“MAJANGA KANISANI NA KUJISAHAU YA KWAMBA YESU ANAWEZA KURUDI SIKU YOYOTE NA MUDA WOWOTE NA CHANGAMOTO YA KUKUMBATIA UDHEHEBU NA UDINI HUKU KIROHO CHAKO KIMEKUFA”
PASTOR DICKSON CORNEL KABIGUMILA,
23/07/2021
(JIPE DAKIKA TANO ZA MUHIMU UTULIE KUSOMA ILI UIPONYE NAFSI YAKO YA THAMANI)
NDUGU YANGU WA THAMANI,
HIVI UNAKUMBUKA BWANA YESU ALISEMA “KURUDI KWAKE ITAKUWA KAMA VILE MWIZI ANAVYOVAMIA NYUMBA YA MTU MUDA, SIKU NA WAKATI AMBAO MWENYE NYUMBA HATARAJII?”
1Wathesalonike 5:2
Ufunuo 16:15
Mathayo 24:43
UNAISHI KILA SIKU NA UFAHAMU HUU AU WAKATI HUU UNAPOCHAT UPUUZI NA KUNAJISI MOYO WAKO UMESAHAU HILI? UNAPOTUMIA MUDA WAKO KUONGEA NGONO NA KUAMSHA TAMAA ZA MWILI UNAKUMBUKA HUU UKWELI AU UMEPOFUSHWA NA DHAMBI? USIJESEMA HUKUONYWA MAPEMA.
HIVI KAMA WEWE AMBAYE CHA MWISHO KUSHIKA KABLA USINGIZI HAUJAKUPITIA NI SIMU NA CHA KWANZA KUSHIKA UKIAMKA NI SIMU… UNAJIAMINI NINI HASA YAANI?
HUNA TENA UWEZO WA KUOMBA WALAU HATA SAA MOJA KWA SIKU ILA UNAKAA ONLINE NA UNATEMBEA NA POWER BANK ILI SIMU ISIZIME… UNADAI UKO BUSY, LAKINI MTU AKIPITA ONLINE ANAKUTA MEMES NA TAARIFA MBALIMBALI UTAFIKIRI NI MWANDISHI WA HABARI! OLE WAKO MAANA SIKU ILE ITAKUKUTA GHAFLA NA UTAKUWA UMECHELEWA, UTABAKI NA HAITAKUWA RAHISI KUINGIA UZIMANI!
UKO BUSY MITANDAONI MARA “MY LIFE MY RULES” AU TUSIPANGIANE VYA KUPOST… USIJALI, SIKU UKIFA GHAFLA AU YESU AKARUDI GHAFLA KAMA ALIVYOSEMA, NDIPO UTAKUMBUKA TULIVYOKUWA TUKIKUKAZANIA USOME SURA WALAU TATU ZA NENO KILA SIKU, UOMBE KWA KUMAANISHA (UKIWA UMEZIMA SIMU) WALAU MARA TATU KWA SIKU KAMA DANIELI (DANIEL 6:10), UPATE MUDA WA KUSIKILIZA NA KUTAZAMA VIDEO NA AUDIO ZA NENO LA MUNGU, KILA SIKU UPATE WALAU NUSU SAA YA KUANGALIA MOYONI MWAKO NA KUJIAMBIA UKWELI WAPI BADO UMEKWAMA NA KUGEUZA KUWA OMBI LA KUCHONGWA NA ROHO MTAKATIFU ILI YESU AJAPO USIJEKUWA KAMA WANAWALI WATANO WAPUMBAVU WALIOISHIWA MAFUTA KWENYE TAA (MATHAYO 25:1-14)!
USIUAMBIE MOYO WAKO UONGO
SIKU ZOTE JIAMBIE UKWELI.
KAMA UNAENDELEA NA DHAMBI YOYOTE SIRINI KAMA UMEOKOKA HAIFUTI UKWELI KWAMBA UMEWAHI KUWA MWANA WA MUNGU LAKINI IKITOKEA YESU AMERUDI AU UMEKUFA NA BADO UPO KWENYE MATAPISHI NA MATOPE HAYO YA DHAMBI, NIKUHAKIKISHIE HUWEZI KWENDA UZIMANI (2PETRO 2:20-22)!
MUNGU ANAWASAMEHE WASIOFICHA DHAMBI ZAO NA WALIOAMUA KWA DHATI KUACHA NA SI WANAOENDELEA NAZO KWA KISINGIZIO CHA TOBA ZA REJAREJA (MITHALI 28:13)!
MATHAYO 25:1-14 INAZUNGUMZA KWA HABARI YA WANAWARI 10, WATANO WENYE HEKIMA NA WATANO WAPUMBAVU!
WATANO WALIOINGIA HARUSINI NA BWANA HARUSI NA WATANO AMBAO WALILALA USINGIZI NA TAA ZAO ZIKAISHIWA MAFUTA WALIPOKUJA KUJIPAPATUA WAJAZE MAFUTA IKAWA TOO LATE TAYARI BWANA HARUSI AMEINGIA NDANI NA WALIOKUWA MACHO NA MLANGO UKAFUNGWA NA IKAWA KILIO NA KUSAGA MENO KWAO!
KUWA MWANAMWALI (KUOKOKA) HAITOSHI HAKIKISHA TAA YA MOYO WAKO INAWAKA NA UKO MACHO KUMPOKEA YESU AKIRUDI MUDA WOWOTE HATA UKIWA USINGIZINI! TUACHE WOKOVU WA IBADA HADI IBADA WA MAIGIZO! YESU ATARUDI GHAFLA NA WENGI HAWATAINGIA UZIMANI!
KUNA NDUGU MMOJA KATIKA KRISTO NA MTUMISHI TU MZURI WA KRISTO KANIFUATA INBOX KUNIAMBIA KWAMBA NAWATISHA WENYE DHAMBI NA SIWAONESHI UPENDO NA NAWAFOKEA, NIKAMJIBU TU KWA UPENDO YA KWAMBA, “KUFOKA FOKA HUKU, KUWATISHA HUKU KWA UKWELI ULIO WAZI KWENYE MAANDIKO KUMEZALISHA MATOKEO YA WATU WALIOTOKA DHAMBINI NA KUWA WANA WA MUNGU KWELIKWELI BADALA YA KUJITIA MOYO KWENYE NEEMA BILA MABADILIKO YA UTU WA NDANI NA TABIA NA MWENENDO KAMA WANA WA NURU”
NIKAMTIA MOYO AENDELEE KUWAFIKIA WENYE DHAMBI KWA LUGHA YAKE NZURI, YA UPOLE KIKUBWA AVUNE WAJE KWA YESU KWELI KWELI, NA MIMI NITAVUNA WA KWANGU KWA LUGHA YANGU HII HII, KILA MMOJA AWE BUSY NA MRABA WAKE!
UNAJUA MAMBO MENGINE YANACHEKESHA SANA!
UNAWEZAJE KUSEMA BWANA YESU ASIFIWE KWA UJASIRI KABISA HUKU UNAENDELEA NA ZINAA? ANASIFIWA KWA LIPI HAPO ILHALI IKITOKEA UMEKUFA AU AKARUDI GHAFLA HUENDI MBINGUNI MAANA HAKITAINGIA CHOCHOTE KILICHO KINYONGE KATIKA MJI ULE? UNAWEZAJE KUSEMA BWANA YESU ASIFIWE WAKATI MIKONO YAKO IMEJAA MBEGU ZA KIUME KAMA MATOKEO YA KUJICHUA (MASTURBATION) AU UNAJIINGIZIA VIDOLE KAMA BINTI AU MWANAMKE ILI KUJIRIDHISHA? UNA MAANISHA YESU YUPI UNAYEMSIFIA BADALA YA KUANGUKA MIGUUNI PAKE AKUFUNGUE TOKA DHAMBI HIYO NA TABIA ISIYOFAA? ILE KWAMBA HAKUNA ANAYEKUONA, HAIMAANISHI UKO SALAMA! UKWELI WEWE NI MTUPU MBELE ZA MUNGU,TUBU.
HIVI NI NANI ALIYETULOGA NA UDHEHEBU/ UDINI SISI WALIOOKOKA?
●UKO KANISA FULANI MASOMO KUHUSU UTAKATIFU, USHINDI DHIDI YA DHAMBI, UADILIFU, MAISHA YA USHUHUDA NA MWENENDO UIPASAYO INJILI, KURUDI KWA YESU, UZIMA WA MILELE NA MAISHA BAADA YA KIFO NI NADRA AU HAKUNA KABISA, LAKINI UMENG’ANG’ANIA KANISA/ DHEHEBU LAKO HUAMBIWI KITU YAANI…. NAFIKIRI UNA MATATIZO YA AKILI NA HUJAWAHI KUWAZA KUHUSU UMILELE YA KWAMBA UKIENDA MOTONI NI MILELE NA HAUTATOKA MILELE… WEWE ENDELEA KUKUMBATIA DHEHEBU LENU HADI MOTONI, SIKU UKIJA KUELEWA DHEHEBU SI KABILA WALA TAIFA LAKO UTAKUWA UMECHELEWA KUTOKA!
UTASIKIA MTU MMOJA ANAYECHEZEA KAMARI ROHO YAKE ANASEMA, “NASALI SEHEMU (DHEHEBU FULANI) NA NI MWENYEKITI WA VIJANA LAKINI UZINZI UNANITESA MNO, SIWEZI KUMWAMBIA MCHUNGAJI WANGU KABISA MAANA ANANIAMINI SANA, NIMEONA WEWE PASTOR DICKSON UNAWEZA KUNISAIDIA…”
UKISHAMSAIDIA ANAKWAMBIA NABAKI HUKU HUKU, BAADA YA MUDA ANARUDI ANASEMA NAONA TENA ILE HALI INATAKA KURUDI AU IMENIRUDIA AU TAYARI NIMEANGUKA TENA, LAKINI TANGU MAPEMA MOYO WAKE UNAMJUA MCHUNGAJI SAHIHI ANAYEWEZA KUMLEA KWENYE NJIA SAHIHI LAKINI UDHEHEBU, VYEO, KUIMBA AU HUDUMA INAMFANYA ABAKI MAHALI AMBAPO HAKUNA NGUVU YA KUMTUNZA MBALI NA DHAMBI… HIVI HUU UJINGA UTAENDELEA NAO MPAKA LINI RAFIKI YANGU? YAANI WEWE HUONI KWAMBA HUPASWI KUKAA HUKO TENA? 😭
HUONI KWAMBA HAKUNA CHAKULA NA MALEZI YA KUKUTUNZA MBALI NA DHAMBI NA UOVU? USIIPENDE DINI/ DHEHEBU KIASI CHA KUWEKA REHANI ROHO YAKO AU KUFA KIMYA KIMYA NA DHAMBI KIASI HUDUMA AU CHEO!
MWINGINE UTAMSIKIA ANASEMA, “PASTOR DICKSON MIMI NI MWANAFUNZI WAKO WA SIRI, NAJENGWA MNO NA UMENIVUSHA MNO, MUNGU AMEKUTUMIA KUNIFANYA BORA NA WA KUWAFAA WENGI, KUPITIA MASOMO YAKO STATUS, YOUTUBE NIMEACHA UZINZI NA MAISHA YA MICHANGANYO LAKINI KUJA HUKO KUKAA JUMLA NA KULELEWA SITAWEZA KWA SASA MAANA HAPA KANISANI NIKO PRAISE AND WORSHIP AU NI SHEMASI AU NI MZEE WA KANISA AU NINAONGOZA KIKUNDI CHA WAOMBAJI”
UNAMUANGALIA UNAISHIA KUMSIKITIKIA TU! HAYA MA NAFASI NA VYEO HAYANA MAANA KAMA HAUKUTANI NA NENO LA MUNGU LINALOBADILISHA MOYO WAKO NA NAFSI YAKO! SIKU ILE YA MWISHO VYEO, HUDUMA HAVITAKUWA NA MAANA! USIKAE MAHALI AMBAPO HAKUNA MCHUNGAJI ANAYEUPENDEZA MOYO WA MUNGU ANAYEKULISHA KWA UFAHAMU NA MAARIFA SAHIHI YA NENO (YEREMIA 3:15, YOHANA 21:15-17)!
NB: KUPATA MASOMO YANGU KUTOKA STATUS WHATSAPP SAVE NAMBA YANGU 0655 466 675 NA KISHA NJOO INBOX HUKO HUKO WHATSAPP UNIPE MAJINA YAKO KAMILI NISAVE UANZE KUSOMA MOJA KWA MOJA!
RUKSA KUSHARE UJUMBE HUU NA WATU WENGINE KADRI UWEZAVYO ILI WA KUPONA WAPONE NA KUIMARISHA MAHUSIANO YAO NA MUNGU!
PASTOR DICKSON CORNEL KABIGUMILA,
ASSEMBLY OF BELIEVERS CHURCH (ABC) GLOBAL,
23/07/2021.
YOUTUBE: PASTOR DICKSON CORNEL KABIGUMILA
INSTAGRAM: @mwalimukabigumila
FACEBOOK: Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila
WhatsApp: 0655 466 675
Mafundisho
SEX BEFORE MARRIAGE
#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo