KUUSHINDA UDANGANYIFU WA SHETANI KWA KWELI YA KRISTO NDANI YETU

(Soma vizuri sana ujumbe huu,utapata KWELI ya Kristo YESU ndani yako)

1.UDANGAYIFU (HILA ZA SHETANI) KUPITIA TEKNOLOJIA na MAMBO YA DUNIA HII.

Na hapa Inahusisha wasomi wa dunia hii,

Ninafurahi kwanza kwamba Hila hizi Tunazishinda! Na wewe Unashinda katika Jina la Yesu!

Kumekuwa na Udanganyifu na hila za Adui shetani DHIDI ya Kanisa,DHIDI ya wanadamu ili wasiifikilie KWELI.

Imeandikwa *”Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.”* Waefeso 6:11

Maana yake hila za Shetani zipo, na tumepaswa kuzishinda!

Shetani anapofusha Akili za watu,kwa lengo la wasiipokee KWELI ya Kristo Yesu, na waliowachanga wa imani waanguke na kupotea,hata baadhi ya wateule wapotezwe na wimbi la Udanganyifu huu.

Siku hizi tunaona mitandao na wasomi wanavyotumia nafasi zao “Yani Shetani ndiye anayewatumia”kuleta MAARIFA na Elimu inayopingana na KWELI ya Kristo Yesu moja kwa moja!

Imeandikwa *”nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.”* 2 Timotheo 4:4

Sasa Kundi la watu wanaanza kuugeukia UONGO,na hapa Kundi kubwa linaloathiriwa ni Vijana, na Wanaacha iliyo KWELI!

Kuna mafundisho na falsafa za kidunia ambalo zikiletwa kwa watu ni UADUI KABISA na KWELI ya Kristo YESU.

Ninaomba uoni mfano wa mambo haya,;

1.Kwa Mfano ” Ni mewahi KUKUTANA na “article” mtandaoni sio Mara moja,hata wewe utakuwa umewahi kuona,na kusikia pia habari hii inasema *”MADHARA YA KUTOKUFANYA NGONO MUDA MREFU”*

Unaona wanaandika kabisa “BINTI ANAYEKAA NA MIAKA 18-24 BILA KUFANYA NGONO YUKO HATARINI”

(Hoja hizi hazina Ukweli,kiafya wala Kiroho,NI UONGO MTUPU WA ADUI SHETANI KUPITIA MAWAKALA WAKE walioko hapa DUNIANI)

Jaribu kufikiri,Kijana alibaleghe, BINTI aliyevunja Ungo, anakutana na ujumbe huu,

*Lazima AKILI ITASHTUKA* na kushtuka huko Shetani anaweza akawa ameshapata nafasi ya kuingiza mawazo machafu na hata kupelekea KUKUFANYA MZINZI,MWASHERATI na MTENDA DHAMBI.

Jumbe hizi zimekusudia Kuuwa, na Kuwapoteza Walio wengi.

Ni nakumbuka ,*”BINTI mmoja alikuwa anasumbuliwa na aumivu ya tumbo akiwa katika siku zake, na Akasikia kwa wenzake wakisema ni Kwasababu “Hajawahi kutana na Mwanaume”

Na hii ikawa inamshawishi sana,kila anapopata maumivu, akafikiri kuhusu vijana wanaomsumbua Mara kwa Mara,akaamua Kukubali “Kumfanya UCHAFU” na hii ni Matokeo ya Udanganyifu wa Shetani kupitia falsafa potofu za kishetani.

Swali ni MABINTI /VIJANA wangapi wameangukia kwenye dhambi na UCHAFU kwasababu ya mafundisho potofu,hoja za Uongo kama hizi?

Vijana ambao wanashinda mtandaoni tu,hata mlango wa Kanisa hawajui,au ni jumapili kwa jumapili,Je TUMEPOTEZA VIJANA WANGAPI ?

Kuna msaada wowote kwenye makanisani wanayosali,ikiwa hakuna semina za kuwafundisha iliyo KWELI,? Na semina zikiwepo tunafundishwa “Ujasiriamali tu”,

Kunajambo la Kufanyika hapo WATUMISHI WA MUNGU!

2.Mfano MWINGINE, ” Unakuta article inasema *”KUPIGA PUNYETO (MASTURBATION) NI AFYA,HAINA MADHARA”*

(Yaani yupo Mtu “anachapisha article kama hizo, na ni msomi KABISA,tena Mkristo,)

Unahamasisha UCHAFU ambao unamaliza vijana isivyokawaida,Uovu kama huu ambao umewafunga vijana minyororo hawawezi kufurukuta,wamekuwa mateka na watumwa wa kuangalia picha za uchi na kumfanya michezo MICHAFU!

Najiuliza sasa,Kijana ambayo Anapigana ashinde ” ADDICTION ” Hii,alafu anakutana na “ujumbe” kama Huu, sindio utaamsha uhalali wa kufanya UCHAFU huu!??

Hivi aliyeandika maana yake “Anahamasisha watu wafanye pasi na mashaka”

Sasa watu Akili zao zinapigwa Giza wanafuata tamaa za dunia hii,

Imeandikwa Waefeso 4:18-19

*”ambao; akili zao zimetiwa giza, nao wamefarikishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao;”*

4:19 *”ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani”*

*”UCHAFU na Kutamani”* ni matokeo ya Akili kupigwa Giza,na Fikra zinapigwa Giza na mafundisho potofu,mungu wa dunia hii(shetani) ,falsafa za UONGO na Hoja za Udanganyifu!

UKWELI NI HUU!

Usiamini wala Kusikiliza “Mafundisho yasio KUBALIANA NA NENO LA MUNGU KATIKA USAFI,HAKI,UTAKATIFU na MEMA”

Hata kama ataongea RAIS,PROFESSOR, LECTURER, MWALIMU,DAKTARI,au Mtu yeyote kwa taaluma yeyote, maneno na hoja zake usizipime kwa “CHEO” Chake,au “UMAARUFU” wake ,au “ELIMU” yake BALI yapime kwa NENO LA KRISTO YESU ,Yani “KWELI YA MUNGU”

VIJANA fanyeni BIDII katika NENO,sio hizi blaablaa za WhatsApp, Instagram, Google,utube n.k!

“Mafundisho haya ya Uongo” ni hila za shetani,ni Sumu inayouwa taratibu!!

Tia Bidii katika KRISTO YESU!

Neno lake Ni KWELI itakasayo!

*”Uwatakase kwa ile KWELI,na Neno lako ndiyo KWELI”*

(Somo linaendelea namba 2)

Prophet Allen Adiel

RGG INT’L MINISTRY

“NEEMA ya Mungu inatutosha”

0756008730

Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »