LUGHA ZINAZOMFURAHISHA SHETANI KILA WAKATI UNAPOZISEMA.

( Hizi Ndio Lugha Zinazofunga Maisha yako Siku Hata Siku, kila unapoamka ndio mambo kama vile yanaharibika)

Zinahamasishwa na shetani mwenyewe
( Na Zinamuhuzunisha Roho wa Mungu )
LUGHA Hizi ni kama za kawaida sana na tumezizoea ni kama vile ni sehemu ya maisha yetu, kwahiyo unajisikia kawaida tu unapozisema.

Lakini Brother and Sister
Hakuna kitu unakisema kwa Kinywa chako ambacho kitaenda Bure “ Huo ni Mtego pekee wa kukunasa ”

#Mathayo 12:36-37
[36]Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.
[37]Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.

#Mithali 18:21
[21]Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.

#Mithali 6:2
[2]Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako,
Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,

LUGHA HIZO NI HIZI

1. Yaan Sijui hata itakuwaje
“ Hii ni lugha ya kushindwa )
“ Umesahau Warumi 8:28 ”

2. Nimechanganyikiwa yaan!!!;
Jua kabisa Hauko na Mungu, Kwasababu Mungu hafanyi kazi na waliochanganyikiwa.
“ Umesahau Wafilipi 4:13 ”

3. Sijui Huu ugonjwa utaondoka lini ?
Hata kama unalia, haitafanya kazi
“ Umesahau Mathayo 8:17 – Yeye Mwenyewe ameyachukua Magonjwa yetu, Ameutwaa Udhaifu wetu ”
ulipaswa kusema “ Bwana Yesu Ulichukua ugonjwa wangu ili mimi nisiwe mgonjwa, Ninaamini Bwana na ninapokea Uponyaji wangu kwa Jina la Yesu.

4. Mambo hayaendi yaan, kila nikigusa ninafeli
“ Hii ni lugha ya kushindwa ”
“ Umesahau Warumi 8:31, 37 – Katika mambo yote tunashinda na zaidi ya kushinda ”

5. Muda Umeenda kweli, na Hata Siolewi
“ Umesahau Mungu alimfanyia muujiza Sara akiwa na miaka 90, unafikiri Mungu amechelewa kwako Mwanzo 21 ”

6. Nimekosa kazi “ Nimepeleka makampuni Yote sijaitwa kazini ” Hata Sijui nifanyeje
“ Unafikiri Mungu ameshindwa kukupa Kazi
kuna wakati anahitaji kukupa Wazo ili wewe uajiri wafanyakazi hata 20 ”

7. Hii hali Inaniua
“ Umesahau Zaburi 118:17 – Sitakufa Bali Nitaishi ”

Hizi Lugha ni kama za kawaida
lakini ndizo zinazompa shetani
uhalali wa kutesa maisha yako
uko hivi ulivyo ni kwasababu
ya yale unayoyasema kila mara.

Mungu anafanya pale Imani yako
inapokuwa hai juu ya kile alichokisema
sio kwasababu ya kulia kwako na kulalamika kwako.

Malalamiko na vilio na huzuni havijawahi kumsukuma Mungu kufanya kitu.

IMANI YAKO IWE HAI
JUU YA KILE MUNGU AMESEMA
HAPO UTAANZA KUUONA USHINDI

HIZI NI LUGHA ZA WATU WALIOSHINDWA
NA WANAOENDELEA KUSHINDWA

KUANZIA LEO UNASOMA POST HII
Kataa kushindwa, kataa kuzungumza lugha za kushindwa, kataa kuzungumza lugha za hofu na Mashaka.

ANZA KUKIRI KILE YESU AMEFANYA KWA AJILI YAKO HUKU UKIAMINI UYASEMAYO YANATUKIA ( Marko 11:22-24, 2 Wakorintho 4:13)

God bless you
Pastor Ibrahim Amasi
ABC – KAHAMA

LivingWord
@2019