MALIMBUKO

Malimbuko Ni sadaka ya KIAGANO Ambayo mtoaji anatoa KIPATO CHAKE CHA KWANZA [Faida kwenye bishara, mshahara wa kwanza, mazao ya kwanza (au hela iliyopatikana kutokana na mauzo ya mazao ya kwanza), mifugo ya kwanza kuzaliwa au pesa iliyopatikana baada ya mauzo ya hiyo mifugo ya kwanza].

malimbuko ya Nyanya

UTOAJI WAKE

Ni sadaka ya HIARI, Na Inatolewa na mtu MWENYE UFUNUO NA MAARIFA; Yaani anayejua ANACHOFANYA KWA MUNGU NA NINI ATAPATA KWA MUNGU.
Si sadaka ya kidini, wala si sadaka ya kisheria au ya lazima.
Mtu ambaye anataka kutembea kwenye AGANO LA UCHUMI na Mungu Aliye hai, Ili Mungu Amstawishe huwa anaitoa sadaka hii.
Na Mungu huwa ANAMUWEKEA MTU MAELEKEZO YA WAPI AKAITOE.

NAMNA INAVYOTOLEWA

Haitolewi kidini, bali inatolewa kwa Ufunuo; Ukijua nini unafanya na nini unatarajia kupokea kwa Mungu.
Unatoa Kipato chako cha kwanza: cha biashara, kazi, kilimo au mifugo.
Kwa waliokomaa wanatoa MALIMBUKO YA MAPATO YAO YA MWANZO WA MWAKA KILA MWAKA: Mfano, Mfanyabiashara anaweza kutoa faida ya mwezi wa kwanza, Mfanyakazi anaweza kutoa mshahara wake wa kwanza [wa mwezi Januari].
Ni sadaka ya hiari, si ya lazima. Wanatoa “wenye jicho la ziada” wanaotaka “kwenda ngazi za juu sana na Mungu kwenye Uchumi wao”
Mungu atakupa msukumo au maelekezo moyoni wapi ukaitoe.

MTU ANAPOTOA MALIMBUKO ANAKUWA ANAMAANISHA YAFUATAYO MBELE ZA MUNGU:

  1.  Unamuonesha Mungu kwamba Yeye ni WA KWANZA KWAKO Kabla ya kula kwako, kuvaa kwako, mahitaji yako nakadhalika… NAFASI YA MUNGU.
  2.  Kumfungulia Mungu mlango [Kumruhusu] aingie kwenye hicho chanzo chako cha uchumi ulichokitolea Malimbuko… Kampuni, biashara, mashamba, mifugo VINAWEKWA WAKFU Mikononi mwa MUNGU.
  3. Ni kumuonesha Mungu kwamba “SITEGEMEI HIKI KINITUNZE AU KINIFANIKISHE” Ila Wewe “ULIYENITUNZA KABLA SIJAWA NACHO UTANITUNZA HATA HIKI KISIPOKUWEPO”
  4. Ni kumwambia Mungu kwamba “MSINGI WA UCHUMI WAKO” Umeujenga kwake; Hivyo ATAKUWA NGAZI YA KUPANDA KWAKO kwenda UTUKUFU ULIO MBELE YAKO; Maana Mungu AMEYAFUNGA MAISHA KWENYE HATUA [LEVELS].
  5. Unaonesha kwa vitendo kwamba UMEINGIA AGANO NA MUNGU ALIYE HAI Na Umeisaliti “miungu” mingine; Unakuwa umefunga milango dhidi ya miungu mingine.
  6. Kama ni mfanyakazi unakuwa UMEMRUHUSU MUNGU WAKO Kuingia kwenye ile kampuni, shirika, wizara nakadhalika na huko ATAPIGANA VITA ZAKO ZOTE Ambazo Adui atazileta dhidi yako kukutoa hapo… Lakini pia ITAKUDHIHIRISHA NA KUKUFUNUA Kama Yusufu kwa Potifa… Vitu kama PROMOTION [Kupanda ngazi na vyeo] itakuwa kugusa tu.
  7. Itaonesha wazi THAMANI NA UPENDO wako kwa Mungu wako.
    Yesu Alimuuliza Petro, “Je wanipenda kuliko hawa??” akimaanisha SAMAKI NA KIPATO CHA UVUVI…. Unapofuzu “KUTOA KIPATO CHAKO CHA KWANZA [MALIMBUKO]” Unakuwa umefanya kama Petro; Umeonesha WAZI Ni nani anayeujaza moyo wako!!

Watoto wachanga katika KANUNI ZA UFALME WA MUNGU Watakwambia MALIMBUKO Ni sadaka ya AGANO LA KALE… Ila kwangu ninayejua “MUNGU NI MUNGU ANAYESHIKA MAAGANO” Nakwambia hii NI SADAKA ISIYO NA MPAKA WA UTENDAJI KAZI… Unaweza ku-download aliyonayo Mungu kupitia sadaka hii.
Usisahau sijakwambai uilete kwangu, hivyo sikufundishi kwa personal ambitions and motives, ni kwa faida yako na uchumi wako.
Mimi nimefundisha, Wewe weka kwenye matendo.
Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com