KWANINI MWILI WA MAREHEMU ULIPAKIWA KWENYE NDEGE YA MIZIGO NA SIO NDEGE YA ABIRIA? NA KWANINI WALISEMA MWILI WA MAREHEMU UTASAFIRISHWA NA SIO MAREHEMU ATASAFIRISHWA KUPELEKWA KIJIJINI KWAO?

Ndugu zake na rafiki zake, walitarajia angerudi salama, lakini bahati mbaya alifia ughaibuni!! Walipotaka kuusafirisha mwili wake, hawakuupakia kwenye ndege ya abiria, badala yake ulipakiwa kwenye ndege ya mizigo. Na ulipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius K. Nyerere jijini Dar, ndugu zake, na marafiki zake, hawakwenda kumpokea sehemu ya kupokelea abiria, ila walikwenda kuupokea mwili wake, sehemu ya kupokelea mizigo (cargo).

Yaani alikwenda ughaibuni kwa ndege ya abiria, akarudishwa Tanzania kwa ndege ya mizigo. Alipokelewa na wenyeji wake huko ughaibuni sehemu ya kupokelea abiria, akapokelewa hapa nyumbani kwao Tanzania na ndugu na marafki zake, katika eneo la kupokelea mizigo (cargo). Kwa maana nyingine alikwenda kama mtu, akarudi kama mzigo, ndio maana wakati wa kwenda alipanda kwenye ndege ya abiria, na wakati wa kurudi alipakiwa kwenye ndege ya mizigo.

Alikuwa anasifika kwa urembo wake, alikuwa akirushia picha zakz FB na INSTA akiwa amevaa vinguo vinavyoonyesha matiti, na makalio yake makubwa, leo hii amerudishwa Tanzania kwenye ndege ya mizigo. Mwili wake umegeuka kuwa mzigo (cargo) na kuna jina limeongezeka tena kabla ya jina lake alilopewa na baba yake na mama yake, jina hilo ni marehemu. Hivi sasa anaitwa marehemu.

Mwili wake uliokuwa unawavutia wanaume wa kila rangi, sasa hivi umepoteza thamani yake. Hakuna tena mwanaume anayeutamani mwili wake, ingawa bado haujaanza kunuka, wala haujapoteza ule mvuto uliokuwa nao kabla roho haijaondoka na kuuacha mwili. Wapenzi wake aliokuwa amewapanga kama foleni ya kwenda kupiga kura, hakuna hata mmoja anayetamani kulala naye tena. Hapo ndipo nilipojifunza kuwa thamani ya mwili ni roho, na mwili pasipo roho ni kama limdoli tu (mwanasesere). Maandiko yanasema “…..mwili pasipo roho umekufa…….(Yakobo 2:26).

Haijalishi wewe ni mzuri kiasi gani, au mtanashati, kiasi gani, thamani ya mwili wako inatokana na roho iliyoko ndani yako. Siku roho yako ikiondoka na kuacha mwili wako, ndipo na thamani ya mwili wako inaishia hapo. Kama uko nje ya nchi ukafia huko, na ndugu zako wakaamua kuisafirisha maiti yako, ujue kuwa haitapakiwa kwenye ndege ya abiria, itapakiwa kwenye ndege ya mizigo. Hata kama ikipakiwa kwenye ndege ya abiria, haitakalishwa na abiria wengine, itawekwa kwenye sehemu ya mizigo; kwanini? Kwa sababu mwili hauna thamani pasipo roho!! Roho inapoondoka na kuuacha mwili, mwili huo hugeuka na kuwa mdoli, ambao muda si mrefu huanza kunuka na kutoa funza.

Sikiliza ndugu, wewe halisi sio huo mwili wako, wewe halisi ni nafsi na roho iliyoko ndani ya mwili wako. Ndio maana mtu anapokufa yaani roho yake inapoucha mwili, na ndugu zake wakaamua kuisafirisha maiti kuipeleka kijijini kwao utasikia wakisema “MWILI WA MAREHEMU UTASAFIRISHWA KWENDA KIJIJINI KWAO”. Ni kwanini wanasema mwili wa marehemu utasafirishwa na sio marehemu atasafirishwa? Ni kwa sababu marehemu mwenyewe (roho na nafsi) hayupo, ameondoka na kuucha mwili wake. Hivyo kinachosafirishwa sio marehemu, ila ni mwili wa marehemu.

Sikia binti, uzuri wako unaoringia, na wewe kijana utanashati wako unaoringia, wanakuita handsome boy (H.B), ukisimama kwenye kioo unajiona wewe ndio wewe, hivyo vyote havina thamani roho yako inapouacha mwili wako. Huo mwili wako unaoringia pamoja na uzuri wake, ukiambiwa uokoke unasema binti mzuri kama mimi siwezi kuokoka, handsome boy kama mimi siwezi kuokoka, siku roho yako ikiuacha mwili wako (ukifa) unageuka kuwa uchafu, baada ya muda mfupi utanuka na funza wataanza kutoka katika huo mwili. Hii ni kwa sababu mwili wako hauna thamani pasipo roho. Acha kuringia uzuri wako. MWILI WAKO SIO WAKO NI NYAMA YA UDONGO!! HUO MWILI USIKUDANGANYE DADA, HUO MWILI USIKUDANGANYE KIJANA, UTAUACHA CHINI YA UDONGO, NA WEWE (ROHO) UTASIMAMA MBELE YA KITI CHA HUKUMU ILI KUJIBU NAMNA ULIVYOUTUMIA HUO MWILI UKIWA DUNIANI. MPOKEE YESU SASA UKIMBIE HUKUMU YA MILELE!!

SHALOM ALEICHEM.

Mchungaji na Mwalimu Pst Gibson Gondwe

UKITAKA MASOMO YANGU KWA NJIA YA WHATSAPP UNAWEZA KUNITUMIA NAMBA YAKO KWENYE HIYO NAMBA HAPO CHINI. LAKINI PIA UKITAKA NIKUUNGE KWENYE GROUP LANGU LA WHATSAPP AMBAMO NINAFUNDISHA MASOMO MBALIMBALI YA NENO LA MUNGU PIA UNAWEZA NITUMIA MESEJI KUPITIA HIYO NAMBA HAPO CHINI.

+255 764 436 087.

KARIBU UABUDU PAMOJA NASI

C.A.G KINGS CHURCH.

NYAMHONGOLO.

MWANZA.

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »

NDOA

Haikuanzishwa Na WANADAMU Bali MUNGU Ndiye Aliyeanzisha TAASISI HII… Imeanzishwa Na MUNGU Ambaye Ni Roho, Uwe Na Uhakika Haiwezi Kuendeshwa Kwa Kutegemea AKILI, HEKIMA NA

Read More »

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »