MAJIBU YA SWALI

YAH: MAJIBU KWA SWALI KAULI ISEMAYO, “KAMA KWELI WATUMISHI NA WALIOOKOKA WANAWEZA KUOMBEA WAGONJWA WAKAPONA, KWANINI WASIENDE MAHOSPITALINI NA KUPONYA WALE WATU WALIOLALA KULE WAKIWA NA MATESO MAKALI NA WAKIWA WAGONJWA KWELI NA SI KUTULETEA SHUHUDA ETI WANAOMBEA WATU WANAPONA MAKANISANI?

MAJIBU NA MCHUNGAJI Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila;

1. Bwana Yesu ambaye ni mwanzilishi wa imani ya wokovu (Mathayo 1:21, Wakolosai 1:13, Matendo 4:12), mwanzilishi wa huduma ya kuponya wagonjwa (Matendo 10:38), aliyetoa mamlaka na nguvu ya uponyaji kuwa sehemu ya ishara zinazofuatana na waaminio (Marko 16:17-20), aliyesema kazi zote ambazo Yeye alifanya (ikiwemo kuponya wagonjwa), na sisi tunaoamini tutafanya (Yohana 14:12), muasisi wa karama za Roho zikiwemo uponyaji, matendo ya miujiza na imani (1Wakorintho 12:6-12), ambazo hasa ndizo zinazohitajika kuponya wagonjwa, YEYE AKIWA HAPA DUNIANI, ALIWAHI KWENDA HOSPITALI MOJA TU IITWAYO ” BETHZATA” ILIYOKUWA IMEJAA WAGONJWA WA KILA NAMNA, NA AKAPONYA MGONJWA MMOJA TU, ALIYEPOOZA KWA MIAKA 38, WENGINE WOTE HATA HAKUWASEMESHA WALA KUWAOMBEA (Yohana 5:1-14).

Kama Yesu alikwenda hospitali (kusanyiko la wagonjwa wanaosubiri uponyaji) mara moja tu, na akaponya mtu mmoja tu, wengine wooote wakabaki wakisubiri mfumo wa malaika kuja kutibua maji ili atakayeingia kwanza apone, ambao hauna tofauti na UPONYAJI KUPITIA MIKONO YA DAKTARI ambayo nayo ni njia ya Mungu kuponya watu wake sasa, INAKUWAJE WATU WANATAKA WATUMISHI WA MUNGU WENYE KARAMA NA HUDUMA ZA UPONYAJI WAJAE MAHOSPITALINI KUOMBEA KILA MGONJWA OVYO OVYO? YESU HAKUTUACHIA MFANO WA NAMNA HIYO KWENYE HUDUMA YAKE YOTE, HAKUPITA MAHOSPITALINI KUPONYA WAGONJWA, BALI WAGONJWA WALIKWENDA ALIPO NA WAKAPONYWA (Mathayo 8:16-17)!

Ikiwa Yesu HAKUPITA MAHOSPITALINI KUPONYA WAGONJWA, si lazima kwa mtumishi wa Mungu mwenye KARAMA NA HUDUMA YA UPONYAJI kufuata wagonjwa hospitalini eti awaombee wapone ili WATU WAPUUZI WASIOJUA KANUNI ZA UFALME WARIDHIKE NA KUSEMA KWELI HUYU ANATUMIWA NA MUNGU KUPONYA!

2. KWENDA HOSPITALI KUKAA KWA MASAA, SIKU KADHAA, WIKI, MWEZI NA HATA MIEZI AU MWAKA MZIMA UKISUBIRI UPONYAJI KUPITIA MIKONO YA MWANADAMU ALIYEPEWA KIPAWA CHA KUTIBU, HAINA TOFAUTI NA WALE WALIOKUWA “HOSPITALI” YA BETHZATA JAMII KUBWA YA WAGONJWA (NAMBA KUBWA YA WAGONJWA) WAKISUBIRI MALAIKA ATIBUE MAJI WAJITOSE (Yohana 5:1-14), TOFAUTI NI KWAMBA KULE ALIKUWA MALAIKA ANATIBUA MAJI YANAPONYA, HUKU HOSPITALI ZA SASA, MADAKTARI “WANATIBUA TIBA WALIZOPEWA KUGUNDUA KUHUSU AFYA NA MWILI” NA ANAYEZINGATIA MAELEKEZO YAO, ANAPATA TIBA NA MUNGU ANAMPONYA KUPITIA NJIA HIYO!

Hospitali kwa sasa, zinafanya kile ambacho kwenye YOHANA 5:1-14 KILIKUWA KIKIFANYWA NA MALAIKA lakini kupona au kutopona inabaki mikononi mwa mgonjwa kutegemea na KUTII KWAKE MASHARTI NA KUDRA ZA MWENYEZI MUNGU!

3. KITENDO CHA MGONJWA KUWA TAYARI HATA KULAZWA SIKU KADHAA, WIKI, MWEZI, MIEZI HATA MWAKA HOSPITALINI AU HATA KUPASULIWA KUONDOA VIUNGO, AU KUWEKEWA VIUNGO AKIWA HAJITAMBUI, NA ANAMRUHUSU DAKTARI KUMFANYIA LOLOTE, AKIAMINI DAKTARI ATATUMIWA NA MUNGU KUMPONYA, “KINAONESHA WAZI” IMANI YAKE IMEELEKEZWA WAPI KWA WAKATI HUO!

Iko wazi imani yake iko kwa hospitali, daktari na fani ya utabibu KUWA SULUHU YA UGONJWA NA MARADHI YAKE na si WATUMISHI WA MUNGU WENYE NGUVU NA KARAMA ZA UPONYAJI, ndio maana yuko radhi akalale hospitali HATA WIKI, MIEZI hata kama daktari hayupo, au huduma ni mbovu, LAKINI ANAAMINI ATARUDI NYUMBANI MZIMA SIKU MOJA ISIYOJULIKANA!

HII NI IMANI KUBWA MNO, AMBAYO KAMA INGEKUWA HIVI HIVI HATA KWA KANISA, WATUMISHI WA MUNGU NA UPONYAJI WA KIUNGU (DIVINE HEALING), TUNGEJIONEA MIUJIZA YA KUSHANGAZA MNO IKITENDWA KWA JINA LA YESU KUPITIA WATUMISHI WAKE!

Mtu akishaamua kwenda KUPATA TIBA HOSPITALI akawa tayari kukaa pale masaa, siku kadhaa, wiki kadhaa au miezi kadhaa, AKISUBIRI TIBA NA UPONYAJI, kupitia watalaam wa afya ambao Mungu kawapa kipawa hicho, NI NGUMU KUMBADILI AKILI, MAAMUZI, IMANI NA MATARAJIO YAKE KUGEUKIA KWA MTUMISHI WA MUNGU ANAYEOMBEA ALIYEKUJA HOSPITALINI KUOMBEA WAGONJWA, maana KAMA ANGELIKUWA NA IMANI HIYO YA KUPONYWA KUPITIA MIKONO YA WATUMISHI WA MUNGU, ANGEWEKA KAMBI KANISANI AU NYUMBANI KWA MTUMISHI WA MUNGU KAMA ALIVYOKWENDA KUWEKA KAMBI HOSPITALINI AKISUBIRI UPONYAJI!

4. UPONYAJI KWA NJIA YA MADAKTARI NA SAYANSI TIBA NI MKONO WA MUNGU WA KUPONYA, KAMA AMBAVYO UPONYAJI KWA NGUVU ZA MUNGU ZA UPONYAJI NI MKONDO WA MUNGU WA KUPONYA (CHANNEL OF GOD TO HEAL), VYOTE VINALENGA KULETA UZIMA KWA MTU, LAKINI BAHATI MBAYA HUWEZI KUGAWA IMANI YAKO KWA VYOTE VIWILI KWA WAKATI MMOJA!

Ndio maana tunaona watu wengi huja kwetu watumishi wa Mungu wenye KARAMA, HUDUMA NA IMANI YA KUPONYA WAGONJWA baada ya kujiridhisha ya kuwa HOSPITALINI IMESHINDIKANA, HAKUNA TIBA YA TATIZO LAO, hivyo sasa wanakuwa HAWANA UCHAGUZI TENA INAWALAZIMU KUKIMBILIA KWENYE MKONDO HUU WA UPONYAJI KWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU, MAANA HAWANA TENA PA KUSHIKA KIBINADAMU!

Mtu huyu anayekubali kuwa SAYANSI TIBA IMEFIKA UKOMO WA KUNIPONYA, AUTOMATICALLY ATAINUA IMANI YAKE KWA NENO, JINA LA YESU, HURUMA, REHEMA NA NGUVU ZA MUNGU KUMPONYA MAANA HAKUNA MSAADA KWINGINE KOKOTE!

Lakini ukitoka wewe mtumishi wa Mungu na kiherehere chako KWENDA HOSPITALINI KUOMBEA WAGONJWA, unapoteza muda kwa sababu HAPO WANA IMANI YA KUPONYWA NA MUNGU KUPITIA HOSPITALI, ukienda kupeleka ya kwako ya KUPONYWA KWA NENO, NGUVU ZA MUNGU NA KARAMA ZA ROHO, WANAWEZA KUKURIDHISHA UOMBE TU KWA VILE WANA HOFU YA UGONJWA NA WAMECHOKA KUUMIA NA KUTESWA NA UGONJWA, LAKINI IMANI YAO HAIKO KWENYE UPONYAJI KUPITIA MIKONO YA MTUMISHI WA MUNGU, NDIO MAANA WAMECHUKUA VITANDA KABISA HOSPITALINI NA WANALIPIA NA PESA ZA MALAZI, WAKISUBIRI KUPONA KITABIBU!

Jitihada zako zote za KUWAONESHA UPONYAJI KUPITIA NGUVU ZA MUNGU ZITAPATA UPINZANI MKUBWA KWA SABABU “HII NI MIHIMILI MIKUU MIWILI” YENYE LENGO MOJA LA KUPONYA LAKINI, IMANI YA MGONJWA HAIWEZI KUGAWANYIKA, HIVYO KILA MMOJA UTAMFANYIA KAZI ALIYEWEKA IMANI YAKE YOTE ASILIMIA MIA!

5. MTU AKIFIA HOSPITALINI NI SIFA, KAFA AKIPAMBANA, KAYAPIGANIA MAISHA YAKE, LAKINI AKIFIA KANISANI “SHUTUMA, LAWAMA, MATUSI NA HATA KUSHTAKIWA NA KUFUNGWA KWA HUDUMA HUSIKA” VINAWEZA KUTOKEA!

Hii inaonesha wazi, MFUMO WA DUNIA hauko tayari KUUPOKEA MFUMO WA MBINGUNI WA UPONYAJI KUPITIA WATUMISHI WAKE, na hivi viwili havifanyi kazi pamoja kwa wakati mmoja!

Akifia hospitalini HATA KWA UZEMBE WA MATABIBU, KUKOSA HUDUMA, KUKOSA MADAWA, UHABA WA VIFAA TIBA, inaonekana mbele ya jamii KAFA AKIPAMBANA NA KAFIA ENEO SAHIHI lakini akifia kanisani ALIPOKUWA AKIOMBEWA, ujue hiyo ni kasheshe na vita kubwa kwa KANISA NA MTUMISHI WA MUNGU, WAKIDAI NI UZEMBE NA UJINGA, wasiwaze kuwa KIFO NI UAMUZI WA MUNGU KULIKO MAPENZI YA MWANADAMU, JAPOKUWA VIPO VIFO VYA KIZEMBE (kwa mujibu wa maneno ya watu)!

MPAKA PALE WANADAMU WATAKAPOIPA HESHIMA HUDUMA YA UPONYAJI, KAMA WANAVYOIHESHIMU NA KUIAMINI HOSPITALI, TUTAANZA KUONA MAMBO YA KUSHANGAZA YAKIFANYWA KWA JINA LA YESU!

6. MTUMISHI WA MUNGU ANAWEZA KUTANGAZA WATU WALETE WAGONJWA, WENYE MARADHI NA UDHAIFU WA KIAFYA, TENA WATAPONYWA BURE KWA JINA LA YESU, LAKINI ATAKUWA KAMA MTU ACHEZAYE MBELE ZA WANADAMU, KANA KWAMBA WAGONJWA HAWAPO, LAKINI WANALIPA HELA KUTIBIWA HOSPITALINI, NA HATA KUSAFIRI NCHI ZA MBALI KWA AJILI YA TIBA ZA KITABIBU!

Hiki ninachokisema nina uhakika nacho, UKITANGAZA IBADA YA UPONYAJI, unaweza usipate WATU WANAOUMWA KUJA IBADANI KUPONYWA, labda wale ambao WALIKAA MAHOSPITALINI, WAKAZUNGUKA KILA MAHALI PA TIBA, HAWAKUPATA SULUHU, SASA WANAONA TWENDE TU KWA YESU, TUKIPONA SAWA LAKINI HATA TUSIPOPONA BASI TUONDOKE DUNIANI VIZURI, TUKAMALIZIE MAISHA KWA YESU!

Mpaka pale WATU WATAKAPO HESHIMU HUDUMA YA UPONYAJI NA UWEPO WA MUNGU, KAMA MAHOSPITALI, HAWATAIONA NGUVU YA HUDUMA YA UPONYAJI!

MSISITIZO:

“NINAWAHESHIMU MADAKTARI, HOSPITALI NA UPANDE HUO WA TIBA, NI MUNGU ALIYEWAPA UJUZI NA HEKIMA HIYO ILI KUSAIDIA WATU WAKE, LAKINI NATAKA KUSEMA WAZI WAZI, THEY ARE LIMITED, YANAYOWAZIDI UJANJA, WAKUBALI MAPEMA NA WAWAELEKEZE WATU KUPATA MSAADA KWA YESU! KINGINE, WATUMISHI WA MUNGU, NI VEMA TUWAPE UFAHAMU WASHIRIKA WETU KUWA HOSPITALI NA SAYANSI TIBA SI VYA SHETANI, NI NJIA YA MUNGU KUPONYA PIA, HIVYO WANAWEZA KUPATA MSAADA HUKO, LAKINI WAKIONA MAJI YAMEZIDI UNGA, WAJE NA REPORT ZAO (MEDICAL REPORTS) MADHABAHUNI KWA MUNGU NA KWA WATUMISHI WA MUNGU, MAANA BADO SULUHU IPO…”

NB: KAMA UKO DAR ES SALAAM NA NI MGONJWA WA UGONJWA WOWOTE, AU UNA MGONJWA WA UGONJWA WOWOTE, NA UNATAKA KUJITHIBITISHIA YA KUWA WAGONJWA WANAWEZA KUPONYWA KWA JINA LA YESU KATIKA ULIMWENGU WA SASA, NINAOMBA TUWASILIANE ILI UJE (KAMA MGONJWA NI WEWE) AU UMLETE MGONJWA KWENYE IBADA ZETU ZA UPONYAJI.

Ni mimi,

Mchungaji Dickson Cornel Kabigumila,

Assembly Of Believers Church (ABC),

16/05/2019

0753 466 675

0655 466 675

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »