACHIE SASA KABLA SIJAWA EXPOSED KWA WATU WENGI!

-Hivyo huyu mtu ANAKAZANIA UPANDE MMOJA WA KIPAWA (MARHAMU) anaacha KUUA MANZI AMBAYO YATAKUJA SIKU MOJA KUFIA KWENYE MARHAMU NA KUUA JUMLA ALIYOYAJENGA KWA MIAKA MINGI!

Wengine hizo tabia mbaya (MAINZI mafu) ni:
-Uzinzi (yakiwemo mambo kama KUJICHUA, PICHA CHAFU, uasherati)
-Ulevi
-Kupoteza na kuchezea muda
-Hasira
-Kutosamehe
-Wivu
-Mashindano
-Kupenda sifa na
-Kiburi
-Dharau
-Kupenda kuinuliwa na kuheshimiwa sanaaa
-Kupenda utambuliwe
-Kupenda uonwe wa maana au wa tofauti na wengine
-Usengenyaji
-Kuongea ovyo (kutoweza kuzuia mdomo na kuwa msikiaji zaidi)
-Ujuaji (kila kitu wewe unajifanya unajua, matokeo yake watu wanaamua kukuacha uharibikiwe au upotee)

10. Jifunze kuwapa PESA NA VITU wale ambao WANAYAJENGA MAISHA YAKO kiroho, kiuchumi, familia, ndoa, kikazi, kibiashara nk!

Maandiko yanazungumzia Malkia wa Sheba AMBAYE alikuja na dhahabu na vitu vingine kumpatia Suleiman, MTU MWENYE HEKIMA WA WAKATI wao (1Wafalme 10:10).

-Ilimpatia NAFASI KWENYE MOYO WA SULEIMANI

-Ilimfanya SULEIMAN AFUNGUKE NA KUMWAGA MADINI ZAIDI hadi yule mama akasema, NILIYOAMBIWA HAYAJAFIKA NUSU YA YALE NILIYOJIONEA NA KUSIKIA TOKA KWAKO (She got more than she knew),

-Kupitia zawadi ALIZOMPATIA SULEIMANI (si maneno matupu), ALIMCHOKOZA NA KUMFANYA SULEIMANI AFUNGUKE ZAIDI YA YALE AMBAYO ALIYASEMA YAKAJULIKANA KWA WATU! She caused him to OPEN THE HIDDEN WISDOM that other people WILL NEVER HEAR AND KNOW!

Yaani Suleiman alimwaga vya ziada kwa sababu ya NGUVU YA KILICHOTOLEWA (ZAWADI YA DHAHABU NA MENGINE) ALIYOPEWA!

-Maandiko yako very clear ya kwamba, *ZAWADI YA MTU itampatia kibali (The gift of a man shall make a room for him)* hii ni Mithali 18:16!

-Tenga kwenye pesa yako, na pato lako kuwe na bajeti kabisa ya BABA WA KIROHO, na MENTORS ambao WANAJIFANYA UTOKE MAHALI ULIPO NA KUPIGA HATUA KUELEKEA UNAPOJIONA!
USIPENDE KUSEMA TU, “Ubarikiwe sana, unanisogeza hatua!”

FANYA HIVYO KWA PESA YAKO PIA.
Kwa kufanya hivyo UNAFANYA HUYU MTU AKUPE SUPER PRIORITY NA SPECIAL ATTENTION
MIMI NIMEMALIZA KWA LEO!
KAMA UNA LOLOTE TUKUTANE INBOX!
Asante kwa kufuatilia kuanzia 1 hadi 10!

KITAKACHOKUBADILISHIA MAISHA YAKO SI KUYAJUA HAYA, NI KUKUBALI TU KUYAISHI NA KUYATENDA NDIKO KUTAKUFANYA MIAKA 10 IJAYO TUKUTANE MAHALI UKIWA MTU WA MAANA KATI YA WENGI WALIOKO DUNIANI!
NI MIMI,

Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »

USIOE KWA SABABU :2

  “Wenzako wote uliokua nao au kusoma nao wanaoa. Ndoa si ALISEREMA ARIJA AU MWENGE TUNAUKIMBIZA. Ndoa ni taasisi ambayo Mungu amemuwekea kila mmoja wetu

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »